Mrejesho kuhusiana na taarifa kuhusiana na Kituo cha Afya Kigamboni: Hatua zimechukuliwa, asanteni JamiiForums

Mrejesho kuhusiana na taarifa kuhusiana na Kituo cha Afya Kigamboni: Hatua zimechukuliwa, asanteni JamiiForums

A

Anonymous

Guest
Hello wanajukwaa,

Nichukue nafasi hii kumshukuru Mungu kwa afya na uzima anaotupa kila siku, pia niwashukuru jamiiforums kwa kuwa karibu na wananchi kwa kupeleka kero zetu mahali husika na utatuzi kutolewa kwa wakati(Asante Team JF). Mwezi wa tatu ilipostiwa kero kuhusu kituo Cha afya Kigamboni kutoka kwa mtumishi/watumishi akielezea changamoto wanazopitia kituoni hapo.

Rejea: KERO - Waziri wa Afya na TAMISEMI, chunguzeni utendaji kazi wa Kituo cha Afya Kigamboni, Watumishi tunapitia mazito

Taarifa iliwafikia wahusika na badhi ya mambo yalifanyiwa kazi.

Taarifa za ndani ZINASEMA:
1) Hela za on-call zilitolewa na za mwisho ni za mwezi wa pili. Bado za mwezi wa tatu mpaka sita.
2) Hela za overtime zilitolewa pia.Bado kuanzia mwezi wa kwanza Hadi wa sita.

3) Upande wa viongozi kujilipa on-call na stahiki wasizohusika, hili bado halijafanyiwa kazi. ukiachilia mbali kubadilishwa kwa mganga mfawidhi na kuwekwa mwingine hakuna mabadiliko ya matron wala katibu ambao nao ni wahusika wa ubadhirifu pia.

4) Wageni kutoka Tamisemi walifika mwezi wa Tano(takribani mwezi mmoja na nusu baada ya taarifa ya JamiiForums kutoka). Ugeni huu ulikaa na baadhi ya watumishi na Kuna taarifa walizokuwa wanauliza ikiwa ni pamoja na masaa ya kazi, ulipwaji wa stahiki n.k. Hawa watumishi baadhi walikuwa wameshapangwa Nini Cha kujibu na viongozi waliokuwepo na ndio maana hata ripoti walioondoka nao mpaka Leo majibu hayajarudishwa mpaka wa Leo.

Mtazamo wangu katika hili ni huu, Lengo la kuleta taarifa huku kwanza ilikuwa ni kuujulisha umma juu ya dhuluma wanazopitia watumishi wa afya, kuwepo na Accountability kwenye hayo yaliyotokea. Kubadilishwa Mganga mfawidhi sio accountability, kinachotakiwa ni watuhumiwa warudishe fedha walizohujumu na walionyimwa/kupunjwa stahiki zao kupewa stahiki Kama ilivyo ada.

Tamisemi kuchukua uharaka kwenye kufuatilia kero hizi na sio kuchukua zaidi ya mwezi(hili linawapa wabadhirifu muda wa kurekebisha madodoso yao hivyo kukosa ushahidi wa kutosha, pia ugeni ilibidi uitishe kikao na watumishi wote na sio kisiri Kama walivyofanya(Kuna watumishi mpaka Leo ukiwaambia Tamisemi walikuja watakukatalia). Hii kamati iliyokuja Kituoni ripoti yenu iko wapi?? Mnyonge mnyonge Haki yake mpeni. Ingelikuwa ni Mtumishi wa kawaida kahisiwa Kutenda kosa, hatua zingechukuliwa kwa haraka Sana( Hata wiki ni nyingi) Ila linapokuja swala la mtumishi kumripotia kiongozi, hatua huwa hazichukuliwi au kuchukuliwa kwa kuchelewa.

Kumbukeni, Hawa watumishi wa afya wanahudumia watu wengi Sana na ikitokea haya malalamiko yao hayafanyiwi kazi, utendaji kazi wao utapungua, kutengeneza mianya ya rushwa, utoaji mbovu wa huduma hivyo kupelekea kuzorota kwa utoaji huduma na mwishoe lawama zote zitairudia serikali yetu pendwa.(Kitu ambacho siyo kweli hata kidogo).

Hawa viongozi wabadhirifu mnaowafuga mwisho wa siku watapandishwa vyeo na watakuwa kwenye nafasi kubwa za maamuzi(kwa vile Jasiri haachi asili,Wataendelea na ubadhirifu wao, wataiba vikubwa zaidi kuliko hata hicho wanachoiba. Hapa tunakuza tatizo badala ya kutatua tatizo)

5)Fedha za kufundisha wanafunzi bado hazijalipwa mpaka Sasa.

6) Whistleblowers ni watu wanaopenda kuona mabadiliko chanya na inatakiwa washukuriwe badala ya kuwasakama na kuona Kama ni maadui. (mkuki kwa nguruwe ni mtamu Ila kwa binadamu ni mchungu).

Kuna kikao kilifanyika wilayani, moja kati ya ajenda yao ilikuwa ni utunzaji Siri wa taarifa za serikali. Je, manyanyaso hayo yanayofanyika ni Siri ya serikali pia? dharau wanazoonyeshwa watumishi wakidai stahiki zao ni Siri ya serikali pia?

Ni wakati Sasa wa Tamisemi kujifunza kupitia wizara Ya Afya (Vilio vya watumishi walioko chini ya Tamisemi ni vingi kuliko walioko chini ya wizara ya Afya. Jifunzeni kwa wenzenu wanafanyaje kukabiliana na changamoto zao, STATISTICS HAPA JAMIIFORUMS ZINASEMA HIVYO)

Mwisho
Ombi letu ni kuwa Mrudi tena Kigamboni fanyeni kikao na watumishi wote na mtajua mengine mengi ambayo hayakuandikwa hapa jukwaani. (Ikiwa ni pamoja na usimamizi mbovu wa duka la dawa la jamii(CDO),nUtoaji huduma bila kutoa risiti kwa baadhi ya wateja ikiwemo wodi ya wazazi.)

HAKI NA ITAMALAKI
 
Back
Top Bottom