TANZIA Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga afariki Dunia

TANZIA Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga afariki Dunia

View attachment 3309148

Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania Hashim Lundega, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kitengule - Tegeta, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa Marehemu Lundenga, Bosco Majaliwa, Lundenga ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu, alikimbizwa hospitalini hapo leo asubuhi baada ya kuzidiwa lakini muda mfupi baadaye akafariki.

Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu itakumbukwa ndio aliyesimamia kwa mafanikio makubwa Mashindano ya Urembo Tanzania na kuyapa umaarufu mashindano hayo.

Lundenga pia aliwahi kuhudumu kwenye Kamati ndani ya Klabu ya Yanga.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake Boko jijini Dar.
Rip
 
Kuna mambo mengi yamebadilika miaka hii 10, kwamza utawala wa Magu ulisambaratisha mishentown wote kuanzia kata mpk taifa, wakiwa bado wanafurukuta ikapiga covid, wale wenye magonjwa nyemelezi maarufu na ma alwatan wameanguka, story zao zimeshia hapo, kazi kwenu kuziendeleza
 
Back
Top Bottom