Mrejesho; Biashara ya madini ya dhahabu... fourth season

Mrejesho; Biashara ya madini ya dhahabu... fourth season

Mkuu mcrounmj kwanza hongera sana kwa hatua uliyofikia inshallah utafikia ndoto zako. Kuna mwanangu nae kavuna kiasi kama chako huku huko ulipo, I wonder kama ndo wewe ha ha

Kwa mahesabu yangu naona umepata unachostahili kutokana na rundo ulilokuwa nalo wala mkemia hajakuangusha, in other words you overestimated your calculations.

Tani 30 x 10 = 300.
300 x 3.5ppm = 1050

Kumbuka huwezi vuna zaidi ya 70% kwenye leeching VAT. Na copper yako ilikua ndogo sana which is a very good thing.

So, 1050 x 0.7 = 735. Hizi ndio gram ulizotakiwa kupata, wewe umepata 860 na purity ya 97. That's very high.

Mkemia kafanya kazi kwa weledi wa juu sana, in this business mkemia akikosea unaweza usipate kitu kabisa maana there's no reversing.

Hongera chief.
how
 
Nataka kujua wakati unaanza ulikiwa na vibali vyote vya kuwa broker au ulianza kibishi tu ukatafuta vibali baadae
 
Nataka kujua wakati unaanza ulikiwa na vibali vyote vya kuwa broker au ulianza kibishi tu ukatafuta vibali baadae

Simjibii ila unaweza kuanza either way. Ni vyema ukatafuta vibali kwanza ila unaweza kuanza either way ni bongo sio mbele huko.
 
Kwa biashara zetu hizi za kawaida, ni vizuri uwe na Business Name tu inatosha kukuendeshea biashara zako bila shida; haya ma LTD COMPANIES yana shida na complications nyingi zcomplications!isizo za lazima na wajanja au wajinga ni wengi tu kwenye eneo hilo kwa ajili ya hizo
habari kiongozi. upo sahihi lakini haupo sahihi
 
Kapicha ka dhahabu
Hii hapa purity yake 97%

Kwa week mm kupata grm 80 kitu cha kawaida kutokana na mitego yangu

Wale wakatao omba connection wasubirie kidogo maana bado kwanza
Namfukuza mwizi kmya kmya

Ova



IMG-20220612-WA0018.jpg
IMG-20220628-WA0014.jpg
 
Nataka kujua wakati unaanza ulikiwa na vibali vyote vya kuwa broker au ulianza kibishi tu ukatafuta vibali baadae
Mkuu ilibidi nitafute kwanza maana nilijaribu kidogo tu kabla ila wale waliokuwa wanajiona magwiji walinipiga bit na kutishia kuniitia police

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Wakuu, hongereni kwa mapambano ya hapa na pale katika kuutafuta mkate wa kila siku, pengine kutengeneza ziada ya kufaa kesho.

Mniwie radhi kwa kuwa niliahidi kila baada ya miezi sita nitakuwa nadondosha mrejesho wa mahali nilipo katika safari yangu kwenye madini. Nikili tu kuwa mambo yamekuwa mengi mno na muda mwingine najikuta naisahau kabisa jamii yangu ya hapa jf ambayo imekuwa mhimu mno katika mapambano yangu kwa kunitia moyo, kunishauri na kunikosoa pia.

Kama ndio mara yako ya kwanza unaingia kwenye uzi huu naomba niambatanishe link za season zilizotangulia.

First season JamiiForums mobile app
Second season
Third season
Wakuu mpige kambi maana nakuja


Fourth season.

Msimu huu wa nne kwangu ulikuwa msimu wa mavuno. Baada ya kazi ya mwaka mzima wa kusaga na kukusanya mchanga wa dhahabu, hatimae mwezi June nilipeleka plant kuchenjua.

Labda tu nifahamishe kuwa nilibeba gari 30 zenye ujazo wa tani kumi. Sample baada ya mchanga kuchanganywa kwenye ubebaji ilisoma 3.5 ppm. Copper pia ilikuwa inasoma 750. That was not surprise kwa sababu mwanzo nilisaga mawe ya kutoka sehemu tofauti.

Changamoto nilizokutana nazo ni.... Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuchenjua hivyo niliogopa kuibiwa mnoo. Mkemia niliyempata hakuwa competent na hiyo nilikuja kujua tayari tupo mzigoni. Yaani ni kama alishindwa kuidhibiti vizuri copper.

Ila yote kwa yote tulijitahidi na ukubwa au uwingi wa mzigo ukanibeba. Kutoka kwenye makadilio ya kilo mbili....nilipata gram 860. Asilimia pia ilisoma 97. Hapo approximately nilipata kama milioni mia moja na tatu. Ukitoa gharama za uchenjuaji na kulipa vijana wa kazi, inabaki kama milioni sabini

Nilijiona kama nimekosa, maana hesabu zangu zilikuwa kwenye milioni mia mbili plus na nilishawaza kutafuta leseni ya dealer ili ni-trade dhahabu kwenye viwango vya juu zaidi.

Kitu ambacho nimejaaliwa na huwa nakiona kama baraka ni kujiona kwenye nafasi ya ushindi kwa kila ninachokipata haijalishi udogo au ukubwa. Kwangu mimi milioni sabini ilikuwa great reservation. Kwanza kwenye maisha yangu na utafutaji wangu sijawahi kuipata hapo kabla.

Malengo yamefeli.... Milioni sabini haziwezi kuwa dealer. Hivyo nimejenga nyumba ya kuishi standard, pia naendelea na biashara ya dhahabu. Hela nyingi nimeirudisha kazini ambako tayari nakuza mlima. Kiufupi hela ya dhahabu ni tamu mnoo, sijui kama ipo siku nitakuja kuacha shughuli hii.


Nimalize kwa kusema kuwa.... uchimbaji ni kama biashara ya madawa ya kulevya kwa namna hela yake inakuja kwa kasi. Ukiwa serious with a capital within 3 years utakuwa billionaire believe me.

Mungu atujaalie uzima na rehema, tuishi maisha ya ndoto zetu. See you on the fifth season.
Nakubali, I wish nami nipate muda niletee season yangu ktk hii sekta. Hela ya dhahabu ni tamu vby mno....
 
Binafsi nilianza na mtaji WA laki 5 chimbo Moja mkoani Shy,
Week ya Kwanza ya biashara nilipata faida ya gramu nzima kabla sijaenda jikoni kuchimba.

Siku nilipoenda kuchoma nikaibiwa gramu nzima na hasara ,pesa ikappungua

Nili-last 2 months kwenye business nikapotea

Najipanga tena wakati ujao nirudi kwenye game kwakuwa nimejifunza vitu vingi na makosa nilivyofanya..
 
Binafsi nilianza na mtaji WA laki 5 chimbo Moja mkoani Shy,
Week ya Kwanza ya biashara nilipata faida ya gramu nzima kabla sijaenda jikoni kuchimba.

Siku nilipoenda kuchoma nikaibiwa gramu nzima na hasara ,pesa ikappungua

Nili-last 2 months kwenye business nikapotea

Najipanga tena wakati ujao nirudi kwenye game kwakuwa nimejifunza vitu vingi na makosa nilivyofanya..
Ulijuaje jikoni umeibiwa gram 1 hadi ukaamua kusema hivyo?
 
Back
Top Bottom