TANZIA Mratibu wa shughuli za mgombea ubunge jimbo la Sengerema amefariki dunia, adaiwa kulishwa Sumu

TANZIA Mratibu wa shughuli za mgombea ubunge jimbo la Sengerema amefariki dunia, adaiwa kulishwa Sumu

Nadir Naimuor

Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
15
Reaction score
15
Jicho linaelekea katika jimbo la Sengerema lililopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza jimbo ambalo kwa miaka kumi na tano liliongozwa na Ngereja kama mbunge Ila mwaka huu baada ya kura za maoni kuisha Chama cha Mapinduzi kilimpitisha mgombea Hamis Tabasam kuwa mgombea ubunge.

Katibu wa CCM kata ya Ibisabageni, Deogratias Medard na pia ni mratibu wa shughuli za mgombea ubunge jimbo la Sengerema amefariki dunia juzi J'tatu majira ya mchana alipokuwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa kampeni kijiji cha Kagunga.

Kisa hiki kilitokea wakati marehemu Deo alipokuwa ameketi siti ya katikati kwenye gari la mgombea ubunge na akiwa na mgombea ubunge, mhasibu na wengine 2 pamoja na dereva.

Kabla ya kuanza safari hiyo Deogratias alitoka nyumbani na kufika kwenye ofisi za mgombea ubunge maeneo ya Sengerema Mjini karibu kabisa na stand ya mabasi kilipo kituo cha kujazia mafuta majira ya saa mbili asubuhi akiratibu shughuli za mikutano ya siku hiyo mida kati ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi alikula chakula makande na chai iliyotoka kwenye mgahawa ulioko nyuma ya ofisi ya mgombea ubunge kwa mama maarufu kwa upikaji wa makande hayo.

Baada ya kumaliza kula walianza safari ya kuelekea kijiji cha kagungu na walipokaribia kufika kijiji cha tunyenye ndipo Deo alipoanza kulalamika tumbo linamuuma; gari likasimama na akaanza kutapika matapishi yenye harufu kali. Ndipo akakimbizwa kituo cha afya Tunyenye na kuwekewa drip mbili kwa wakati mmoja ila hali ikazidi kuwa mbaya, gari la mgombea liligeuza na kurudi mjini Sengerema na Deogratias Medard akawa amefariki dunia njiani.
Screenshot_20201023-092833.png

IMG-20201023-WA0022.jpg
IMG-20201023-WA0021.jpg

Jnne mwili tuliutoa hospital ya misheni hapa Sengerema a na kuupeleka Bugando hospitali kwa ajili ya kuufanyia post-mortem na usiku wa jnne hiyo mwili tuliurudisha sengerema na jtano tukauzika.

Hadi sasa ni watu sita wameshahojiwa. Siku ya Jumatatu walikamatwa watu sita. Wawili wakaachiliwa Jumanne.

Mama mwenye Mgahawa na Wasaidizi wake, ni miongoni mwa watu waliokamatwa

=====

UPDATES:23 Oct 2020

======

Polisi Mwanza wanachunguza chanzo cha kifo cha Deogratias Meded(42) Mkazi wa Sengerema aliyefariki muda mfupi baada ya kudaiwa kula makande na chai akiwa kwenye Kampeni za Mgombea Ubunge Sengerema kwa Ticketi ya CCM, Hamis Tabasamu ambapo Marehemu alikuwa Meneja wa Kampeni wake.
 
Kwenye maswala ya kibinadam au swala lolote lisilo la kibinadam lisihusishe vyama au itikadi binadamu yyte ana haki sawa na mwingine
 
Swala la mtu kupewa sumu sio jambo la kawaitwa na alie fanya hivyo sio binadamu wa kawaida haijalishi alie mfanyia ana itikadi gani wala chama gani.
 
Back
Top Bottom