Mrejesho baada ya kuanza kutumia software ya 'Gavana' kwenye biashara

Mrejesho baada ya kuanza kutumia software ya 'Gavana' kwenye biashara

Hommy

Senior Member
Joined
Mar 23, 2023
Posts
107
Reaction score
249
Baada ya kukutana na mjadala wenye kichwa cha "Mnatumia program gani ku-manage biashara" niliona jibu la mtu aliyesema anatumia programu ya Gavana. Baada ya kusoma maelezo yote kwenye hiyo thread, niligundua kuwa ni matamanio yangu kuendesha biashara kupitia programu maalum itakayoniwezesha kufuatilia mzunguko wa biashara.

Nikaona isiwe kesi, nikadownload software ya Gavana na kuanza kuitumia kwa mara ya kwanza. Kama unavyoona kwenye mshale wa rangi ya carrot hiyo ni bidhaa iliyoleta hasara.
a.png

Mshale wa kijani unaonesha sehemu ya notification ikionyesha kuwa kuna bidhaa yenye upungufu wa stock.

d.png

Kwenye picha ya pili, hii ni sehemu unayopangilia njia za mauzo. Mfano, unapouza simu, unaweza kuweka mpangilio kuwa mteja akinunua simu kuanzia kumi, bidhaa hiyo itakuwa na punguzo la asilimia unayopenda, mfano 10%. Pia, kuna sehemu unayoweza kuweka riba iwapo mteja atanunua kwa mkopo. Mara tu mteja anaponunua, kiasi halisi kulingana na settings zako hujiweka automatic ikiwa bidhaa ipo kwenye settings zako haina haja ya kupiga hesabu pembeni.

Kuna sehemu nyingine ambayo sijascreenshot ya mauzo ambapo huandiki bei moja kwa moja. Mfano, ukiuza charger, badala ya kuandika 5,000, unaweka tu idadi ya charger, kisha mfumo unakokotoa bei kamili ili kuepuka makosa ya hesabu. Pia, nimetengeneza risiti kulingana na mpangilio ninaoupenda na kumkabidhi mteja.

Kwenye picha hii nyingine nyingine, utaona ripoti ya mauzo ikionyesha loss, capital, stock, profit, na zaidi.
c.png

Tukiachana na hayo yote hapa ni sehemu nyingine ya program
b.png
kibox cha kwanza chenye mshale mweupe kinaonyesha jumla ya mapato kabla ya matumizi. Mshale wa bluu unaonyesha mauzo yaliyofanyika kupitia risiti na invoice. Mshale mwekundu unaonyesha matumizi mbalimbali kama kodi, mzunguko wa kibiashara, na malipo. Mshale wa njano unaonyesha uwiano kati ya kipato na matumizi, ili ujue kama matumizi yako yako juu ya kipato au la. Ukibonyeza kibox hicho, utaona maelezo yote ya matumizi pamoja na tarehe.

Mshale wa pink unaonyesha sehemu ya kujaza iwapo unataka kuchukua kiasi fulani cha fedha na kuandika sababu. Na mshale wa kijani unaonyesha jumla ya kiasi kilichobaki baada ya mauzo na matumizi yote.

Hayo yote ni kwa uchache tu bado sija weka sehemu ya wanaonidai na ninao wadai pia inaruhusu kuuza bidhaa nyingi kwa mkopo na uuzwaji wa kutangulizia kidogo kidogo na unaweza kubadili bei ya bidhaa kulingana na hali ya soko kuliport loss na kuongeza stock kwenye bidhaa zilizopo tayari kama unavyo ona kwenye picha ya kwanza hapo juu kwenye buttons za chini.

Nimefanya majaribio kwa program zaidi ya tatu ila yingine gharama zake zipo juu baada ya kukutana na gavana naona nimetimiza kiu yangu shukrani zangu kwa Maffada baada ya kuleta uzi wake hapo juu nami nimepita humo humo tangu nii-download hii program leo ndio nimelipia baada ya kuifanyia test ni hayo tu GAVANA
 
Tangazo limeenda.
Haya taja na bei yake
Seems alike lakini nipo kiuharisia mimi ni user tu kama wengine izungumzia unaweza kuangalia baadhi ya threads Ok
Malipo yapo kwenye program kwa kila mwezi ni elf 8,000 mkuu malipo yanafanyika kwa paypal ina trail ya wiki moja bure fanya review
 
Seems alike lakini nipo kiuharisia mimi ni user tu kama wengine izungumzia unaweza kuangalia baadhi ya threads Ok
Malipo yapo kwenye program kwa kila mwezi ni elf 8,000 mkuu malipo yanafanyika kwa paypal ina trail ya wiki moja bure fanya review
Sawa nitaicheki nina kazi nayo
 
Back
Top Bottom