Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

CPU ilifika ukaitwa ukachukue K'nyama ukaenda ukapewa. Sasa mbona huamini Posta wakati mzigo ulipata?
 
+255 sio Zip code. Mr Mtui Ukiandika p.o.box haina tatizo. Kitu muhimu weka mobile number na mji. Watu wa Posta wana orodha ya miji Tanzania nzima.
Yah kwa purchase ya mwanzo.... Then after zitakua zinajitokeza.. Mfano mimi nikitaka nunua sasahv detail zangu zote zinajitokeza automatically kuanzia simu hadi address.. So sinahaja ya kujaza kila purchase labda kama nimehama location..
 
Mtui umewasaidia wajasiriamali hawa. Kazi kwao fursa hiyo kupata bidhaa bora kwa Bei nafuu. Huitaji kusafiri. Just stay and make orders. e-commerce.
 
Ndio. Mfano nipo Iringa. Naandika mobile number then Iringa. Mzigo unafika.
Andika
Jina lako kamili
Nchi
Mkoa
Wilaya
Mtaa ukipenda tho hawatakuletea mtaani
Zipcode +255
Ur mobile number if is required sikumbuki if transaction ya kwanza iliitaji number ya simu user mpya wa ebay atatuelezea Cc@Greencity
 
Mimi mwenyewe nimetoka kuagiza nguo fulani kwaajili ya bibi yangu na kwasasa zipo njiani zinakuja.. Mpaka kati ya mwezi huu nazipata..
 
Asante kwa mrejesho.Vipi zile Land cruiser V8,GX zinazouzwa kwa.mnada buwa ni za kweli au utapeli.Zile hazipiti posta
 
Wauzaji wenyewe hawajui kiingereza cha msingi ni kujua hitaji lako coz uzuri wa hii system inatumia zaidi picha na fedha.. So kutokujua english isiwe kikwazo kwako..
Uliposema unapigiwa simu kutoka uko mbele ndo nimechanganyikiwa, kizungu cha kusoma na kuandika najitahidi ila kuflow fluently hapana
 
Address yako uliandikaje share hapa ili watu wapate vionjo tofauti.. Mimi niliitwa posta kuu
 
Uliposema unapigiwa simu kutoka uko mbele ndo nimechanganyikiwa, kizungu cha kusoma na kuandika najitahidi ila kuflow fluently hapana
Mbele hawapigi labda kama kunaulazima.. Zaidi wanatumia emails
 
+255 sio Zip code. Mr Mtui Ukiandika p.o.box haina tatizo. Kitu muhimu weka mobile number na mji. Watu wa Posta wana orodha ya miji Tanzania nzima.
Sawa mkuu...
 
yaan kwa ufupi naomba connection between ebay au nikisema seller sijakosea na hawa paypall
Ebay ni platform ya wauzaji na wanunuzi mbalimbali wa bidhaa.. Kila muuzaji ana bei yake.. Usishangae ww ukanunua simu kwa usd 100 mimi nikainunua kwa USD 50..Paypal wanacontrol transaction ya fedha kati yako na muuzaji wa bidhaa ili kuleta usalama wakati wa manunuzi.
 
Nafikiri ni kwa usalama zaidi haiwezekani mtu ukawa na ela ndogo alaf ukanunua kitu cha gharama kubwa ndo mana ikawa inawashtua hao wazungu..
 
Walinipa inaonyesha kimefika ila nikienda Posta hamna kitu;
Yaani sijawapenda kabisa Amazon
Fungua case.. Au amazoni hawana hizo mambo.. Ebay ikitokea hvyo unafungua case wanarefund
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…