Mrejesho; Biashara ya madini ya dhahabu... fourth season

Upo sahihi mkuu,na mara nyingi maboss hukimbilia kusema mkemia kazingua.
 

Mwanzo ppm ilikua 8 kama sikosei
 
Ni kwema wakuu habar za siku tupeane location wapi tufunge karasha maana huku shilalo Kwa SASA njaa ni Kali, material adimu ,Kwa SASA gharama za uendeshaji ni mtiti bin mufilis

Shilalo iko wapi
 
1) Je , ni kweli kuwa 'carbon' ipo feki? If YES, carbon genuine au feki naitambuaje?

2) Je, ni kweli kuwa wauzaji carbon huuza carbon used kwa udanganyifu? i.e. used carbon 'inaoshwa' kisha wanarebag na kuiuza as 'new'. Naamanisha mteja anaaminishwa carbon ni 'mpya' lakini kumbe ni used.

3) Brand za carbon zipo nyingi. Je, kwasasa, ni kampuni gani ya cabon ambayo ni the best?

4) Je, cyanide nayo pia ina ufeki feki kwenye soko? If yes, feki naitambuaje? na brand gani ni the best?

5) Je, ni kweli kuwa kwenye Vat leaching plant hufanyika uhuni (kimagumashi) wa kubakisha dhahabu kwenye kapi? If yes, wanafanyafanyaje?

6) At Elution Plant, Je ni kweli kuwa jikoni ndipo pana uhuni mwingi Sana ili kuiba dhahabu ya mteja? Dhahabu baadhi kubakia kwenye mfumo wa uchomaji. Inasemekana wanaingiza (kiharamu) steel wires mle ndani ya pipes ili kuiba dhahabu ya mteja. Hili lipoje?

7) Maji ya kuoshea/kusafishia dhahabu (sokoni). Je ni kweli kuwa kuna Maji feki wanatumia wanunuaji wahuni ili kuishusha 'purity' ya dhahabu?

8) Kuanzia ''Vat leaching plant (kuozesha)'' hadi "Elution Plant (jikoni/jikoni)" hadi sokoni (kuuza dhahabu)... kwa mtu ambaye ni mgeni kabisa kwenye game anaenda mara ya kwanza (totally BEGINNER), azingatie na ajisimamie kwenye mambo gani ili 'asipigwe'?

Cc: Bufa , mcrounmj , Nasibunduki , Nizhneserginsky , Kiduila , Mwanamaji , mrangi .

-Kaveli-
 

Mkuu, hapa ndo natamani JF ingekua na sehemu ya voice note ningekujibu kwa kina maana nikisema nijibu yote haya kwa maandishi itabidi nitafute muda nitulie kuandika.

In a nutshell, hii biashara inahitaji kujuana, usimamizi na uaminifu wa hali ya juu. Any mistake has no reverse unakula hasara maradufu. Wapigaji ni wengi kuliko waaminifu japo waaminifu wapo. The more you have control of the processing chain the better.
 
Ni maswali muhimu sana inabidi yafanyiwe utafiti wa kina, kwa dunia ya leo ni kuwa makini, au kama kweli mtu anataka kuwekeza huko ni kuwa na plant yako mwenyewe.
 

Okay.

-Kaveli-
 
Ni maswali muhimu sana inabidi yafanyiwe utafiti wa kina, kwa dunia ya leo ni kuwa makini, au kama kweli mtu anataka kuwekeza huko ni kuwa na plant yako mwenyewe.

Yep, that's it mkuu. Kama una sufficient capital, unajenga Vat leaching plant yako mwenyewe + Elution plant yako mwenyewe, to be on safe side.

Otherwise, watu wanapigwa mno mno kwenye hii bizna ya uchenjuaji dhahabu.

-Kaveli-
 
Ngoja nijaribu kukujibu kwa vitu vichache kulingana uelewa wangu,
Issue ya kaboni kuwa feki au original sio issue Sana kwenye kuozesha sababu kazi ya kaboni Ni kushika dhahabu so ikitokea kaboni Ni feki tanks zinakuwa hazikati sababu dhahabu inakuwa inazunguka ikitokea Hali hiyo unaongeza kaboni au unasafisha hiyo kaboni kwa kutumia acid

Sokoni Kuna mchezo wa kuweka maji machafu kupunguza purity ya dhahabu lakini now days sokoni tunatumia vipimo sio vya maji hii Ni ngumu kidogo kuchezewa mchezo,ipo hivi sokoni Kuna watu wa madini ofisi ya madini kabla haujauza dhahabu wanaipima wao then unaenda kwa dealer so madini wanatuma kipimo Cha exray which are the best

Yes unaweza kujenga elution au plant yako ,plant nzuri Hadi ikamilike Ni almost 30M na ellution almost ,150M
Wizi mwingi wa plants Ni kuvamiwa na watu kuiba kaboni

Wizi mwingi wa elution kuweka stillwire sahemu isiyo rasmi hapa unaweza kwenda na fundi ukague mashine before haujapandisha mzigo.
Wizi mwingine ambao watu hawajajua ipo hivi,ukipeleka mzigo ,wanapakia kwenye mashine then wanawasha Sasa katikati wanakuzimia transformer hapo piga ua stillwirehaishiki dhahabu means dhahabu inabaki kwenye kaboni Sasa wakati wa kushusha wanakubafilishia kaboni solution uwe makini wakati wa kuwasha mashine kila muda uwe unakagua heater zote zinawaka , transformer inawaka na pamp inawaka muda wote kimoja kisipofanya kazi dhahabu inabakia kwenye kaboni
 
Ukienda kuozesha marudio Kama unakodi plant hakikisha unatumia mkemia wako ili asiache dhahabu kwenye kapi,jitahidi wakati anafanya colour test unakuwepo asikate tanks bila kupima hapo itamsaidia kuvuna dhahabu yote kawaida kwenye kapi lazima dhahabu ibakie so ilibakia 0.4 ppm sio mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…