MBUNGE wa Rombo, Basil Mramba, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Kilimanjaro.
Mramba ambaye amepata kuwa Waziri wa Fedha wakati wa Serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, alichaguliwa kushika wadhifa huo jana wakati wa kikao cha bodi hiyo kilichofanyika mjini hapa.
Mbunge huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya ufisadi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya sh bilioni 11.7 wakati akiwa Waziri wa Fedha, atashika nafasi hiyo chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye kwa utaratibu mpya wa serikali, ni mkuu wa mkoa huo, Monica Mbega.
Kwa bahati mbaya waTanzania na takriban Africa nzima bado hatujaweza ku-
pinpoint MAMA au kichwa cha matatizo tuliyonayo. Tunafirkiri matatizo ni:
1. Hali ngumu ya maisha, kifedah na kiuchumi
2. Rushwa iliyotapakaa kila idara
3. Ubaguzi/Upendeleo wa kikabila/kidini n.k
4. Udhalilishaji wa kijinsia/ulemavu n.k
Kwa kifupi haya yote si matatizo. Haya na mengineyo ni matokeo tu ya tatizo kichwa/mama tulilonalo ambalo ni
VIONGOZI MAFISADI . Hili ndio tatizo kichwa/mama tulilonalo. Kutokana na wao kujikusanyia kila kitu, mambo haya hupatikana:
1.
Tabaka hujengeka baina walionacho na wasionacho (matajiri na masikini) pasipo uhalali wa utajiri na umasikini huo. Mafisadi wanakwapua/wanalipana pasipo uhalali wala usawa zaidi ya wanavyostahili au kuhitaji wakati wadhulumiwa wanakwapuliwa pasipo uhalali wala usawa chini ya kiwango wanachostahili.
2. Hii inapelekea mafisadi ku-indulge katika "luxuries" and "lavishness" na walalahoi kuingia katika hali ya "desperation". Desperation ambapo mtu anavuja jasho jingi lakini kipato kidogo kiasi cha kutokuwa tena "kazi ndio kipimo cha akipatacho na utu wake" Ili ku-survive, ina maana afanye lolote lile kupata angalau basics. Nini matokeo yake???
3. Katika hali kama hii, Mwenyezi Mungu ameachia balaa nyengine ituteremkie. Nayo ni
kiburi (arrogance) kwa mafisadi na
kijicho na choyo (jelousy) kwa walalahoi. Hii inapelekea mtu watu wa katikati na chini kufanya semi-fasada katika kuhakikisha nae anapata kama fisadi. Tofautisha hii rushwa (matokeo) na fasada (chanzo).
Binafsi, ninashuku, situhumu na kwa hiyo sina ulazima wa ku-prove. Ninashuku kwa mapana na marefu kuwa UFIASADI (kichwa/chanzo/mama) wa matatizo yetu unaweza tu kufanywa na watu wa ngazi za juu, yaani kuanzia MARAISI, MAWAZIRI NA MANAIBU WAO, MAKATIBU WAKUU na kuendelea mpaka kwa uchache WAKURUGENZI WA MIKOA. Kwa upande mwengine WABUNGE. Hawa hawali rushwa bali wanalolifanya ni UFISADI. Utaratibu wa kushughulikia watu hawa ni:
1. Mazingira yawekwe safi kwa sheria kufuata mkondo wake pale wanapotuhumiwa kwa ufisadi. Kweli kwa mazingira ya sasa
(a) Je!! muendesha mashtaka anaweza kumshitaki mtu aliye mbunge??? -Hawezi na anaogopa hasa, ni sawa na kusema amezuiliwa kufanya kazi yake.
(b) Je!! Raisi/Mwenyekiti wa chama anaweza kumstaafisha mbunge wa kuchaguliwa?? Hawezi kwa maana amechaguliwa na wananchi.
(c) Bila ya shaka jambo lililobakia ni kwa Mwenyekiti wa chama wakiwa ndani ya chama chao KUWAFUKUZA KUTOKA CHAMANI, KUWAVUA UANACHAMA au KUWASIMAMISHA UANACHAMA. Lolote moja kati ya hayo ya kifungu (c) yakifanyika basi kifungu (a) na (b) yatatokea automatically, kwasabababu hasimami mbunge TZ bila ya chama.
Hapo tena taratibu/hatua Na. 2 zitafuata (hii mada tuiweke kando kwanza) Maana heheeeee!!! kama mimi ningekuwa ndio Raisi wenu TZ mliyenipa political capital ya aslimia 85%, mngeyaona mambo safari hii!!!. Maana Mwenyezi Mungu akikupa nafasi ya jihadi usiiache ikupite. Raisi wetu na vingunge wa CCM hawayajui haya???, ilichobaki sisi tutapigwa kiswahili tuuuuuuuuuuuuuuu. Masikini ama sisi waDAnganyika !!!!
Frustrating, better to keep quite