Mrejesho: Nilifanya biashara kwa wazo la hapa JamiiForums

Mimi ni miongoni mwa watu wanaojaribu vitu vingi sana, Naamini katika so called risk taking.

Kuna mwana Jamii Forums humu alikuja na wazo, nilipoliangalia nikaona kama linawork, nikampigia simu akanipa ushirikiano nzuri sana( hakuwa tapeli kabisa nashuhudia hili hapa wazi wazi, he was a humble youth).

Biashara yenyewe ilikuwa ifanyike mkoani, sitaki kuitaja Kwa sababu mpaka sasa hata yeye hajui ID yangu hapa Jamii Forums.

Nilisafiri tukaanza biashara tulifanya vyema kama inavyotakiwa ingawa Niko busy sana nilikuwa namuachia.

Kwa ufupi niliingiza TSH 2,850,000 mpaka mwisho wa project nikipata jumla 520,000. Nilikula hasara kubwa mno.

Faida niliyopata ni shule, nikipata shule kubwa yapo mambo sitarudia kufanya, lakini yapo nitarudia kufanya ila Kwa umakini mkubwa sana.

Huyu kijana hakunitapeli ila tu basi biashara isikie hivi hivi, inalipa ikiwa inaadithiwa, ukiibgia ground unakutana na mengine kabisa ambayo hayakuwa kwenye hadithi.

Kama kuna mwingine ana wazi analodhani linaweza kutulipa vizuri karibu.
Ingia kwenye biashara ya waste inalipa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hivyo kwenye biashara kuna risks na uncertainties nyingi sana mkuu yaani usipo pata faida utapata shule.
 
Sasa hizi ndio feedback zakuweka hapa. Tunaelezana ukweli wenyewe.
Hongera kwa kuthubutu mzeya. Sie wengine ata biashara ya bodaboda tunaogopa. Hela zimekaa tuu hazina la kufanya
Aisee

Hela imekaaa tu?

Take riskw au peleka fixed account basi kama unaogopa sana.

Au nunua kiwanja, jenga nyumba kama inatosha.

Nunua government bonds
 
Kichwa cha Habari na kilichomo ndani ni takataka tu
 
Mimi ni miongoni mwa watu wanaojaribu vitu vingi sana, Naamini katika so called risk taking.

Kuna mwana Jamii Forums humu alikuja na wazo, nilipoliangalia nikaona kama linawork, nikampigia simu akanipa ushirikiano nzuri sana( hakuwa tapeli kabisa nashuhudia hili hapa wazi wazi, he was a humble youth).

Biashara yenyewe ilikuwa ifanyike mkoani, sitaki kuitaja Kwa sababu mpaka sasa hata yeye hajui ID yangu hapa Jamii Forums.

Nilisafiri tukaanza biashara tulifanya vyema kama inavyotakiwa ingawa Niko busy sana nilikuwa namuachia.

Kwa ufupi niliingiza TSH 2,850,000 mpaka mwisho wa project nikipata jumla 520,000. Nilikula hasara kubwa mno.

Faida niliyopata ni shule, nikipata shule kubwa yapo mambo sitarudia kufanya, lakini yapo nitarudia kufanya ila Kwa umakini mkubwa sana.

Huyu kijana hakunitapeli ila tu basi biashara isikie hivi hivi, inalipa ikiwa inaadithiwa, ukiibgia ground unakutana na mengine kabisa ambayo hayakuwa kwenye hadithi.

Kama kuna mwingine ana wazi analodhani linaweza kutulipa vizuri karibu.
Sasa si useme ni biashara gani na ulifeli wapi ili na wengine wajifunze
 
Aisee

Hela imekaaa tu?

Take riskw au peleka fixed account basi kama unaogopa sana.

Au nunua kiwanja, jenga nyumba kama inatosha.

Nunua government bonds
Ah hawa fixed account yaani wanakupa asilimia 6 for 50mil. Hapana wacha ikae niwe naichungulia tuu.
 
Back
Top Bottom