Mrejesho biashara ya madini 'third season'

Huku wingi wa germstones utashangaa.unaweza ukapata alexandrite ukaidharau gold maana bei ya germstones ni juu zaidi ya gold. Though wanunuzi wa germstones ni wengi sana pia hasa wa srilanka
Tatizo la biashara ya Gemstones ni kwenye ununuzi wake hasa hasa kwa hawa Wasrilanka, hawana bei maalum wala vipimo = ni suala la kukadiria tu. Unaweza leo ukawa na Gemstone Y ya uzito wa gram 2 akanunua kwa bei X lakini ukileta baada ya muda fulani na aina ile ile na labda bora nzuri zaidi, anaweza kununua kwa bei ya X-1! Hapo ndio kwenye ngoma, si sawa na dhahabu hasa baada ya kuwa na masoko yake ambapo kila kitu ni WAZI! Nadhani Serikali inabidi pia iingie na kuingilia hii biashara ya Gemstones. Kuna pesa sana nako huko!
 
Kuna exporter/trader 1 dsm ananuaga madini yangu kwa bei tamu sana.ananiletea wateja kutoka us na wahapahapa bongo madealer napatana nao kupitia yeye then namuachia yake ya ofisi.ivo tu.yuko poa sana

Yaani mimi ninachoangalia ninapouza madini yangu nataka bei ya soko staki janja janja dalali aniletee wateja namlipa mimi
 
Sawa, lakini ni wachimba wadogo wa gemstones wangapi wenye fursa kama yako!? Ndio maana naitaka Serikali iingie na huko na ifanye kama ilivyofanya kwenye dhahabu na Tanzanite ili wote tufaidike.
 
Hizi gemstone nadhan znapatikana wilaya ya TUNDURU maana huko wasrilanka ndio wamejazana Sana
 

Wakuu nauliza vipi nafasi ya mafundi mitambo katika kutengeneza mashine za uchimbaji na uchenjuaji hasa kwa anae taka kujiajiri mwenyewe au kuajiliwa nauliza kwakuwa sijawahi fika katika mgodi wowote.
 

Masalakulangwa ule mwala. Mihayo wayombile iko getegete..
 
Ppm ni parts per million. Mfano 6ppm ni sawa na kusema 6 gramu za Dhahabu kwa tani moja ya mchanga au sinate. Kwahiyo ni sawa na kusema kuna gramu 6 za Dhahabu kwenye gram milioni moja (tani 1) za mchanga
 
Ppm ni parts per million. Mfano 6ppm ni sawa na kusema 6 gramu za Dhahabu kwa tani moja ya mchanga au sinate. Kwahiyo ni sawa na kusema kuna gramu 6 za Dhahabu kwenye gram milioni moja (tani 1) za mchanga
Asante sana Msomi wangu kwa elimu hii ingawa imechukua muda kidogo kujibu, nadhani ni kwa wingi wa shughuli huko Makongorosi. Kongore for everything and keep it up. By the way bei ya dhahabu sokoni, ukilinganisha na bei ya machimboni, inatia moyo na hamu ya kufanya biashara hii. Tutawasiliana Msomi wangu.
 
Asante sana kaka nmefuatilia uzi huu vizuri sana naomba nikushukuru tena na tena umenifungua macho na umenipa nguvu ya kuwashinda wakatishaji tamaa.
 
Mkuu hivivhuu uchimbaji wa gemstone mnatumia nini kugundua mwamba wake
 
Congratulations and keep it up
 
Mashine zipi wanatumia kupimia au n hizihizi detectors zinazotumika kupimia dhahabu kabla ya uchimbaji
Kuna mashine za ku - detect vito au gemstones; hizi ni tofauti na za dhahabu! Si unajua dhahabu ni aina ya chuma au metal, lakini gemstones siyo metal! Hivyo mashine zake ni tofauti ila unaweza kukuta kwenye mashine ya ku - detect dhahabu ikawa na setting ya ku - detect vito au gemstones.
 
Sawa kaka nmekupata uzuri hapo ubarikiwe
Pia nna mashine moja inaitwa fisher gold bug2 inapima 1m deep sjawahi kuitumia ila iko ndani tu vp hii unaeza kuwa na unauelewa nayo
 
Hahaha nimecheka kishenzi, hizo ndio lugha zetu huko kwenye migodi

excavator kule tunaita skaveta

jaw crusher tunaita jograsha
Ebu nipe ufunuo kuhusu hivyo vijiko.
kazi zipo ?
 
Sawa kaka nmekupata uzuri hapo ubarikiwe
Pia nna mashine moja inaitwa fisher gold bug2 inapima 1m deep sjawahi kuitumia ila iko ndani tu vp hii unaeza kuwa na unauelewa nayo
Hapana siijui ila from the name naona kama ni ya ku - detect dhahabu! Kwa nini usiende nayo field - labda Chunya au Geita au Bunda, mkoani Mara, sehemu moja inaitwa KINYAMBWIGA. Huko kuna machimbo ya dhahabu unaweza kui - test huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…