Bila shaka haya ya kufikishwa mahakamani ni mafanikio ya serikali iliyopo madarakani. Lakini usisahau pia kwamba haya ni mafanikio ya upinzani maana ndio wamekuwa wakipigia kelele kwa zaidi ya miaka miwili sasa kwamba hawa watu waende mahakamani. Ni kweli pia kuwa hii ni changamoto kwetu sisi wapinzani maana wananchi watatuuliza, ok mlitaka hawa mafisadi wafikishwe mahakamani, wameshafikishwa, so what is next? Ndio maana ni muhimu kwa vyama vyetu kufanya kazi zaidi ya kuzomea tu na kuibua hizi kashfa.
Kuzomea, kuibua kashfa za serikali, kupinga na kukosoa ni kazi muhimu sana ya chama cha upinzani, lakini hii peke yake haikufanyi wananchi wakuchague. Ili uchaguliwe lazima uonyesha kwamba wewe ni alternative government kwa kuwa na timu imara na sera mbadala utakazotekeleza mara ukabidhiapo madaraka. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, hiki kilichokwishafanywa so far na opposition, hasa CHADEMA, is sufficient enough to make us a credible opposition, but not good enough to convince the masses that we are a better government in waiting. Ili tuwe a credible government in waiting lazima tuchukue the next step, ambayo ni kuwaonyesha wananchi kwamba sisi tuna mawazo,sera, mikakati na timu mbadala murua na bora zaidi zitakazotatuta, pamoja na matatizo mengine, tatizo la ufisadi kama wakitupa tuendeshe serikali yao. Kuna haja kubwa sana sasa kujikita katika kuelezea sera na mikakati yao juu ya matatizo mbalimbali ya nchi yetu.
Kwa hiyo JokaKuu, mimi binafsi naona kwamba haya yanayoendelea ni ushindi kwa nchi yetu lakini pia kwa vyama vya upinzani, maana vinatupa fursa na haki zaidi ya kusikikilizwa na wananchi. Sasa wazee kama Kingunge hawawezi kuthubutu tena kukaa ukumbi wa maelezo na kuwaambia wananchi kwamba wapinzani ni waongo. Wananchi sasa wanaelewa kwamba walio waongo ni akina Kingunge na CCM yao! Kama wapinzani walikuwa waongo pale Mwembe Yanga, iweje basi leo akina Mramba wafikishwe mahakamani?