Mhmm!! kainzi nomaa, nadhani umeshasikia wawili wako wapii! huyo mmoja ndio itabidi watu watuambie yuko wapiiHawa watu wanne ??? nina hamu sana ya kujua walipo sasa hivi.. Kwani nimesikia king'ora kimelia na kuna dalili mmoja wao akawa ametoweka kimoja! Lakini kati ya wote ningependa kujua Basil Mramba leo hii yuko wapi, kuna mtu anamtafuta sana...
Yote Tisa kuna fisadi mmoja sijasikia hata tetesi na yeye kaamua kueka profile yake low saaaaaaaaaaaaaaaana. hata Kwenye media hasikiki nae ni :::::::SUMAYE:::::::: je Mramba, Yona hawakuwa karibu na huyu mkuuuuu?????
Si huyo pekee, hata our previous IGP ....Mr. Mahita ....mbona hatusikii wakitafutwa?
.....whistling.....
By the way, hongera sana.
Kuhani,
..nilipotuma posting ile nilikuwa na nia ya kuchokoza mjadala tupime kama hii timu ya Raisi imetimiza wajibu wake, na kwa kiwango kipi.
..nilitegemea wachangiaji makini kama wewe wangetoa hoja kuhusu mafanikio na mapungufu kuhusu kazi iliyofanyika.
..kuhusu maswali yako: Polisi akifukuza mwizi sugu na kusababisha mali aliyoiba kupatikana, hata kama asipomkamata mwizi yule, wananchi wanaweza kumpa asante/pongezi.
..tunaweza kumshukuru Mkuu wa Taasisi ya Rushwa ya serikali ya CCM kwa kujirudi na kuamua kupambana na rushwa. tunapofanya hivyo siyo lazima tuwe tumeridhika na kazi yake, bali ni kumpa moyo apambane na rushwa kubwa zaidi.
..zingatia kwamba tunaishi ktk Tanzania inayoongozwa na CCM.
Kitila Mkumbo,
..sijui Chadema mmejiandaa vipi with these developments.
..sidhani kama mlifanya kazi ya kuridhisha katika ku-establish a link btn rushwa na wizi huu na CCM na kampeni za uchaguzi.
..pia mmeelekeza nguvu nyingi kumuandama Raisi mstaafu kuliko huyu ambaye yuko madarakani.
..nadhani the end game ni JK kujikosha mbele ya wananchi kwamba anashughulikia rushwa, na kupata huruma na imani ya wananchi.
..nilitegemea ungejielekeza kujenga hoja ktk masuala hayo hapo juu, badala yake umekuja na hoja ya BABA na NEPI!!!
....the siren is on...
Kitila Mkumbo,
..sijui Chadema mmejiandaa vipi with these developments.
..sidhani kama mlifanya kazi ya kuridhisha katika ku-establish a link btn rushwa na wizi huu na CCM na kampeni za uchaguzi.
..pia mmeelekeza nguvu nyingi kumuandama Raisi mstaafu kuliko huyu ambaye yuko madarakani.
..nadhani the end game ni JK kujikosha mbele ya wananchi kwamba anashughulikia rushwa, na kupata huruma na imani ya wananchi.
..nilitegemea ungejielekeza kujenga hoja ktk masuala hayo hapo juu, badala yake umekuja na hoja ya BABA na NEPI!!!
Lets add Gen. Mboma and Cornel Apson on the list!
Unamshukuru polisi kwa kufukuza mwizi ?
Unamshukuru Mkuu wa Tume ya kupambana na rushwa kwa kupambana na rushwa ?
Unamshukuru Mwanasheria Mkuu kwa kufuata sheria ?
Mimi ni kuli. Kwa kila mzigo ninaopakia na kupakua kwenye malori ya kampuni bosi anadunduliza hela sehemu kila mwisho wa siku. Zikifika wiki mbili karani wa kampuni ananipa hundi. Sijawahi kuambiwa ahsante. Tena mwenye mizigo hii, mmiliki wa kampuni, sijawahi hata kuteta nae.
Nikadai shukurani ?
Rev.Kishoka,
..Gen.Marwa Waitara alikuwa CDF kabla ya huyu wa sasa hivi.
..sidhani kama Mgonja,Mrisho,na Rutabanzibwa, wanaweza kupelekwa mahakamani ktk kundi moja.
..Rutabanzibwa ndiyo kwanza amehamishiwa wizara ya mambo ya ndani.
Bila shaka haya ya kufikishwa mahakamani ni mafanikio ya serikali iliyopo madarakani. Lakini usisahau pia kwamba haya ni mafanikio ya upinzani maana ndio wamekuwa wakipigia kelele kwa zaidi ya miaka miwili sasa kwamba hawa watu waende mahakamani. Ni kweli pia kuwa hii ni changamoto kwetu sisi wapinzani maana wananchi watatuuliza, ok mlitaka hawa mafisadi wafikishwe mahakamani, wameshafikishwa, so what is next? Ndio maana ni muhimu kwa vyama vyetu kufanya kazi zaidi ya kuzomea tu na kuibua hizi kashfa.
Kuzomea, kuibua kashfa za serikali, kupinga na kukosoa ni kazi muhimu sana ya chama cha upinzani, lakini hii peke yake haikufanyi wananchi wakuchague. Ili uchaguliwe lazima uonyesha kwamba wewe ni alternative government kwa kuwa na timu imara na sera mbadala utakazotekeleza mara ukabidhiapo madaraka. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, hiki kilichokwishafanywa so far na opposition, hasa CHADEMA, is sufficient enough to make us a credible opposition, but not good enough to convince the masses that we are a better government in waiting. Ili tuwe a credible government in waiting lazima tuchukue the next step, ambayo ni kuwaonyesha wananchi kwamba sisi tuna mawazo,sera, mikakati na timu mbadala murua na bora zaidi zitakazotatuta, pamoja na matatizo mengine, tatizo la ufisadi kama wakitupa tuendeshe serikali yao. Kuna haja kubwa sana sasa kujikita katika kuelezea sera na mikakati yao juu ya matatizo mbalimbali ya nchi yetu.
Kwa hiyo JokaKuu, mimi binafsi naona kwamba haya yanayoendelea ni ushindi kwa nchi yetu lakini pia kwa vyama vya upinzani, maana vinatupa fursa na haki zaidi ya kusikikilizwa na wananchi. Sasa wazee kama Kingunge hawawezi kuthubutu tena kukaa ukumbi wa maelezo na kuwaambia wananchi kwamba wapinzani ni waongo. Wananchi sasa wanaelewa kwamba walio waongo ni akina Kingunge na CCM yao! Kama wapinzani walikuwa waongo pale Mwembe Yanga, iweje basi leo akina Mramba wafikishwe mahakamani?