TANZIA Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga afariki Dunia

TANZIA Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga afariki Dunia

Mwislamu hatakiwi kushindanisha wrembo duniani kwa sababu anatakiwa afanye juhudi apate mahurulaini huko akhera basi.
HHakuanmambo awa wanaoitwa mamiss wengi wao huwa ni wabaya kuliko wanaopatikana majumbani

Lundenga ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu, alikimbizwa hospitalini hapo leo asubuhi baada ya kuzidiwa lakini muda mfupi baadaye akafariki.

Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu...
Sawa
 
Siti mtemvu alikuja kuvuruga kila kitu saivi haina ladha kabisa
Unajua zamani tukiwa wadogo enzi hizo miaka ya 90 mwiahoni na 2000 mwanzoni, ilikuwa aisee mashindano ya Miss Tanzania hamlali kabisa.

Kuna shida imetokea mahali, nyakati hizi haya mashindano ndo yangetakiwa yawe moto bati maana pesa ipo na wadhamini ni wengi sana
 
RIP Lundenga, you left a mark, tangu umetoka tu na mashindano yamekufa, hawana hata nauli ya kumpeleka Miss World mtu mmoja tu!
Yalianza kufa mikononi mwake kwa kutokea skendo kubwa kama ya sitti mtemvu lakini pia baada ya Vodacom kujiondoa kama main sponsor. Kiufupi alifanya kuyaachia kwa kuchelewa na akamkabidhi mtu ambaye nae hakuwa compitent kuyafufua.
 
Kauli yake dhidi ya waumini wenzake waliomshambulia kwa maneno dhidi ya mashindano ya urembo ".....nikifa na kama hamtotaka kunizika basi ninyi ndio mtakaopata shida kwa kunukiwa na maiti yangu....".

#Resty easy mjomba amen!
 
View attachment 3309148

Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania Hashim Lundega, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kitengule - Tegeta, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa Marehemu Lundenga, Bosco Majaliwa, Lundenga ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu, alikimbizwa hospitalini hapo leo asubuhi baada ya kuzidiwa lakini muda mfupi baadaye akafariki.

Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu itakumbukwa ndio aliyesimamia kwa mafanikio makubwa Mashindano ya Urembo Tanzania na kuyapa umaarufu mashindano hayo.

Lundenga pia aliwahi kuhudumu kwenye Kamati ndani ya Klabu ya Yanga.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake Boko jijini Dar.
Hatimaye NGWENGWE ime mbwaga fundi mkuu.
 
Yaani jamaa limefaidi sanaa
Ila nImeelewa hapo kwamba amefariki baada ya KUUGUA MUDA MREFU.
 
Yalianza kufa mikononi mwake kwa kutokea skendo kubwa kama ya sitti mtemvu lakini pia baada ya Vodacom kujiondoa kama main sponsor. Kiufupi alifanya kuyaachia kwa kuchelewa na akamkabidhi mtu ambaye nae hakuwa compitent kuyafufua.
Kwani sahiv yapo chini ya nani, siyasikii tena?
 
Huyu mzee alikuwa ni rafiki wa Babu yangu. Sasa wanaenda kukutana peponi 🥺😥😭

mlale salama
 
Back
Top Bottom