Mramba auza hoteli yake?

Mramba auza hoteli yake?

Ninachoipendea Tz ni kwamba hata kama ukimuuzia mtu mwingine itajulikana tu.
Huyu anayeshrikiana na mwizi kununua kitu cha wizi na yeye pia hana tofauti na mwizi.Waandishi wa habari kazi kwenu
 
nasikia wabunge wameamua kutuchangisha wananchi kwenye kikako kijacho cha bajeti ili tuwarudishie Mkapa na wenziwe zile shilingi millioni 70 walizolipa kule Kiwira, kumbuka kuwa Mramba naye yupo kule, iwapo serikali haitachukua hatua nzito dhidi yao,

bado siwaamini wabunge wetu kiasi hicho, endapo watathubutu watakuwa wameonyesha uzalendo mkubwa na unaweza ukawa mwanzo wa mageuzi makubwa kwani Serikali itakuwa imepata fundisho kubwa sana. Watanzania, pamoja na umasikini wetu, tutajitahidi kuchangia na kumrudishia hizo fedha zake.
Hiyo italeta maana kubwa kwani tutakuwa tumeanza kuongoza nchi yetu sisi wenyewe na wabunge wetu na Serikali kwa upande mwingine inakuwa na mafisadi wao bila wananchi wa kuwaongoza.

Wabunge thubutuni hili basi hata kwa kuijaribu Serikali tu.
 
hii vibweka vya wakubwa mod !!

au na mie nilete "facts" za mbowe kuajiri wasauzi kwenye hoteli yake (aliyoshindwa kumalizia mkopo)?.... where is this guy's patriotism ? mkopo kapewa tanzania, kashindwa kulipa, then anaajiri wasauzi ?

Kada Mpinzani, rejea mtiririko wa mada na utiririke nayo. Unapoleta mada mpya unaukwaza mtiririko wa mawazo wa wasomaji na wanaochangia. Ni ushauri tu!!!

Hili suala la mbunge Mramba kuuza mali zake ni zuri sisi wazawa kulijua ili kutuweka katika nafasi nzuri kuzifuatilia. Na waendele kufanya manouvers za kuficha mambo, kumbe ndipo wanajionyesha wazi. Pesa na mali zinazotokana na rushwa kubwa kubwa hazifichiki kwani huwa zinaacha uvundo kila zinakopelekwa!! Yetu macho na masikio.
 
Mkulu KM,

Kwani hili nalo CCM inamasirahi gani nalo, mramba anashitakiwa kama mramba nashangaa wewe unamtetea au uliambiwa utee watu wote waliokuwa CCM hata kama CCM haina masirahi nalo. Naanza kuhisi hili jina linatumiwa na watu wengine sio yule kada tuliyekuwa naye siku za nyuma ambae alikuwa objective katika kuitetea CCM.

Shy anafaamu kuwa pamoja na kuitetea CCM lakini hili mramba atakufa peke yake.
 
nimependa jibu lako... ndio maana hii inaitwa JF..tunazungumzia Mramba mtu anakuja kutishia mtu mzima nyau!

Safi sana MMJ! Kwa kweli hata mimi nakupongeza. Any way, huyo jamaa ni kweli lakini atakiona cha moto.

Hapo chini umeuliza swali jibu lake ni hili: Kitu ambacho tunaweza kufanya vizuri zaidi ni BIG BROTHER AFRICA!
 
hii vibweka vya wakubwa mod !!

au na mie nilete "facts" za mbowe kuajiri wasauzi kwenye hoteli yake (aliyoshindwa kumalizia mkopo)?.... where is this guy's patriotism ? mkopo kapewa tanzania, kashindwa kulipa, then anaajiri wasauzi ?

Ninavyojua mimi ni kwamba hajawaajiri wa South African,ila kawakodisha.Na hio ni Protea kule Machame,sio? Billicanas,yes ana mkopo na sio siri.Sasa kama its a question of patriotism kwa yeye kukodisha hoteli yake kwa wasauzi,then tutasema nini kuhusu serikali yetu,iliyowapa baadhi ya rasilimali zetu haohao wasauzi,bureee!
 
huyu mramba ni fisadi wa kutupa, ila kuna magazeti ameyanunua pia, lile scandal la alex sterwart auditing ni lake, mnakumbuka kuwa alivyokanusha kuwa godfery mramba ambaye ni mkurugenzi wa alex stewart hana uhusianao naye, na kuwa ikijulikana kuwani mtoto wake atajiuzulu? tunaomfahamu mramba ni kuwa godfery ni mtoto wake tena wa pekee wa kiume na walishirikiana kuchota yale mamilioni ya alex sterwart, mali zake nyingi ziko kwa majina bandia, kampuni ya konoike ana makubwa kule, yeye ndo ile housing estates ya kutisha wanaokaa wajapan ni yake, alikula mlungula akaikwamisha kabisa ile kampuni kumalizia kazi ya dodom kwenda manyoni, isitoshe kuna kampuni nyingine inaitwa highlands estates iliyopewa shamba la nafco, au kapunga rice projects, wale waburushi wanamtaja kuwa ni mtu wa tamaa kama fisi anavyosubiri mkono wa binadaamu udondoke
 
Ninavyojua mimi ni kwamba hajawaajiri wa South African,ila kawakodisha.Na hio ni Protea kule Machame,sio? Billicanas,yes ana mkopo na sio siri.Sasa kama its a question of patriotism kwa yeye kukodisha hoteli yake kwa wasauzi,then tutasema nini kuhusu serikali yetu,iliyowapa baadhi ya rasilimali zetu haohao wasauzi,bureee!

Hivi watu majibu mnajifunzia chuo gani? maana kuna majibu hadi yanafanya huzuni na hofu yote itoke. Zanaki umenifurahisha.
 
hii vibweka vya wakubwa mod !!

au na mie nilete "facts" za mbowe kuajiri wasauzi kwenye hoteli yake (aliyoshindwa kumalizia mkopo)?.... where is this guy's patriotism ? mkopo kapewa tanzania, kashindwa kulipa, then anaajiri wasauzi ?

Tunajua kazi ya makada wa CCM ni nini!! Mbowe hahusishwi na masuala ya corruption wakati Mramba yuko linked na watanzania wanajaribu kujadili namna ya kupata kilicho chao. Kama mwenzetu husikii uchungu wa kuibiwa na hawa watu halafu wanasema tukale majani, then you might be benefiting in one way or onother. Suala la Mbowe ni lake na benki. Angekuwa amechukuwa mkopo kutoka serikalini then tungekuelewa.
 
Mimi niko nina hakiki kampuni ya Mohemmed Seig Khatibu ambayo ina shughulika na magari hapo Holland kwenda Tanzania .Najua magari kadhaa yamekamatwa kwa muda sasa baada ya kutaka kutumia nafasi yake ya Uwaziri kupitisha mizigo na magari yale bila ya ushuru .Ni zaidi ya mwaka sasa kila kitu kiko Bandarini .Kampunu yake lakini kajifanya ni mali ya mdachi
 
Hii vita tunashinda pamoja na kuwa kuna watu wananjaa kiasi cha kuakikisha kuwa wanawatetea mafisadi kwa nguvu zote, lakini tutashinda bado kidogo tutatamba kifua mbele.
 
Mimi ndio maana naona ni bora Dr Wilbroad Slaa agombee uraisi na asafishe nchi nzima.

Mramba pia si amewahi kuwa bosi wa THB na benki hio ya wananchi ikafa na kupotea kabisa na kuwa hatuna tena "Symbol" hio kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Hakuna alieulizwa kuhusu kufilisika kwa benki hio hadi leo, Dr Slaa anaweza kupitia mafaili yooote na kuona kama watu hawa wanaweza kufilisiwa mali zao zote na THB irudishwe ili wananchi wa kipato cha chini wakope pesa za kujenga nyumba.

Watu wameachwa tu wapete hivihivi, lakini safari hii ni lazima Mramba awajibike kwa kukiri kwamba amekuwa mbunge kwa muda mrefu huku akiwa na mambo yake mengine.

CHADEMA-2010
 
... Bw. Basil Mramba ameamua kuachilia umiliki wa hoteli yake ya Kibo Palace iliyoko Arusha karibu na cliniki ya AICC.

Loh Kumbe kile kitu ni cha Mzee huyu!!! Its beutiful project I tell you!!! Ufisadi mtamu ..you need to have tough character and courage of JKN to overcome all the temptation not to be one of them..especialy if the oppotunities are to your exposure...Basili Pesa mbili Mramba the way I know Him..akionyeshwa raamani ya jengo kama lile akaaambiwa "weka saini hapa".... against the interest of the nation asingeweza kuacha!!!
 
Back
Top Bottom