Mtoa mada unachekesha walionuna, Hicho kituo cha afya ulichoenda wakakubali majibu yako ya HIV wampe mtu wa pili ni kituo gani, je kuna fomu ulizojaza kuwaruhusu watoe siri za mgonjwa kwa mtu wa pili, hata kama ni mkeo mtoa huduma alithibitishaje kama ni mkeo.
Na hata kama alithibitisha kama ni mkeo, je majibu ingekuwa umeathirika je mkeo angeyapokeaje ilihali hajapewa uthauri nasaha.
Umemkuta mkeo anacheka na majirani, kipi kilichokuthibitishia ya kuwa alipewa majibu yako. Tufanye alipewa majibu yako je kama naye alikuwa muathirika siku nyingi kwa hiyo anafurahia wote ngoma sawa.
Ushauri wangu kama ni kweli unataka kubadilika na kuacha umalaya, kwanya tubu mbele ye mkeo kuwa hukuwa muaminifu na umekuwa na mahusiano mengine nje zaidi ya wanaweka 40, halafu muombe muende wote mukahakikishe afya zenu