Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

upon arrival of your parcel kwenye post yako utamkuta mtu wa TRA
niwie radhi kama nakusumbua, kama niko sengerema inamaana mzigo wangu utatumwa sengerema na kodi nitafanyiwa assessment nikiwa sengerema?
 
Mkuu ya kwangu nimeweka wamenambia this card is not accepted use another card sijui kwa nini labda kesho niwasiliane na watu wa bank
Hatua ya kwanza: Fika benki waeleze kadi yako unataka itumika kufanya miamala mtandaoni, Utapewa fomu utajaza, Then utajulishwa kuwa iko tayari baada ya kusubiri kwa muda utakao elezwa.

Hatua ya pili: Ingia paypal na link kadi yako - Watakata salio kidogo.

Hatua ya tatu: Rudi benki tena - Omba account statement, na utaona akato ya paypal sambamba na code kwa ajiri ya kufanyia verification cardi yako.

Hatua ya nne: Rudi paypal na ingiza code ulizopata kwenye account statement.

Benki zingine card zao hazina huomzunguko wote, Unachukua kadi ikiwa iko tayari kwamatumizi mtandaoni.
 
niwie radhi kama nakusumbua, kama niko sengerema inamaana mzigo wangu utatumwa sengerema na kodi nitafanyiwa assessment nikiwa sengerema?
Nina hakika Mwanza Posta kuna wa TRA staff, wilayani sina hakika, Nakushauri tumia posta ya Mwanza. Mzigo ukifika wanakupigia simu uje kuchukua, Tumia poscode ya Mwanza
 
Tatizo kubwa la Ebay, Exchange rate wanayotumia ni kubwa sana. Usifanye kosa kufanya conversion kwa kutumia BOT rates unless you maintain USD account
 
Nina hakika Mwanza Posta kuna wa TRA staff, wilayani sina hakika, Nakushauri tumia posta ya Mwanza. Mzigo ukifika wanakupigia simu uje kuchukua, Tumia poscode ya Mwanza
thank you
 
Nashkuru mkuu

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
FAIDA ZA KUFANYA MANUNUZI EBAY
1. USALAMA WA TAARIFA ZAKO ZA KIBENKI
Kwenye manunuzi ya mtandaoni kuna wanaotumia ebay, alibaba, aliexpress, amazon etc. Lakini kwa wataalamu wa mambo wanaashauri kwamba iwapo unahitaji usalama wa taarifa zako za kibenki. Usalama wa taarifa zako za kibenki ni muhimu sana ili kuepusha kuibiwa fedha zako mara baada ya kufanya manunuzi online.
Ebay wana utaratibu wa kumlinda mteja wao na kumuhakikishia usalama wa taarifa zake za kibenki mara baada ya kufanya manunuzi. Mara nyingi wanashauri wateja wao wafanye manunuzi kwa kutumia paypal...na kuwazuia wanunuaji kufanya mawasiliano na wauzaji nje ya mfumo rasmi wa ebay.
2. UHAKIKA NA UFIKAJI WA HARAKA WA MIZIGO
Ebay wana utaratibu wa kuwabana wauzaji na kuhakikisha hawafanyi udanganyifu wowote wakati wa mauzo.Muuzaji hulipwa fedha zake baada ya siku ishirini toka alipofanya mauzo na iwapo hakutatokea malalamishi yeyote.. kawaida muuzaji hulipwa fedha zake mara baada ya kutoa vielelezo vyote kwamba mzigo umetumwa au umemfikia mnnuaji. Ili kuhakikisha hili wanawapa wateja wao uhuru wa kufanya madai iwapo watahisi hawajatendewa haki.. Malamiko hayo hupewa uzito mkubwa sana na ebay. Nilinunua bidhaa kwa muuzaji baada ya malipo muuzaji akanambia stock imeisha.. Nikamuuliza kuhusu altenative akawa haeleweki nikamripoti ebay na hivi ndivyo ilivyokuwa..

Mtandao mwingine wenye uhakika kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ni amazon.
Wakina aliexpress, alibaba n.k wanafanya mauzo ma pengine bidhaa zao ni cheap but kuna tatizo kubwa sana la ubove wa customer care, mizigo kuchelewa na wizi wa fedha kwenye acount za watu coz unawalipa wauzaji direct kupitia kadi yako.. Hii hapa chini ni mifano ya malalamiko yabwateja wa aliexpress...

View attachment 495423 View attachment 495424
View attachment 495432
 
Juzi nilienda crdb kwaajili ya kadi yangu kuanganishwa na online purchase. Sasa leo wamenitumia message wananiambia. Please register for VBV/Secure Code, wamenipa access code ili nitumie kwenye website yao, so wakuu hapo mm sijawaelewa wanataka nn naomba msaada kwenye tuta.
 
Ngoja wajuvi waje..
 
Naiona hii kuwa option nzuri
 

Wengine hupenda kutumia pia 25522 kama msimbo wa posta wao. Mimi pia nilikuwa nautumia huohuo. Tatizo ni kwamba barua ikija posta inapelekwa kwenye P.o. Box 255 au 25522. Najuaje? Nilishawahi kuitwa na mwenye sanduku moja ya hayo kuniletea kipaseli changu. Toka siku hiyo naweka anuani yangu ya posta kama post code. Na hata kama nafahamu msimbo wa posta wa ukweli (angalia Postcode List) lakini siutumii bado.

Kuhusu kununua mitandaoni, ni njia ya uhakika. Matatizo machache (bidhaa feki, jina la orijino, hasa vifaa vya elektroniki, kutoka nchi fulani ya Mashariki ya Mbali).

Uchumi wa Marekani ulishahama kutoka kwenye viwanda kwenda kwenye huduma. Matokeo yake huduma zitolewazo ni bora sana kwa vile ushindani ni mkali. Jitahidi kukwepa kutumia credit card yako kufanyia miamala pale inapowezekana tumia Paypal au huduma zifananazo nayo.
 
Vipi gauni ni 2.5$ na shipping cost 6.23$. Je hii inamaana kuwa gauni hadi lifike Tz gharama Itakuwa ni 8.73$ ? Pia na TRA Je? Gharama si kubwa. Em nisaidie nijue cz nataka nifanye biashara, nimechoka kutegemea mshahara.
Cheki vizur waweza pata ambayo yana fre shipping cost.. Na mengine usipokuwa makini unaweza ukajikuta umejicommit kubuy bidhaa yenye shipping cost ata 90usd wakati kitu hcho kinauza dola 1."so kuwa makini kuangalia gharama
 
Cheki vizur waweza pata ambayo yana fre shipping cost.. Na mengine usipokuwa makini unaweza ukajikuta umejicommit kubuy bidhaa yenye shipping cost ata 90usd wakati kitu hcho kinauza dola 1."so kuwa makini kuangalia gharama
Poa asante
 
Fursa nzuri uoga ndo umaskini ngoja tujitose kwani sh ngapi
 
Nataka kununua dsrl camera, amazon au ebay taratibu zinakuaje kwa hapa Tanzania kwa maana ya ushuru n.k
 
Paypal inakuwaje mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…