Mrejesho baada ya kung'oa jino. Shikamoo Jino

Mrejesho baada ya kung'oa jino. Shikamoo Jino

grandMullah23m

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2017
Posts
245
Reaction score
331
Jamani nawaasa na kuwaomba chondechonde tuliheshimu jino. Jino limeniweka kwenye nusu kaput, umwamba wote, mafunzo yote ya kibabe niliyasahau[emoji119]

Nimeapa kuwa balozi mzuri kuhusu haya mambo:

[emoji117]Tuzingatie usafi wa kinywa siku zote maana haya mambo huwa yanaanza mdogomdogo kama mzaha.

[emoji117] Wenzangu mnaopiga zile bia mbili tatu(haswa zile za ofaa za kule kambini) tusisahau kusukutua hata kidogo na maji ya chumvi.

[emoji117] Kumbe sio bia tu...hata juisi tunazogida nyumbani...pamoja na akina energy...zoote hizo usisahau kusukutua na maji masafi mara baada ya kunywa.

[emoji117] HAKUNA DAWA YOYOTE MTAANI itakayotoa suluhu ya kuumwa jino...tofauti na kufika tu hospitalini na kupata matibabu (tuache kubeti na jino tafadhali, nilikuwa mbishi sana ila duh[emoji119] nimejikuta katikati ya uhai na kifo).

[emoji117] Tuache uoga kwenye kufwata matibabu...Kuna tofauti kati ya Dokta, Dakitari na Daktari....aheshimiwe sana huyu wa mwisho(Daktari).

[emoji117] Mwisho kabisa tujipende wenyewe na tuheshimu wake zetu [emoji18] nimepikiwa mtori na mke wangu na anapambania sana afya yangu...michepuko yote haisaidiagi ukifikia hapa....Mama chanja I promise..nimeacha hayo mambo[emoji119][emoji119]

Viva [emoji1241]
 
😂😂😂😂😂😂😂Hapo mwisho umenifurahisha sana, kwamba michepuko haisaidiagi.
 
Dawa ya Jino nikung'oa tu mkuu ,polee Sanaa endeleaa kulaa mtori kwanza nyama utakulaa ukiponaa
 
Mkiambiwa mle vitamin c kama kinga mnasema watu wamezidi ukisasa ungetakiwa uoze mpaka fizi.
 
Dah umenikumbusha mbali mno mno niliumwaga na hio kitu usiku alafu mvua kubwa inapiga balaa niko geto alone sina hata kipande Cha paracetamol!
Nikicheki muda hauendi nizunguka kama kichaa mpaka nikaingia chini ya kitanda(sijui niliwaza Nini!)

Saa kumi na Moja kamili nilishafika zahanati ya levolosi arusha nikalichomoa tu
 
Pia yalinde na kuimarisha meno yako kwa kutafuna vitu vigumu kama mahindi ya kuchoma.

Ni mazoezi na inasaidia sana
 
Kwan ulitafuna nn bimdada?
Too much of anything is harmful
Ukitafuna sana vitu vigumu kwa kipindi kirefu unaumiza fizi,mzizi wa jino.
I mean ni kitu ya kuja kuona impact yake hata 5-10yrs mbele huko.
 
Too much of anything is harmful
Agreed


Ukitafuna sana vitu vigumu kwa kipindi kirefu unaumiza fizi,mzizi wa jino.
Na akitafuna vilaini sana tu meno yanalainika na taya linakuwa dogo na legelege hadi linashindwa kuhimili meno na fizi vizuri. Hasara inaendelea hadi kwa watoto atakaowazaa (epigenetics) ndio chanzo cha uhitaji wa braces kwa watoto wa kishua/kidhungu.
Ni afya meno yapatiwe mazoezi kwa kiasi mfano kutafuna mahindi ya kuchoma au miwa hapa na pale.
Lakini isichukuliwe kwamba nashabikia kufungua bia/soda kwa meno au kuvunja mifupa. La. Ni zaidi kama kumwambia mtu ale na makande sio uji pekee.
 
Back
Top Bottom