Mrejesho baada ya kuambiwa nichague kati ya Vanguard na Harrier ili ku compensate kama malipo ya kazi

Mrejesho baada ya kuambiwa nichague kati ya Vanguard na Harrier ili ku compensate kama malipo ya kazi

Mkuu,

Pole sana kwa maswaibu yaliyokupata.

Ila umefeli kitu kimoja. Huyo mwanamke aliyekujibu hovyo ulipaswa kumripoti. Mbona kaleta dharau namna hiyo?
Umripoti wapi sasa?
Unadhani hivyo viburi vyao viko bure bure?
Mabosi wanamega na hiyo ndo inawapa kiburi.
Ukimueleza bosi utaitikiwa tuu ndio nalifanyia kazi ,Ila sahau jambo lolote kufanyiwa kazi
 
Huyo dada ndio wale Aina wanachelewesha maendeleo ya nchi halafu jiwe alikua anawapa lawama wapinzani,
Tanzania tukiendekeza ujinga Kama huo hatutaendelea kamwe!
Mamlaka nadhani mmepata muongozo uzembe wa huyo dada unalicost taifa ni mzigo Bora arudi kitaa kulea watoto na kudanga maana ndio fani saizi yake

Hili ni povu la buku jero tu!😤😤

Baadhi ya wadada au wanaume wenye tabia hizi makazini aidha wanamahusiano kimapenzi na bosses, ukaribu wa kikabila, kigodfather, makuwadi, mashemeji wa mabosi, dawa za kichawi hasa mazombi, baadhi ni hulka za asili na kunachangamoto ofisi nyingi za umma hazina miongozo,nyaraka na taratibu za uadilifu na unyenyekevu katika kuhudumia wateja wao. Na hasa idara ambazo zina taswira kama ya kutegemewa na zenye hulka ya utisho sana mfano TRA, Tanesco, tanroads, tarura, ofis ya mkurugenzi, ofis xa elimu, ofis za malipo ya ada, ofisi za mitihani, lipo jambo haliko sawa tanzania kwenye kuhudumu maofisi kwa namna ya kumfanya mteja ama mgeni aondoke na sifa bora ya kusikilizwa au kutatuliwa tatizo au kushauriwa na kuelekezwa au kufamishwa vema.

There is something lacking among us across all spheres in our portifolios or rather dockets. I dearly submit for imminent desirable reforms.
 
Kama maelezo ndio yameishia hvyo. Hilo gari sio lako na hauna uhalali wa kuliuza ama kumpatia mtu mwengine yeyote na kuendelea kuwa nalo litakuletea shida.. kwa maelezo hayo hilo tatizo mmelitatua kienyeji sana Mkuu, hautambuliki ktk mamlaka yoyote kama ww ni mmiliki halali. Ulipaswa kubadili kadi ya gari kwanza na magari mengi ya miradi uwa yana exemption na ili gari ibadilishwe umiliki kwenda kwenye umiliki binafsi ni lazima ile kodi iliyokuwa exempted ilipwe na kama kulikuwa na kodi zingine kampuni inadaiwa lazima izilipe mana kwenye kufanya transer lazima itahitajika tax clearance ya kampuni.
 
Dah! Una bahati sana.
maisha ya kibongo haya kumiliki gari kubwa ni shughuli kweli.

Mimi pale kahama mining nimeservice miaka 4 kabla sijatupiwa virago lakin sikununua

Huwa najuta sana.sidhan kama nitanunua tena.
hiyo ndo athari ya kufanyia kazi migodi ya vijijin.
Ndio.... Mana makubariano nichukue moja but wakasema niwaongezee hyo pesa wanipe zote.
 
Kama nilivyowaomba ushauri kwenye post yangu ya 8/1/2021 nikitakiwa kuchagua kati ya gari tajwa hapo juu na kampuni moja ya ujenzi kama fidia ya deni nililowadai kwa muda mrefu bila malipo.

Nawashukuru sana wana Jf na members wa forum hii kwa ujumla kwa mchango wenu wa ushauri , maoni na mawazo kwa ujumla. Na kwa faida ya msomaji mpya ni kwamba Wadau walinishauri nifanye observation ili ku confirm kama zimelipiwa kodi kihalali au zina msamaha wa muda kabda ya kuchagua gari yakuchukua.

Tarehe 11 /1/2021 siku ya j3 nilifika ofisi za TRA kuulizia suala hilo. Nikamkuta dada mmoja (alie barikiwa dharau ya kiwango cha flyover) nikajaribu kumuelezea but hakunipa ushirikiano kabisa ikabidi nitoke kinyonge sana. Nikapata wazo lakwenda bandari kukagua kwenye importation special book kwa kutumia tar ya gari zilipoingia nchini ili kujua kama ziliingia kwa vibari maalum au ziliingia kama mizigo mingine kawada. Nilibahatikiwa kufika nikamkuta mama mmoja (namshukuru sana) alinipokea vizuri nikamueleza story nzima na nia ya kuja kwangu ofsin kwake. Bimkubwa akanambia Gari hazijapita pale bandarini na kuhusu usajili na kibari nipeleke plate numbers TRA (kulekule nilikoletewa dharau) pia kuna ofisi kama tatu alinielekeza nifatilie uhalali wa zile gari hapa Tz.

Ikabidi nirudi TRA tar 13 j5 nikakakuta kale kadada tena ikabidi nikakwepe niingie ofis nyingne but nikaambiwa muhusika ni kalekale kadada duh! Nikaona isiwe kesi nikazama ndani kale kadada kakajifanya hakanijui hakajawahi kuniona ofsini kwake nami nikabadili gia angani nikakaambia nimekuja kama mmiliki wa magari anaetaka kujua tar ya mwisho yakulipia, kakaniomba kadi kakakagua kakasema mbona gari ni za kampuni? nikajibu nimekunja sura ko zakampuni hazilipiwi? Kakanambia kamuuliza mke wako, Nikatoka ofsini kwa hasira kwa bahati nikakutana na mwanangu mmoja tulisoma nae Tosamaganga (advance) anaitwa Mudi , nikamuelezea tukio ndo akachukua documents nilizokuwa nazo akazama ndani akapita nukta kwa nukta tukiwa nae ofsn huku kale kadada kakinitazama (mana walikuwa ofis moja japo meza yake ipo mbali sana na mudi) Mudi kwa mamlaka yake huku akiwasiliana na jamaa zake wa sector zingne husika tukagundua zile gari zliingia nchini kutokea Kenya hivyo ile kampuni imefanya kazi Nakulu kenya kabda yakuja bongo Ila zipo kiuhalali .

Wakuu kama mlivyonishauli nichukue Vanguard so nikawafata kuwaambia kama nachukuwa Vanguard wakanambia nirudishe card ya Harrier nikawapa wakasema kesho tunaitaka kwanza hiyo gari ulochukua nikaona poa tu mana nina kadi yake. Kesho yake nikaipeleka ile gari kufika wakanambia niwaendeshe twende sehem nikawapeleka mara tukafika "Tanroad" hapo ndo walipokuja kunivuruga baada yakunambia kuwa zile gari zinatakiwa kubaki under Tanroad na ndo makubariano ya uingizwaji wake toka bandarini na zina special offer as under government ownership nikawaambia kuhusu deni langu wakasema mtajuana mnalipanaje ila si kwa kumilikishana gari za serikali. Nikaona kuna picha inachezwa mana nimeshapita bandarini gari hazjapita pale afu huku naambiwa mavitu mengne tofauti kabisa .

Kiukweli walinipiga mkwala sana nikaona isiwe kesi nikajifanya mpole nikasema nitawajibu . Nikamfata Mudi nikamuelezea ilivyo akasema pw nimuachie atafte ukweli. Tar 13 / 4 nikiwa moja kati ya ofisi yangu pale ubungo liverside nikakutana na Mudi akiwa na mmoja kati ya wafanyakazi wa "tanroads" ambae alikuwepo kipindi napigwa mkwara jamaa akanichukua tukaenda pale mawasiliano kuna cafe flan kama unashuka stand ya mawasiliano mkono wa kulia . Jamaa akanipa mchezo wote juu ya ile inshu na ukweli ni kwamba kuna misunderstood kati ya wale jamaa (wachache) wa Tanroad na ile kampuni na ni baada yakujifanya hawataki madili ko wale jamaa wa Tanrd wanawasumbua sana kabda hata ya kumaliza mradi na ndo mana wale wachina wakataka kunipa gari ili kupunguza usumbufu mana wanafatiliwa sana na yote hayo ni baada ya kushindwa kushindwa kuwapa hati mbaya mana ile kampuni pia ni kubwa.
Sasa Mudi na yule mshkaji anaitwa Robart wakasema watanipambania basi mpaka mwezi wa 3 nikawa sijapeleka gari naskilzia tar 25 March nikakutanishwa na boss mmoja wa Usalama nikamuelezea akaja hotel walipo wale wachina akatukusanya akasema hiyo michezo huw ipo na miradi mingi inayofanyika tz baada yakukamilik huwa kuna viongozi hasa wa Tarura na Tanroad huwa wanajigawia baadhi ya mali. Jamaa akawafata wale jamaa wa tonrd akawapiga mkwara nikawa nimepona hivyo. Chakushangaza Wale wachina wakanirudishia ile Harrier wakataka niwaongezee kama usd3000 wakasema nimewaponeshea vitu vingi pia nimefanya nao kazi kwa uaminifu nakujitoa kwao katika nyakati ngum huku nikiwa silipwi mishahara yangu kwa wakati.
Kadem gani hako ka TRA kana behave kama kako nyumbani kwake!!?
Ebana hebu turudi sote nikakachape vibao....
watu kama hao hawatakiwi ofisi za uma
 
Aliyekukutanisha na boss wa usalama ni nani na n usalama gani
Mjini connection mkuu na kuongea na watu vizuri.

Wakati fulani mwaka jana nilikuwa na shida na baadhi ya vitu vilihitaji signature na mihuri ya wakuu wa idara kama mbili za serikali moja nikafanikiwa nyengine ndani ya week mbili sikufanikiwa hata kugusa kitasa cha mlango wa mkuu wa idara husika zaidi secretary na walinzi wananirudisha mara njoo baadae njoo kesho njoo baadae njoo kesho,siku moja baada ya kuchoshwa na danadana zao nikawaomba waniambie exactly ni siku gani atakayokuwepo huyo boss wao wakaniambia siku imefika nimeenda wananiambia hajafika nikakwaruzana nao nikaona na issue yenyewe niachane nayo maana inanipotezea muda wangu mwingi.

Wakati nipo njiani kurudi sehemu yangu ya kazi nikakutana na jamaa yangu nikawa namuelezea anipe ushauri nifanyeje mara katikati ya mazungumzo yetu akawa anapita jamaa mmoja simple sana,i mean simple humdhanii akaja yeye tulipo akatusalimu wanafahamiana na mshkaji wakasogea pembeni wakaongea ongea mara wakanirudia yule jamaa akaniuliza umekwama wapi na baada ya hapo utaenda wapi?kufupisha story alipiga yeye simu kumuuliza mtu (sikujua ni nani) kumuuliza kama yupo ofisini na sikujua upande wa pili ulijibu nini ila akaniambia chukua namba ya simu hii rudi pale ulipotoka ukifika mpigie mwambie (akanitajia jina) kanituma kwako,kumbe ni namba ya yule mkuu wa idara kufika nikampigia akanifungulia yeye mlango na hata yeye alishangaa akaniuliza “Huyu mtu umejuana nae vipi?”

Alinipa na namba yake nilipotoka pale ili kukamilisha ile ishu kila nilipokuwa naingia na ambako kabla sijakutana na huyu jamaa nilitumia zaidi ya siku mbili ili kusikilizwa nilikuwa nikisema fulani amenielekeza nije hapa nimuone fulani wenyewe walikuwa wananielekeza.yaani kitu nilichofuatilia karibia mwezi nilikuja kumaliza ndani ya siku moja na ½ ila yote ni kwa sababu ya connection.
 
Baadhi ya wadada au wanaume wenye tabia hizi makazini aidha wanamahusiano kimapenzi na bosses, ukaribu wa kikabila, kigodfather, makuwadi, mashemeji wa mabosi, dawa za kichawi hasa mazombi, baadhi ni hulka za asili na kunachangamoto ofisi nyingi za umma hazina miongozo,nyaraka na taratibu za uadilifu na unyenyekevu katika kuhudumia wateja wao. Na hasa idara ambazo zina taswira kama ya kutegemewa na zenye hulka ya utisho sana mfano TRA, Tanesco, tanroads, tarura, ofis ya mkurugenzi, ofis xa elimu, ofis za malipo ya ada, ofisi za mitihani, lipo jambo haliko sawa tanzania kwenye kuhudumu maofisi kwa namna ya kumfanya mteja ama mgeni aondoke na sifa bora ya kusikilizwa au kutatuliwa tatizo au kushauriwa na kuelekezwa au kufamishwa vema.

There is something lacking among us across all spheres in our portifolios or rather dockets. I dearly submit for imminent desirable reforms.
It's true brother. Na ofis yenyewe ni TRA wilaya ya Ilala pale kuna dem mrefu mweusi ana penda kuvaa earphones. Pia kuna jamaa mweupe anasifika kwa kukadiria kodi za ajabu ili kutengeneza mazingira ya rushwa (kwa mfn kodi yako ni 20000 anakukadiria 100000 ukilialia ndo anakwambia atakupunguzia ila umpe chochote ukikubari ndo anakuwekea viwango vya kawaida unamshukuru unajua kakusaidia na pesa unampa kumbe ushapigwa)
 
Aliyekukutanisha na boss wa usalama ni nani na n usalama gani
Muddy alinikutanisha na mkuu wa idala flan ivi yule mkuu ndo akatutambulisha kwa yule jamaa kama wadogo zake ko jamaa akalibeba kama lake. Ni usalama wa taifa mzee . Wale jamaa huwa wanajua kila k2 kinachoendelea hapa bongo ( salute kwao)
 
Kama maelezo ndio yameishia hvyo. Hilo gari sio lako na hauna uhalali wa kuliuza ama kumpatia mtu mwengine yeyote na kuendelea kuwa nalo litakuletea shida.. kwa maelezo hayo hilo tatizo mmelitatua kienyeji sana Mkuu, hautambuliki ktk mamlaka yoyote kama ww ni mmiliki halali. Ulipaswa kubadili kadi ya gari kwanza na magari mengi ya miradi uwa yana exemption na ili gari ibadilishwe umiliki kwenda kwenye umiliki binafsi ni lazima ile kodi iliyokuwa exempted ilipwe na kama kulikuwa na kodi zingine kampuni inadaiwa lazima izilipe mana kwenye kufanya transer lazima itahitajika tax clearance ya kampuni.
Shikamoo kaka .. yani umepita mulemule kama ulikuwepo. .. Nawashukuru sana wadau wa JF mlinishauri yote haya na tumeyafanyia kazi na kuna mwanasheria asha play part yake ko kila k2 kipo sawa sema nimeshindwa kuandika yote. Shukran sana kaka. Ila janja janja za kukwepa kodi ndo hazikosagi mkuuu. hahahahahhahahaha
 
Dah! Una bahati sana.
maisha ya kibongo haya kumiliki gari kubwa ni shughuli kweli.

Mimi pale kahama mining nimeservice miaka 4 kabla sijatupiwa virago lakin sikununua

Huwa najuta sana.sidhan kama nitanunua tena.
hiyo ndo athari ya kufanyia kazi migodi ya vijijin.
Kaka sema hukunifatia post yangu ya kwanza kiufupi hawa jamaa nimefanya nao kazi zaidi ya mwaka mmoja but tukasumbuana kwenye malipo baada yakuwapiga mkwara na kuzuwia baadhi ya mali zao ndo wakanipa hizo gari mbili nichague moja ili tu compensate na deni langu .. nilileta uzi humu kuomba ushauri ndo nikaambiwa niwe makini nisiuziwe mbuzi kwenye gunia
 
Dah! Una bahati sana.
maisha ya kibongo haya kumiliki gari kubwa ni shughuli kweli.

Mimi pale kahama mining nimeservice miaka 4 kabla sijatupiwa virago lakin sikununua

Huwa najuta sana.sidhan kama nitanunua tena.
hiyo ndo athari ya kufanyia kazi migodi ya vijijin.
Migodi ya vijijini ina shida gani mkuu?
 
Kadem gani hako ka TRA kana behave kama kako nyumbani kwake!!?
Ebana hebu turudi sote nikakachape vibao....
watu kama hao hawatakiwi ofisi za uma
Kapo ofisi za TRA wilaya ya Ilala ni keusi karefu. Siku ukipita maeneo yale hebu ingia ofisin watazame vizuri staff wa mule utakaona huwa kana jifanya kapo bzebze hivi
 
Back
Top Bottom