Mheshimiwa IGP,
Watanzania wengi wanaupongeza uongozi wa jeshi la polisi kwa hatua ya kuwafikisha mahakamani vijana wanne, yaani Clinton Damas (Askari wa JWTZ Na. MT. 140105), Amin Lema, Nickson Jackson na Praygod Mushi (Askari Magereza na. C.1693).
Vijana hawa ni kati ya watu watano, waliofanya shambulio la kimwili katika mdommo, kumma na mkunndu wa binti wa Yombo Dovya ("JM") kwa kutumia mmboo zao zilizodisa kumwingilia kimwili.
Kitendo hiki kilifanyika kikiwa na sura ya adhabu ya kivita ambayo kwa kawaida huwa inatolewa kwa njia ya ngono-shuruti dhidi ya mlengwa, na katika tukio la sasa dhidi ya binti asiye na hatia.
Adhabu hii dhidi ya binti yule ilikiuka haki za "JM," kwa sababu "JM" ni mtu kamili kama watu baki, yaani "JM" ni nafsi ya utendaji ambayo ni ushirika wa mwili na roho, roho yake ikiwa inajumuisha akili, utashi na hisia.
Hivyo, "JM" alinyimwa haki ya kuheshimiwa kwa "ukuu wa nafsi ya kiutu" aliyo nayo yeye, kama mtu, yaani "
the right to personal sovereignty."
Kwa mujibu wa haki hii, "kila mtu mwenye akili timamu ni nafsi yenye haki ya kufikiri juu ya mbinu na malengo yake, kuamua juu ya mbinu sahihi za kufikia malengo aliyojiwekea, na kisha kufanya utekelezaji huru wa mbinu alizojichagulia, akiwa anafanya yote haya kwa uhuru kamili pasipo kuulizwa na mtu yeyote baki mwenye nafsi iliyo na hadhi ya kimaumbile iliyo sawa na hadhi yake."
Kwa maneno mengine, katika ulimwengu wa sheria, msingi wa "kanuni ya ridhaa," au "kanuni ya ridhio la moyoni," ni ukweli kwamba kila mtu, bila kujali kama ni mwanamke au mwanamume, anayo haki asilia ya kuheshimiwa kwa ukuu wa nafsi yake, kwa maana kwamba anayo haki ya kutoguswa kwa namna yoyote na mtu baki mpaka hapo atakapotoa "ridhaa" ya wazi ya kuguswa.
Kwa sababu hizi, kuna dosari kuu tatu zinazojitokeza na zinazoweza kuufanya weledi wa Jeshi la polisi kutiliwa mashaka kwa sababu ya namna yake ya kushughulikia tukio hili.
Mosi, tayari uchunguzi wa kipolisi umethibitisha katika upeo usio na shaka juu ya wasifu wa mtu aliyewatuma vijana hawa kufanya uhalifu huu.
Ushahidi usiokanushika uko hivi:
- Namba ya simu iliyokuwa inatumiwa na binti aliyebakwa imepokelewa na jeshi la pilisi;
- Binti aliyebakwa kataja namba ya simu ya mwanaume aliyekuwa anatongozana naye tangu mwanzo;
- Kitengo cha makosa ya mtandao kinao weledi mkubwa wa kukusanya ushahidi wa kielektroniki kwa kutimia taarifa za miamala ya hizi namba za simu, zenye kujumuisha taarifa za minara ya simu iliyotumika wakati wa mawasiliano, namba ya IMEI, namba zote zilizowahi kutumiwa kwenye simu yenye IMEI husika, na taarifa baki kadhaa;
- Mwanaume aliyekuwa anamtongoza huyu binti amemtaja "mke" wake huyo kwa jina; na
- Vijana waliofanya ubakaji wamemtaja "bosi" wao huyo kwa jina, yaani mtu aliyewatuma.
Lakini bado "afande" huyo hajaunganishwa kwenye kesi.
Pili, kuna watuhumiwa wawili hawakufikishwa mahakamanui kwa sababu hawajakamatwa hadi leo. Katika taifa hili ambako kila kilometa moja ya mraba kuna afisa nusa nusa wa serikali, yaani "government security officer" (GSO), haiyumukiniki kwamba Jeshi la Polisi limeshindwa kazi yake ya “kusaka, kukamata, kuhoji na kuwafungulia mashtaka” watuhumiwa hawa.
Kwa sababu ya pengo hili sasa imejengeka tena hisia kama ile iliyoanzia kwenye kesi ya Jamhuri dhidi ya Abdallah Zombe na Wenzake 12, yaani, Kesi Na. No. 26 ya mwaka 2006.
Katika kesi hii Zombe alichomoka kwa sababu mhusika mkuu aliyepokea na kutekeleza maagizo ya mauaji kutoka kwa Zombe, yaani CPL Saad, alilazimishwa kuwa “mgeni wa Mungu” kwa kukatiwa "tiketi ya kwenda mbinguni" kabla ya kufika mahakamani kusomewa mashtaka na kutoa ushahidi wake.
Hofu ya umma ni kwamba hawa vijana ambao hawajaunganishwa kwenye kesi hii ya binti wa Yombo wanaweza kukatiwa "tiketi ya kwenda mbinguni" kabla ya kufika mahakamani kusomewa mashtaka na kutoa ushahidi wake, kama ilivyokuwa kwa yule CPL Saad.
Na tatu, hati ya mashitaka hakutaja mashtaka yote yanayohusiana na tukio.
Makosa mengi yamepuuziwa. Hujambo Kuna kosa la utekaji, kufanya ngono na binti aliye na umri chini ya miaka 18, shambulio la kimwili kwa kutumia chupa, na kusambaza maudhui yaliyokatazwa kisheria.
Ukiweza kurekebisha dosari hizi tatu, basi, hii hiyo itakuwa ni hatua kubwa katika kujenga Imani ya jamii kuhusu umakini na weledi wa Jeshi la Polisi.
Nimalizie kwa kufupisha maudhui ya kifungu cha 22 cha Sheria ya “Mkusanyiko wa Kanuni za Adhabu,”hapa chini, ili wasomaji wasio na muda wa kupekua aya zote za “Kanuni ya Adhabu” wasikwame. Kifungu hiki kinasema mambo manne:
- Mosi, mashtaka dhidi ya mtu aliyeshawishi wenzake kutenda kosa yanaweza kuendelea bila mtenda kosa halisi kushtakiwa kwanza;
- Pili, mashtaka dhidi ya mtenda kosa halisi yanaweza kuendelea bila mtu aliyeshawishi wenzake kutenda kosa hilo kushtakiwa kwanza;
- Tatu, mashtaka dhidi ya mtenda kosa halisi na dhidi ya mtu aliyeshawishi wenzake kutenda kosa yanaweza kuendelea kwa wakati mmoja kupitia kesi moja.
- Na nne, ushahidi wa kesi unanoga pale mtenda kosa na mtu aliyeshawishi kosa litendeke wanapounganishwa kwenye kesi moja kwa wakati mmoja.
Ni kwa sababu hii, Watanzania wanaomba sana mtu aliyeshawishi wale vijana kufanya ubakaji wa mdomoni, ukeni na matakoni dhidi ya yule binti wa Yombo, Dar, kuunganishwa kwenye kesi hii kupitia ofisi ya DPP.
Picha za baadhi ya watuhumiwa katika sakata hili ni hizi hapa:
Watuhumiwa wanne wa ulawiti wakiwa mahakamani: Clinton Damas (Askari wa JWTZ), Amin Lema, Nickson Jackson na Praygod Mushi (Askari Magereza)
Assistant Superintendent of Police (ASP), Fatuma Kigondo, Afande anayetuhumiwa kuwatuma walawiti
Nakutakia utendaji kazi mwema,
Dr. Mama Amon,
"Sumbawanga Town,"
P.O.Box P/Bag,
Sumbawanga,
Tanzania.