Mrejesho: Kuagiza rice combine harvester toka China

Mkuu vipi return yake
 
Mkuu hongera sana. Umenifungua macho sana na kunipa mawazo mapya.
 

Hongera sana mkuu hakika Mungu atakusimamia na utafika mbali sana, hapo juu mashamba unayozungumzia ni yale ya Kapunga kule au Mbalali mkuu??
 
Mi labda nikuulize
1) Hela $12,000 ulilipa direct to supplier au ulilipa kwa Alibaba wao wakampa Supplier?

2) Kuna zile zenye mkonga wa kumwaga ambazo hakai mtu kukinga bali zikifikia gunia 6-7 inapiga alar unaenda kumwaga, zipi poa kati ya hiyo yako na zile kiutendaji?? Nini kilikupendeza kununua hiyo brand?

3) Brands zinazotamba/zilizojaa sasa hapa Bongo ni KUBOTA, means hata spares zake ziko available, je hiyo yako umefikiriaje swala la spares?? Hao Supplier wana any "after-sales services" kwa Tanzania??

4) Clearing Agent umempa jumla ya Tshs 3.5Mil, je amekupa mchanganuo wa Port/TPA Charges, Kodi (if any), Agency Fees, ni kiasi gani each? Tufanye Trekta halina kodi, ila ni kodi zote kabisa halina? Import Duty, Excise Duty, Excise Duty due to Age, VAT zote hazipo?

5) Kule kwetu ruvu tunavuna kwa Tshs 120,000 - Tshs 130,000 kwa heka, je huko Mbeya unavuna kwa Bei gani??

6) Inajulikana msimu wa Kilimo cha Mpunga ni June to Septeber (Kwa Ruvu), natumai hata Mbeya itakua ni miezi hiyohiyo minne ila sio lazima iwe June - September. Je iezi minane inayobaki sio hasara kuliacha liekaa tu?? Kwaba ungenunua tabo wa aina ingine (Labda trekta) lingekua linavuna, linabeba mazao na vitu vingine??
 
Safi sana mkuu. Maswali yenye tija. Na mimi nasubiri majibu mkuu.
 
Hii ni thread bora kabisa ya mwaka 2016 ambayo nimewahi kusoma very interested. Halafu mods muwe mnaweka nyuzi kama hizi upande wake na ziwe za pekee kabisa tuwe tunaziona mara kwa mara na mziandike kama " THREAD BORA ZA MWAKA"
 
Hii ni thread bora kabisa ya mwaka 2016 ambayo nimewahi kusoma very interested. Halafu mods muwe mnaweka nyuzi kama hizi upande wake na ziwe za pekee kabisa tuwe tunaziona mara kwa mara na mziandike kama " THREAD BORA ZA MWAKA"
Mkuu tatizo muhusika hajibu maswali l.
 
Hongera kaka tutakuwa pamoja mwakani tukijaliwa uzima
 
mi nilikuwa msomaji tu wa hili jukwaa kama mwaka mzima kwa kweli limenibadilisha sana na sasa nimekuwa mfugaji wa kuku wakati mwingine hadi najishitukia

mkuu hongera kutokuwa mchoyo wa maelezo
 
Mpunga una hela asikuambie! Soko lake lipo nje nje
 
mtoa mada hongera, nimevutiwa na Uzi wako na namna unavyoonesha ushirikiano katika kujibu maswali ya wadau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…