Nashukuru wote mlionipa ushauri nilipoleta tatizo langu la kujamba sana kila siku.
Alfajiri leo nimeenda kumuona doctor nimefanyiwa vipimo vyote vya tumbo sina tatizo lolote pia jana usiku nilikula papai na tango bila kula kitu kingine nimeamka vizuri nimejamba kama vijambo viwili tu vya kawaida.
Mungu alie mwema awabariki sana maana kachanga kangu leo kamelala vizuri bila hofu ya kushtuliwa na sauti zozote.
Wanasayansi wanasema kutoa ushuzi ni afya
Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni.
Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni
Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti watu wanauchukulia utafiti huu kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile Saratani.
Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
"ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani, ''asema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha Exeter.
Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.
Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa
Chanzo: bbc
Mkuu usiache kujamba, kujamba kuna faida tele tu.