Wengine hupenda kutumia pia 25522 kama msimbo wa posta wao. Mimi pia nilikuwa nautumia huohuo. Tatizo ni kwamba barua ikija posta inapelekwa kwenye P.o. Box 255 au 25522. Najuaje? Nilishawahi kuitwa na mwenye sanduku moja ya hayo kuniletea kipaseli changu. Toka siku hiyo naweka anuani yangu ya posta kama
post code. Na hata kama nafahamu msimbo wa posta wa ukweli (angalia
Postcode List) lakini siutumii bado.
Kuhusu kununua mitandaoni, ni njia ya uhakika. Matatizo machache (bidhaa feki, jina la orijino, hasa vifaa vya elektroniki, kutoka nchi fulani ya Mashariki ya Mbali).
Uchumi wa Marekani ulishahama kutoka kwenye viwanda kwenda kwenye huduma. Matokeo yake huduma zitolewazo ni bora sana kwa vile ushindani ni mkali. Jitahidi kukwepa kutumia
credit card yako kufanyia miamala pale inapowezekana tumia Paypal au huduma zifananazo nayo.