Mrejesho (feedback): Nina Shilingi Laki moja na nusu, ni mwanafunzi, naweza fanya biashara gani?

Weera weraaaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
740
Reaction score
657
Habari Wakuu?

Nilikuja hapa jukwaani 29.04.2014 na kuomba msaada wa wazo la biashara.

Nashukuru wote mlio changia, kwani May Katikati nilianza kununua pens na daftari & stationaries zingine na kuuza chuoni.
Hivi ninazungumza nina mtaji wa sh. milion moja na laki sita na nazidi kutafuta fursa za kuwekeza kusonga mbele.

Ahsante sana Bulldog, King Octavian, Mama Joe, delly, Mbunda E, Coping Strategy, maringeni Na Exorcist na wengine wote mlio changia chochote pale, Mungu awabariki.

Msinichoke nikija kuomba msaada wa mawazo zaidi.

VIVA JF!!
 
Nicheki 0714883861 nikuongezee idea inayoweza kukuongezea kipato
 

Safi sana inaelekea umetulia kaza buti ndugu....
 
Nicheki 0714883861 nikuongezee idea inayoweza kukuongezea kipato

Wewe unafikiri idea iliyompatia 1.6M kutoka kwenye laki mbili aliipata kwa simu? Watu walifunguka hapahapa watu wakajadili mhusika akachambua akaanza, wewe unataka akupigie simu mkutane sehem mzungumze vizuri huku mnakunywa kilimanjaro siyo? Funguka hapa kama aidea ni viable, inginevyo utaonekana tapeli unataka kumwingiza mjini mwanafunzi...dhambi!
 
Nicheki 0714883861 nikuongezee idea inayoweza kukuongezea kipato

Kwani hujasoma maelezo ya mtoa hoja, kaja jamvini kushukuru. Nani kakwambia kaja kuomba nawazo ya kuzungusha hizo mil 1.6. Umekaa kifisadi tu kama kiongozi wa chama tawala.
 
Ahsante mkuu Kigogo, hizi ndizo akili amekupa mwenyez Mungu,na nikikulaumu nitakuwa nakufuru.
Jaribu basi hata kusoma mada kabla ya kuchangia.
ubarikiwe.
Ndio JF Senior Expert Member hao kazi yao. Huyo Kigogo ana posts 16,910 hivi unafikiri kazipataje? Kazi yao ndio hiyo mitusi na kuchangia kila post hata kama hana cha kuchangia cha kujenga anaharibu. Watu makini kama Malila wanaokuja kutoa mawazo ya kujenga humu chunguza tarehe walizojoin JF na idadi ya posts zao utaelewa.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu Kigogo, hizi ndizo akili amekupa mwenyez Mungu,na nikikulaumu nitakuwa nakufuru.
Jaribu basi hata kusoma mada kabla ya kuchangia.
ubarikiwe.
Mungu hatoi akili kama za Kigogo usimsingizie
mtu kama huyu ni wakumpuuza tu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…