Mrejesho kuhusu Suzuki Jimny 2000

Mrejesho kuhusu Suzuki Jimny 2000

Hiki kigari shida hakipo stable hasa offroad kepesi mno sijui walikakosea chassis yake vipi.
Ila mkuu ungechukua ya 1.3L/1.4L manual isio na turbo ndo vina nguvu sana kote kambi!

Yote kwa yote hongera mkuu
Thanks man tatizo budget yangu Ilikuwa milioni 9 na sasa hivi naona vinazidi kupanda bei mkuu .unajua kipya ni 70 milioni?
 
Kweli mkuu.kuna siku mama mmoja aliniomba nimsogezee gari yake ya manual nikamwambia samahani sijui kuendesha manual gear niliona aibu sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji853]
Hahahah maza alikuona mama mwenzie tu sema alikausha 😅 ulipoona stick shifter tu ukajiwahi fasta!
 
Mbona Serikalini wanaagiza Manual mkuu ,hizi hard top zote ni manual gear.na hizi za kwenda porini ni manual gear ..Hivi hizi Kilimo kwanza ni Manual au AT maana sijawahi hata kuchungulia huko ndani kukoje .
Nazo ni Manual mzee! Serikali haiagizi Automatics! Ukiona li Auto-matic jua ni specs za Mkurugenzi alizotaka wakati anaagiza la kwake
 
Vijana punguzeni kula chips mayai, yaani kuendesha manual Dar - Arusha unalia lia? Sasa ukipiga Dar - Kigoma? Manual raha sanaaaaa na huwezi sinzia hovyo...
Hahahahah utamu wa manual ni pale umetanua halafu unataka upangue urudi site yako 😅 maana Scania XT inataka kuja kukufanya chapati 😅😅😅
 
Inatesa kivip wakati safari ndefu haubadili gia mara kwa mara. Sema hiko kigari kina cc ndogo Ndio maana kimemchosha jamaa
Hicho kigari sio comfortable mkuu! Utachoka tu hata ukienda nacho Dar-Moro tu sababu ni low budget car!

Nunua Prado iwe manual with Air Suspension uone kama ukiliendesha hata Dar-Tunduma kama utajihisi kuchoka!
 
Thanks man tatizo budget yangu Ilikuwa milioni 9 na sasa hivi naona vinazidi kupanda bei mkuu .unajua kipya ni 70 milioni?
Sema naona ulidhamiria yakuagiza ila kwa hio bajeti yako ungepata escudo safi kabisa yenye power kubwa au hata escudo ile second gen.hizo ndo gari ndogo zenye 4wd ya uhakika,very economical,power,zina space zaidi kuzidi jimny!
Mil 70 kununua jimny ni kuchezea pesa!
 
Hiki kigari shida hakipo stable hasa offroad kepesi mno sijui walikakosea chassis yake vipi.
Ila mkuu ungechukua ya 1.3L/1.4L manual isio na turbo ndo vina nguvu sana kote kambi!
Ninayo hii, ya mwaka 2013. Kambi popote nimetia tairi AT basi nakatizabkila sehemu.
 
Siku ukitaka kusukuma unijuze.
Hizi gari huwa naziota Kila wakati
Hizo hapo mkuu .
Screenshot_2021-10-20-19-09-24-067_com.ding.kupatana.jpg
 
Teknolojia Ya Manyo Kwenye Gari ni sawa na analogia kwenye Mawasiliano. Baada Ya Miaka Kadhaa Viwanda Vitaacha Kuzalisha.
Hiyo haiwezi tokea ji sawa na kusema simu za battan zisiwepo tena sokoni
 
Back
Top Bottom