Mi labda nikuulize
1) Hela $12,000 ulilipa direct to supplier au ulilipa kwa Alibaba wao wakampa Supplier?
2) Kuna zile zenye mkonga wa kumwaga ambazo hakai mtu kukinga bali zikifikia gunia 6-7 inapiga alar unaenda kumwaga, zipi poa kati ya hiyo yako na zile kiutendaji?? Nini kilikupendeza kununua hiyo brand?
3) Brands zinazotamba/zilizojaa sasa hapa Bongo ni KUBOTA, means hata spares zake ziko available, je hiyo yako umefikiriaje swala la spares?? Hao Supplier wana any "after-sales services" kwa Tanzania??
4) Clearing Agent umempa jumla ya Tshs 3.5Mil, je amekupa mchanganuo wa Port/TPA Charges, Kodi (if any), Agency Fees, ni kiasi gani each? Tufanye Trekta halina kodi, ila ?
5) Kule kwetu ruvu tunavuna kwa Tshs 120,000 - Tshs 130,000 kwa heka, je huko Mbeya unavuna kwa Bei gani??
6) Inajulikana msimu wa Kilimo cha Mpunga ni June to Septeber (Kwa Ruvu), natumai hata Mbeya itakua ni miezi hiyohiyo minne ila sio lazima iwe June - September. Je iezi minane inayobaki sio hasara kuliacha liekaa tu?? Kwaba ungenunua tabo wa aina ingine (Labda trekta) lingekua linavuna, linabeba mazao na vitu vingine??