Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

kwaio account ninayotakiwa kufungua n ya paypall tuu? . Na ebay ni kwaajili ya kuagizia bidhaa tuu kwa kutumia web page yao? haihitaj ufungue account?
 
yaan kwa ufupi naomba connection between ebay au nikisema seller sijakosea na hawa paypall
 
Tatizo ndugu yangu uaminifu wa watu wa hapa POSTA za kwetu, kwanza kumbuka mzigo ukifika pale lazima waufungue wajue kama umetumiwa bomu au nini... Sasa picha linaanza watakapokuta digital camera nzuriii au iphone 7 iko pale hiivii... uwo mzigo utapotea

Mimi nilishawai kununua Vifaa Vya Electronics mf. MicroCPU, Capacitors, Sensors jamaa wa Kjitonyama pale wakanipigia simu nikachukue

Sasa agizi digital camera au iphone7 huone kama utapigiwa simu.

Mkuu wewe uliagizia nini ukapata? Labda unaweza ukaongeza imani yao
 
Kuna restriction kali sana wanapewa wauzaji wa bidhaa ikiwemo evidence na deliverance ya bidhaa kwa mnunuaji..
PayPal Security Center - PayPal Safety - PayPal
 
Mkuu kama kutapeliwa popote unatapeliwa acha mambo ya ajabu.

Mbona hapa hapa mjini watu bado wanatapeliwa.
bora umemchana! ana distort uzi sana!

Mkuu Mr. MTUI nakuelewa sana, ila nilipofikia kufungua akaunti ya PAYPAL kuna sehemu ya kujaza imeandikwa CSC/CVC, naweka kitu gani hapo!
 
bora umemchana! ana distort uzi sana!

Mkuu Mr. MTUI nakuelewa sana, ila nilipofikia kufungua akaunti ya PAYPAL kuna sehemu ya kujaza imeandikwa CSC/CVC, naweka kitu gani hapo!
Hizo ni nambs za mastercard au VISA card ..zinapatikana nyuma ya kadi (CSC-CREDITCARD SECURITY CODE, CARD VERIFICATION CODE-CVC, CARD CODE VERIFICATION-CCV) ni maneno tofauti lakini yanamaana sawa.. ni additional info zinazowezesha katika utambuzi wa kadi hako na zinahakikisha kwamba manunuzi yanayofanyika yamefanywa na muhusika wa kadi.. Ata kama mtu atakuibia au ataguess number ya kadi siyo rahisi kuguess hadi CSV yako.. Hasa kwa wale wazee wa kuguess number...
 
La Protection des Achats - PayPal France
Ni jukumu la muuzaji kutumia reputable courier na dropper ili mzigo ukufikie otherwise usipoupata mzigo case inarudi kwao
 
nimefanikiwa kufungua akaunti EBAY na PAYPAL, nitaendelea kuleta mrejesho!
 
Yah... Wengine hawataki kabisa mambo ya p. O. Box.. Andika nchi na mkoa na wilaya.. Na ile zip ckde +255 mzigo unafika.
+255 sio Zip code. Mr Mtui Ukiandika p.o.box haina tatizo. Kitu muhimu weka mobile number na mji. Watu wa Posta wana orodha ya miji Tanzania nzima.
 
UNAFIKA WAPI NA UTAJUAJE AU NITATAKIWA KUANDIKA NAMBA YA SIMU BADALA YA PO BOX ?
Mfano: Unaitwa Mkaruka Mabhai.
0612444444 .Unakaa Dodoma. Huo mzigo utafikaje hapo Dom bila kuandika Town Location? Pobox sio lazima saaana muhimu weka town location eg: Iringa, mafinga,Dodoma,Mwanza,Musoma nk
 
Kama vinakufikia haina shida.. Kuna seller wengine hawataki kabisa kusikia mambo ya P. O. Box so hiyo code ndo unaweza tumia
Wanaogopa customs declaration. Ukiweka p.o box watu Wa customs wanakagua. Unajua customs wana ofc post office.
 
Ukiwa na anuani ya Posta sio vibaya ukiandika. Ni vyema sana ukiandika namba ya simu jamaa Wa Post office watapiga au kutuma SMS.
Namba yako ya simu utaiandika wakati wa kufungua acount.. Ebay watampa seller wa bidhaa yako pale mtakapoingia makubaliano ya kuuziana.. Na Itajitokeza kwenye kila manunuzi utakayofanya... Hairuhusiwi kuandika au kutoa details zako za simu as ni rahisi kwa scammer kukuingilia na kukuibia.. Mawasiliano hote yafanyike kupitia ebay na siyo nje ya ebay coz lilkitokea la kutokea ebay hawatakulinda...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…