Mrejesho: Ndoto inayojirudia kwa Miaka 12 sasa!

Mrejesho: Ndoto inayojirudia kwa Miaka 12 sasa!

Sio kweli kabisa... Ungekuwa unadhurika kirahisi usingekuwa hai mpaka sasa! Kinachokutesa ni hofu uliyoamua kuipa nafasi katika mustakabali wako! Vita vya kiroho si mchezo ungekuwa dhaifu huna kinga ya kiroho zamani sana ungeshaondoshwa
Anyway huo ni mtazamo wangu tu na nilichokushauri utumie ni tiba yenye nguvu sana
Mkuu Mshana kuna hili la kulishwa sijui ndo madawa kwenye chakula nasaidikeje?....Maana naambiwa mpaka ntapishwe mkuu
 
Mkuu Mshana kuna hili la kulishwa sijui ndo madawa kwenye chakula nasaidikeje?....Maana naambiwa mpaka ntapishwe mkuu
Acha kuteseka ndugu.

Fanya maombi ya kufunga na kuomba nawe utapona. Mwombe Mungu akutakase kwa damu ya Yesu na akufanye uwe mpya. Utu wako wa kale utaondoshwa nawe utakuwa mpya kabisa.

Mwombe Mungu akusamehe kwa kutokumwamini yeye, na kwa kutegemea wanadamu (Maana imeandikwa amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake, lakini amebarikwa amtegemeaye na kumtumainia Mungu)

Ukimkiri Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako, na kumruhusu akutangulie na kukuongoza katika njia zako zote, NAYE ATAYANYOOSHA MAPITO YAKO YOTE.
 
Back
Top Bottom