Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

Kama umepoteza kadi ya benki ya master au visa mtu anaweza tumia hio card kufanya manunuz mtandaoni
- Ndio inawezekana iwapo tu kadi yako ilikuwa tayari imewezeshwa kufanya manunuzi mtandaoni.
- Maana waweza kuwa na master au visa card ambayo haijawezeshwa kufanya miamala mtandaoni,
- By default kadi zitolewazo na benki hapa TZ hazijawezeshwa, Hadi mmilikiwa kadi aombe hiyo huduma kwa kujaza fomu maalum.
 
Paypal akaunti yake inafunguliwaje na inatumikaje kufanya transactions manake naona watu wengi wanadai kufanya manunuzi via paypal
 
Mimi natumia UBA na ninaona wapo vizuri...tembelea tawi lao lolote watakupa maelekezo
 
Mkuu hapo kwenye zipcode nnatuima +255!!? Maana nlienda posta kuulza wakanambia nitumie postal code ya mkoa...ambayo kwa nilipo sasa hv (Dodoma) ni 41000 sasa hapo inakuwaje..maana sina experience na hzi online shopping!
 
Mkuu hapo kwenye zipcode nnatuima +255!!? Maana nlienda posta kuulza wakanambia nitumie postal code ya mkoa...ambayo kwa nilipo sasa hv (Dodoma) ni 41000
Zipcode / postal code - Ni kitu kimoja
- Kama upo dodoma ni hiyo 41000
- Kwa dsm ni 11000
Na hii 00255 ni country code, TZ, hivyo katika ujazaji wa fomu online hutumika kimazoea na tena kimakosa. Fuata maelekezo uliyopewa posta. Hivyo tusifanye mazoea ya kimakosa kuwa ndio usahihi wa jambo.

a] Kwa kuangalia zipcode / postal code kwa kila mkoa tumia hii link: Postcode List

b] Ili kufahamu zipcode / postal code hadi kwa ngazi za wilaya / kijiji basi download hii pdf

Note
QUESTION:

What's the difference between Zip Code and Postal Code

ANSWER:

The two codes are essentially the same in their purpose, but the term Zip code is mainly used in the USA; Postal Code is commonly used in other countries.
Hivyo popote ukiona haya maneno: postal code/ postcode/ ZIP Code - Yote yanamaanisha kitu kimoja

KARIBU
 

Attachments

kwa bidhaa ambazo ni free shipping kwa ebay zinachukua siku ngapi mtoa post
Mimi nimezoea aliexpress sana mkuu ila huku ebay.naona ni ngumu sana kununua bcoz mpaka ujaze address za marekani hata kama mzigo unatumwa duniani kote
halafu changamoto nyingine nayoiona ni mfumo wa app yao kule aliexpress tumezoea kuona kwenye nchi pale kwenye setting unajaza tanzania kwahiyo bidhaa zote na gharama ya kutuma tanzania unaona huku ebay nitofauti
kweli aliexpress kwangu kwa huku africa ni nzuri na rahisi kuielewa kuliko ebay

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna njia nyingine ya kufanya manunuzi kwa kutuma pesa zikawa converted to us dollars?
 
Ununuzi wa magari unautaratbu wa tofauti.. But ukinunua unapata
hapa kwenye magari ndo wawe makini zaidi maana kuna issue ya TRA na maswala ya clearance ambayo lazima uyajue na lazima ulipie
 
Wadau kwema? Kwa dhati nishukuru thread hii kwani niliweeza kuagiza simu aina ya Motorola moto x play na kunifikia salama kabisa...ila shida ni namna ya kuswitch 4g LTE inagoma licha ya kuwa na uwezo huo wa 4g ..msaada tafadhali
Ilichukua mda gani kuipata tangu uiagize
 
Maelezo mazuri mkuu, ila kawaida zip code kwa watu wanaokaa nje ya US, huwa ni 00000 (yaani zero tano). Hiyo +255 sio zip code, bali ni telephone code ya Tanzania.

Ukatumwa tarehe 16 na leo umefika..

NILICHOJIFUNZA

1. Wakati mwingine woga wetu ndio unaotufanya kuwa nyuma kimaendeleo.. Dunia ya sasa imekua kijiji unaweza pata bidhaa yeyote toka ulimwengu wowotena kwa bei rahisi cha msingi ni kutumia njia sahihi wakati wa manunuzi..

2. Wizi wa pesa kwenye acount.. Kuna wakati nilikua na wasi wasi kwamba uenda jamaa wangenipiga ela zangu kwenye acount.. Hii si kweli jamaa wa ebay wapo makini sana hasa hasa ukiwa na acount ya paypal yani chagua bidhaa ebay lakini lipa kwa kutumia paypal..
Kuna jamaa mmoja alikweka bidhaa kiwizi wizi nikainunua jamaa wa paypal walipogundua wakamblock jamaa na fedha zangu zikarudishwa kwenye acount yangu.. Haijalishi ni kiasi gani kitarudishwa..

View attachment 489334
KUHUSU ZIP CODE NA POSTAL CODE

Hizi zisiwasumbue.. Andika detail zako za nchi, mkoa na wilaya, na code yetu pendwa ya +255 plus jina lako kamili trust me mzigo wako utafikishwa posta kuu ya mkoa wako na watu wa posta watakupigia simu uufate mzigo wako mara unapofika.. Hasa wakituma kwa register..

Usiandike P. O. BOX kwani wengine huwa hawataki mtu atumie P. O. Box.

2. Kuna vingine vingi ambavyo ukiwa interested unaweza jifunza cha msingi tuache woga.
 
Hivi huwa kuna mizigo inatumwa pasina kuwa na tracking number?
Screenshot_2019-01-24-08-00-59.png
 
Inashauriwa kabla ya kunua bidhaa ebay uwe umejiridhisha kuhusu huyo seller.

Na ikibidi ni vyema kwanza ukawasiliana naye ili kujua njia ya usafirishaji na maswala ya tracking number.
Hivi huwa kuna mizigo inatumwa pasina kuwa na tracking number?
- Ndio huwa inatokea, na tegemea kuupata mzigo baada ya wiki 4 hadi 7.
- Epuka FREE shipping za ebay thamani ya item kama ni ndogo basi hakuna tracking number.
- Ila pia hakikisha unasoma TOS za ebay kuhusu urudishaji wa fedha pindi mzigo haujafika ndani ya siku stahiki.

Kwa wanao anza manunuzi mtandaoni ni vyema wakatumia zaidi aliexpress na chagua standard shipping ili mzigo wako ufike mapema na ukiwa na tracking number
 
Inashauriwa kabla ya kunua bidhaa ebay uwe umejiridhisha kuhusu huyo seller.

Na ikibidi ni vyema kwanza ukawasiliana naye ili kujua njia ya usafirishaji na maswala ya tracking number.

- Ndio huwa inatokea, na tegemea kuupata mzigo baada ya wiki 4 hadi 7.
- Epuka FREE shipping za ebay thamani ya item kama ni ndogo basi hakuna tracking number.
- Ila pia hakikisha unasoma TOS za ebay kuhusu urudishaji wa fedha pindi mzigo haujafika ndani ya siku stahiki.

Kwa wanao anza manunuzi mtandaoni ni vyema wakatumia zaidi aliexpress na chagua standard shipping ili mzigo wako ufike mapema na ukiwa na tracking number
Shukrani Mkuu, nimekusoma
 
Back
Top Bottom