TANZIA Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga afariki Dunia

Ukiona inatamkwaf "aliugua kwa muda mrefu" OGOPA.
R.I.P Papaa Lundenga. Mafataki hawatakaa wamsahau huyu mdau muhimu kwenye career yao.
Figo watu wanaugua kwa muda mrefu,kisukari watu wanaugua kwa muda mrefu,kuna kupooza (maradhi ya utu uzima ambao Lundenga alikuwa nao) nayo watu wanaugua kwa muda mrefu.

Tunafanya kuhukumu tu hapa currently wengi wetu hapa hata status za afya zetu hatuzijui siyo ajabu tukipimwa leo tuna magonjwa makubwa na ya aibu ambayo hata huyu mzee hajawahi kuwa nayo.
 
Tusingewafahamu akina K-Lynn, Wema Sepetu, Faraja Nyarandu, Happyness Magese n.k isingekuwa huyu Mzee na miss Tanzania yake.

Tunamuombea marehemu apumzike kwa amani

Mbele yetu, nyuma yake 😭😭
Astaghfirullah

Atapumzikaje kwa amani wakati yeye muislamu na aliwatembeza mabinti ma miss nusu uchi majukwaani wakitembea mbele ya kadamnasi bila kuvaa hijabu? Kama maamrisho ya uislamu yanavyotaka?

Mungu amuweke panapomstahili anapoona panamfaa barabara kwa alichofanya duniani kwa ma miss Tanzania
 
Pumzika kwa amani shemeji yetu!
 
Mkuu tupo kwenye maombolezo ujue

Hata hivyo Kwa mujibu wa maandiko ya vitabu vya Dini, mwenye mamlaka ya kuhukumu ni mola wetu pekee

Huenda nyakati za kuugua kwake Kwa muda mrefu jamaa atakuwa alimrudia Mungu wake Kwa kufanya toba

Kwa maana tunaambiwa Mungu wetu ni mwingi wa rehema ambaye hutoa msamaha Kila tunapoenda kumlilia miguuni pake
 
Hicho ulichoaandika ni ujinga wa dini.
 
Miaka ya 2000 hadi 2010. Huyu Mwamba amekula maisha sana
 
Hawa wazee ndio walileta misemo ya Laki si Pesa. Bata kila mahali enzi za kina Wema na kina Sinta mama ya J nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…