Mramba achaguliwa Mwenyekiti Bodi ya TANROADS MKOA.

Mwacheni afanye alichoagizwa.mmesahau mliambiwa kwamba tu wavivu wa kufikiri?
Sijui kama hili lina hitaji msomi wa chuo kikuu kuona mambo yanaenda ndivyo sivyo.Tumsaidie Kikwete kuimaliza CCM machoni mwa wananchi kuelekea 2010
hivi wewe upo kambi gani vile?😀
 
If that happened in Tanzania, then it doesn't surprise me.
 
MBUNGE wa Rombo, Basil Mramba, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Kilimanjaro.


Atafanya ziara jimboni kwake Rombo na sehemu nyingine mkoani Kilimanjaro kuelezea mikakati ya TANROADS kwa miaka ijayo...i hope you all know where this is heading.
 

Kwa bahati mbaya waTanzania na takriban Africa nzima bado hatujaweza ku-pinpoint MAMA au kichwa cha matatizo tuliyonayo. Tunafirkiri matatizo ni:

1. Hali ngumu ya maisha, kifedah na kiuchumi
2. Rushwa iliyotapakaa kila idara
3. Ubaguzi/Upendeleo wa kikabila/kidini n.k
4. Udhalilishaji wa kijinsia/ulemavu n.k

Kwa kifupi haya yote si matatizo. Haya na mengineyo ni matokeo tu ya tatizo kichwa/mama tulilonalo ambalo ni VIONGOZI MAFISADI . Hili ndio tatizo kichwa/mama tulilonalo. Kutokana na wao kujikusanyia kila kitu, mambo haya hupatikana:

1. Tabaka hujengeka baina walionacho na wasionacho (matajiri na masikini) pasipo uhalali wa utajiri na umasikini huo. Mafisadi wanakwapua/wanalipana pasipo uhalali wala usawa zaidi ya wanavyostahili au kuhitaji wakati wadhulumiwa wanakwapuliwa pasipo uhalali wala usawa chini ya kiwango wanachostahili.

2. Hii inapelekea mafisadi ku-indulge katika "luxuries" and "lavishness" na walalahoi kuingia katika hali ya "desperation". Desperation ambapo mtu anavuja jasho jingi lakini kipato kidogo kiasi cha kutokuwa tena "kazi ndio kipimo cha akipatacho na utu wake" Ili ku-survive, ina maana afanye lolote lile kupata angalau basics. Nini matokeo yake???

3. Katika hali kama hii, Mwenyezi Mungu ameachia balaa nyengine ituteremkie. Nayo ni kiburi (arrogance) kwa mafisadi na kijicho na choyo (jelousy) kwa walalahoi. Hii inapelekea mtu watu wa katikati na chini kufanya semi-fasada katika kuhakikisha nae anapata kama fisadi. Tofautisha hii rushwa (matokeo) na fasada (chanzo).

Binafsi, ninashuku, situhumu na kwa hiyo sina ulazima wa ku-prove. Ninashuku kwa mapana na marefu kuwa UFIASADI (kichwa/chanzo/mama) wa matatizo yetu unaweza tu kufanywa na watu wa ngazi za juu, yaani kuanzia MARAISI, MAWAZIRI NA MANAIBU WAO, MAKATIBU WAKUU na kuendelea mpaka kwa uchache WAKURUGENZI WA MIKOA. Kwa upande mwengine WABUNGE. Hawa hawali rushwa bali wanalolifanya ni UFISADI. Utaratibu wa kushughulikia watu hawa ni:

1. Mazingira yawekwe safi kwa sheria kufuata mkondo wake pale wanapotuhumiwa kwa ufisadi. Kweli kwa mazingira ya sasa

(a) Je!! muendesha mashtaka anaweza kumshitaki mtu aliye mbunge??? -Hawezi na anaogopa hasa, ni sawa na kusema amezuiliwa kufanya kazi yake.

(b) Je!! Raisi/Mwenyekiti wa chama anaweza kumstaafisha mbunge wa kuchaguliwa?? Hawezi kwa maana amechaguliwa na wananchi.

(c) Bila ya shaka jambo lililobakia ni kwa Mwenyekiti wa chama wakiwa ndani ya chama chao KUWAFUKUZA KUTOKA CHAMANI, KUWAVUA UANACHAMA au KUWASIMAMISHA UANACHAMA. Lolote moja kati ya hayo ya kifungu (c) yakifanyika basi kifungu (a) na (b) yatatokea automatically, kwasabababu hasimami mbunge TZ bila ya chama.

Hapo tena taratibu/hatua Na. 2 zitafuata (hii mada tuiweke kando kwanza) Maana heheeeee!!! kama mimi ningekuwa ndio Raisi wenu TZ mliyenipa political capital ya aslimia 85%, mngeyaona mambo safari hii!!!. Maana Mwenyezi Mungu akikupa nafasi ya jihadi usiiache ikupite. Raisi wetu na vingunge wa CCM hawayajui haya???, ilichobaki sisi tutapigwa kiswahili tuuuuuuuuuuuuuuu. Masikini ama sisi waDAnganyika !!!!

Frustrating, better to keep quite
 
And it tells it all that we are not serious about what we are doing.
 
Hivi hao watu wakifukuzwa nafasi zao zitachukuliwa na malaika? Kwa mfano kesho muungwana akitekeleza hicho kinachopigiwa kelele , tunadhani ndo ufisadi utaisha? Nadhani inatakiwa pendekezo "comprehensive" litakalobadilisha mfumo kama alichosema Obama-Afrika haihitaji personalities but institutions. Tuanze sasa kuandaa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu ili kujenga taasisi imara ili tuondokane na hizi kelele na karaha za watawala.
 
Mbona Shehe Yahya hajamtabiria ushindi wa ile kesi yake ya ufisadi?
 

Wacha upuuzi wewe wa kuwadhania dhana mbaya watu ambao hata huna ushahidi wowote wa wao kufanya kosa lolote. Kwa mfano tutakuchagua wewe, kama wewe ni malaika au binadamu utajijua mwenyewe, lakini sisi hatutakuhukumu bila kosa. Kwa wakati huo utakapochaguliwa, utakuwa umeshajua tu kwamba mwenzio aliyepita sio tu kafukuzwa, kavuliwa au kasimamishwa chamani, bali kapata ile hatua Na. 2 ya sheria na mkondo wake (ambayo mjadala wake kwa sasa tumesema tumeiweka kando kwanza, maana habari zake ni nzito na za kutikisa nyoyo za kiFISADI zitakazobakia). Yaani utakuwa na yakini ya kutokuwa na pahala pa kujifichia UFISADI wako kama nawe utakuwa una mtazamo wa kifisadi.

Kwa hivi sasa, kuacha kufanya hivyo kwenye chama chao CCM ni ishara tosha kwamba sio tu WANAWAFICHA/WANAJIFICHA HUMO na kwamba wanalolifanya viongozi wao (NEC) kwetu ni kututoa upepo tu kwa kutulaghai, bali vilevile hizo ni harakati zao mahsusi/maalum KUZUIA sheria isifuate mkondo wake dhidi ya mafisadi. Hatua Na. 2 haiwezi kuwafikia kwa mafichoni walimo sasa. Na kwa mara nyengine tena, nashuku ninayoyasema, situhumu wala sishutumu hivyo sina ulazima wa ku-prove. HAYA YOTE, WAO CCM "ORGANS" ZAO ZOTE SIO WAJINGA KAMA MIMI WA KUTOWEZA KUYAJUA na KUYAFAHAMU!!! Wewe unasemaje ??? Ndio maana nasema, "masikini roho zetu waDAnganyika".

Kwa taarifa yako Obama ni Raisi wa Marekani na sio wa Tanzania. Wewe vipi lakini wewe??? Kwani sisi lazima tufuate formula za kimagharibi. Hapo juu nili-suggest mfano wa kukuchagua wewe kwa "fairness" niliyonayo moyoni mwangu na kwa kujua kwamba na wewe ni Mtanzania kama sote tulivyo, lakini hapa nasema "HUTUFAI NA HUNA MAANA WEWE" mpaka hapo utakapojikomboa kiakili mwenyewe na kuwa na "independent ideas", au kinyume na hivyo, basi ni rahisi kugeuka kuwa fisadi. Wake up my friend, don't you think that we can do better, and come up with better ideas than OBAMA especially when it is about ourselves.
 
Mwizi wa mali ya umma ni mwizi tu hapaswi hata kupewa dhamana nashangaa sisi tunaona kama ni udokozi gengeni
 
MBUNGE wa Rombo, Basil Mramba, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Kilimanjaro. ...

habari hii ingeanza hivi "mtuhumiwa katika kesi ya ufisadi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali (ambaye pia ni mbinge wa rombo), basil mramba amech..."
 
kwa uzoefu wake wa kulazimisha issues rejea "ikibidi watanzania wale majani..." sitashangaa iwapo pia aliwatunishia misuli hiyo bodi ya tanroads
 
Unajua ile barabara ya Moshi - Rombo mpaka Tarakea inakaribia kukamilika kwa kiwango cha lami...sasa hi ni kama Ahsante kwa mhe Mramba..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…