TANZIA MRATIBU Msaidizi Baraza la Usalama wa Taifa, Brigedia Jenerali Vitalis Andrew Chakila amefariki dunia

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
MRATIBU Msaidizi Baraza la Usalama wa Taifa, Brigedia Jenerali Vitalis Andrew Chakila amefariki dunia.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda. Kwa mujibu wa Taarifa iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, Luteni Kanali, Gaudentius Ilonda, Brigedia Jenerali Vitalis alifariki dunia Juni 23,2024.

Aidha taarifa imesema kwamba heshima za mwisho kwa marehemu zitatolewa Makao Makuu ya Jeshi, Msalato, Jijini Dodoma, Juni 26,2014 saa tano asubuhi. Baada ya heshima hizo mwili utasafirishwa kwenda Kahama, Shinyanga kwa maziko yatakayofanyika Juni 27,mwaka huu. Brigedia Jenerali Vitalis alizaliwa Mei 29,1965 katika Kijiji cha Mhungula, Kata ya Nyihogo, wilaya ya Khama mkoani Shinyanga. Alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Bwiru Boys na kuhitimu kidato cha nne 1984.

Alihitimu kidato cha sita Sekondari ya Kibaha mwaka 1987 na kujiunga na JWTZ Septemba 30,1987. Alihudhuria kozi ya Afisa Mwanafunzi nchini Tanzania na kutunukiwa kamisheni katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania mwaka 1989. Alipata mafunzo mengine ya kijeshi nchini Uholanzi, Mali na Tanzania kwa nyakati mbalimbali.

Katika kipindi cha utumishi wake jeshini alipandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali hadi cheo cha Brigedia Jenerali alichopandishwa Aprili 12,2018.

Katika utumishi wake jeshini aliwahi kushika madaraka mbalimbali yakiwemo Mkuu wa tawi la Ukaguzi Makao Mkuu ya Jeshi mwaka 2020 hadi 2021 aliposhika wadhifa wa Mratibu Msaidizi wa Baraza la Usalama wa Taifa ,wadhifa aliokuwa nao hadi alipofariki dunia Juni 23,2024.
 
MRATIBU Msaidizi Baraza la Usalama wa Taifa, Brigedia Jenerali Vitalis Andrew Chakila amefariki dunia. Taarifa ya kifo chake imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda. Kwa mujibu wa Taarifa iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, Luteni Kanali, Gaudentius Ilonda, Brigedia Jenerali Vitalis alifariki dunia Juni 23,2024. Aidha taarifa imesema kwamba heshima za mwisho kwa marehemu zitatolewa Makao Makuu ya Jeshi, Msalato, Jijini Dodoma, Juni 26,2014 saa tano asubuhi. Baada ya heshima hizo mwili utasafirishwa kwenda Kahama, Shinyanga kwa maziko yatakayofanyika Juni 27,mwaka huu. Brigedia Jenerali Vitalis alizaliwa Mei 29,1965 katika Kijiji cha Mhungula, Kata ya Nyihogo, wilaya ya Khama mkoani Shinyanga. Alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Bwiru Boys na kuhitimu kidato cha nne 1984.Alihitimu kidato cha sita Sekondari ya Kibaha mwaka 1987 na kujiunga na JWTZ Septemba 30,1987. Alihudhuria kozi ya Afisa Mwanafunzi nchini Tanzania na kutunukiwa kamisheni katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania mwaka 1989. Alipata mafunzo mengine ya kijeshi nchini Uholanzi, Mali na Tanzania kwa nyakati mbalimbali. Katika kipindi cha utumishi wake jeshini alipandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali hadi cheo cha Brigedia Jenerali alichopandishwa Aprili 12,2018. Katika utumishi wake jeshini aliwahi kushika madaraka mbalimbali yakiwemo Mkuu wa tawi la Ukaguzi Makao Mkuu ya Jeshi mwaka 2020 hadi 2021 aliposhika wadhifa wa Mratibu Msaidizi wa Baraza la Usalama wa Taifa ,wadhifa aliokuwa nao hadi alipofariki dunia Juni 23,2024.
Shauri yake. Si wanatetea CCM japo inatutesa wananchi.
 
1719385328318.png
 
Thank you for your service sir, Rest where peace resides.
 
Gwanda hata haijachafuka..yan kahudhuria mafunzo nchi 3 tu in his entire career????
 
Back
Top Bottom