Mrejesho: Hatimaye nimejilipua

Mrejesho: Hatimaye nimejilipua

8.5m mkuu
Hongera sana,maana umekuwa muwazi hadi kwenye Mtaji.
Maana wale wazembe pesa hiyo wangekimbilia kununua Gari wauze nyago,wakiona Daladala hazina issue.
Hongera sana kamanda.Nikijenga Goba nitakutafuta ili tuungane mkono.
Ila hakikisha Bidhaa zako ni Genuine,la sivyo hali inaweza kuwa mbaya saana
 
Nashukuru sana mkuu kwa kunipa moyo, suala ubora nalifuatilia sana mkuu nko makini

Nikupe mawili ya tahadhali katika biashara ya hard ware,

Moja ogopa sana au usithubutu kununua mali za magendo, kaka zinafaida ya haraka na kubwa, ila unaweza kufa, jitahidi kulipa kodi vizuri, japo utaumia sana mwanzoni,ndio kujenga jina mkuu. Maua ya dunia yatakufuata sana, mwisho utaishia kutumia mashudu, jamaa zangu kibao pale Buguruni, wanaishi kwa buster.

Na mwisho, jitahidi sana kuyakwepa mafeki, japo mafeki yanaingiza hela haraka, ila ushindani ni mkubwa, kujenga jina utakaa kidogo.
 
Hapa Sijakupata

1.utaumia sana mwanzoni

2.maua ya dunia yatakufuata sana

3.utaishia kutumia mashudu

4.wanaishi kwa buster

Ahsante
 
Hapa Sijakupata

1.utaumia sana mwanzoni

2.maua ya dunia yatakufuata sana

3.utaishia kutumia mashudu

4.wanaishi kwa buster

Ahsante

1. Mwanzoni utaumia sana, sababu utakuwa unabambikiwa bei unaponunua mzigo wa jumla, si mgeni, mpaka uvijue vijiwe vya bei nzuri, ndio utaanza kupata faida.
2. Maua ya dunia mkuu ni totoz, wakishajua una duka la hardware,ujue wako mgongoni.
3. Mashudu ni ARV
4. Busta, ni madawa kwa ujumla ya kuongeza siku za kuishi.
 
Hapa Sijakupata

1.utaumia sana mwanzoni

2.maua ya dunia yatakufuata sana

3.utaishia kutumia mashudu

4.wanaishi kwa buster

Ahsante

Jiongeze mkuu

1.Mwanzo wa biashara halali kodi huwa ni mzigo mzito kwa sababu inakuwa haijaanza kuingiza faida kubwa

2.Mademu watakufuata sana si unajua mademu wakihisi sehemu kuna slope a.k.a gradient?

3 na 4 madhara ya mambo yetu yaleee.....ARV zitahusika,kuwa makini.

Kwa nyongeza tumsubiri mkuu Malila
 
Last edited by a moderator:

Ahahaha mkuu nimekusoma.kiswahili kinakua kila uchao duuuh...
 
Last edited by a moderator:
Jiongeze mkuu

1.Mwanzo wa biashara halali kodi huwa ni mzigo mzito kwa sababu inakuwa haijaanza kuingiza faida kubwa

2.Mademu watakufuata sana si unajua mademu wakihisi sehemu kuna slope a.k.a gradient?

3 na 4 madhara ya mambo yetu yaleee.....ARV zitahusika,kuwa makini.

Kwa nyongeza tumsubiri mkuu Malila

Nimekuja mkuu,

Hapa ndio vijana wenzangu wanapopotea njia, afya ya mwili na akili ni mhimu sana. wakati mwingine mademu tunawaita wenyewe. Ningependa kuona kijana anapanda taratibu mpaka kufikia mafanikio akiwa na afya njema, ana amani tele ktk maisha yake na familia kwa ujumla. PR yake iko vizuri ktk jamii. Piga mzigo vizuri,pia pata muda wa kupumzika ili hata majirani zako upate nao muda wa kucheka na kucheza nao pool.

Lingine ni hili, jifunze na ujitahidi kujua jinsi ya kufikia kuwa wakala wa bidhaa zako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom