Wakuu, hongereni kwa mapambano ya hapa na pale katika kuutafuta mkate wa kila siku, pengine kutengeneza ziada ya kufaa kesho.
Mniwie radhi kwa kuwa niliahidi kila baada ya miezi sita nitakuwa nadondosha mrejesho wa mahali nilipo katika safari yangu kwenye madini. Nikili tu kuwa mambo yamekuwa mengi mno na muda mwingine najikuta naisahau kabisa jamii yangu ya hapa jf ambayo imekuwa mhimu mno katika mapambano yangu kwa kunitia moyo, kunishauri na kunikosoa pia.
Kama ndio mara yako ya kwanza unaingia kwenye uzi huu naomba niambatanishe link za season zilizotangulia.
First season
JamiiForums mobile app
Habari za mda huu mabilionea wa sasa na wajao. Tumaini langu mnaendelea vema na harakati za kutimiza ndoto zenu. Ni kama mwezi nilikuja kuomba msaada kwa wajasiliamali wenzangu juu ya biashara ya dhahabu. Nishukuru watu walitoa uzoefu wao, wapo walionitaadhalisha juu ya songombingo zilizopo...
Second season
Panapo majaaliwa ya mwenyezi Mungu tumekutana tena kwenye kikao cha wapambanaji. Wakuu wa jukwaa hili hususani vijana nawasalimu kwa Salam adhimu ya mama yetu Samia Suluhu Hassan...... Bila kuwachosha ni kuwa tangu nimeianza safari yangu ya kibiashara nimekuwa nikiwashirikisha hatua...
Third season
Salam zangu na zisambae kwenu nyote. Matumaini yangu mu buheri wa afya tele, na hata walioteteleka mwenyezi Mungu awajaalie wepesi wa kupona haraka. Ahadi ni deni. Nami tangu nimeanza mbio zangu za kibiashara kwenye madini ya Dhahabu nimekuwa na tendency ya kuripoti wapi nimefikia kila baada ya...
Wakuu mpige kambi maana nakuja
Fourth season.
Msimu huu wa nne kwangu ulikuwa msimu wa mavuno. Baada ya kazi ya mwaka mzima wa kusaga na kukusanya mchanga wa dhahabu, hatimae mwezi June nilipeleka plant kuchenjua.
Labda tu nifahamishe kuwa nilibeba gari 30 zenye ujazo wa tani kumi. Sample baada ya mchanga kuchanganywa kwenye ubebaji ilisoma 3.5 ppm. Copper pia ilikuwa inasoma 750. That was not surprise kwa sababu mwanzo nilisaga mawe ya kutoka sehemu tofauti.
Changamoto nilizokutana nazo ni.... Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuchenjua hivyo niliogopa kuibiwa mnoo. Mkemia niliyempata hakuwa competent na hiyo nilikuja kujua tayari tupo mzigoni. Yaani ni kama alishindwa kuidhibiti vizuri copper.
Ila yote kwa yote tulijitahidi na ukubwa au uwingi wa mzigo ukanibeba. Kutoka kwenye makadilio ya kilo mbili....nilipata gram 860. Asilimia pia ilisoma 97. Hapo approximately nilipata kama milioni mia moja na tatu. Ukitoa gharama za uchenjuaji na kulipa vijana wa kazi, inabaki kama milioni sabini
Nilijiona kama nimekosa, maana hesabu zangu zilikuwa kwenye milioni mia mbili plus na nilishawaza kutafuta leseni ya dealer ili ni-trade dhahabu kwenye viwango vya juu zaidi.
Kitu ambacho nimejaaliwa na huwa nakiona kama baraka ni kujiona kwenye nafasi ya ushindi kwa kila ninachokipata haijalishi udogo au ukubwa. Kwangu mimi milioni sabini ilikuwa great reservation. Kwanza kwenye maisha yangu na utafutaji wangu sijawahi kuipata hapo kabla.
Malengo yamefeli.... Milioni sabini haziwezi kuwa dealer. Hivyo nimejenga nyumba ya kuishi standard, pia naendelea na biashara ya dhahabu. Hela nyingi nimeirudisha kazini ambako tayari nakuza mlima. Kiufupi hela ya dhahabu ni tamu mnoo, sijui kama ipo siku nitakuja kuacha shughuli hii.
Nimalize kwa kusema kuwa.... uchimbaji ni kama biashara ya madawa ya kulevya kwa namna hela yake inakuja kwa kasi. Ukiwa serious with a capital within 3 years utakuwa billionaire believe me.
Mungu atujaalie uzima na rehema, tuishi maisha ya ndoto zetu. See you on the fifth season.