Mrejesho: Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba

Ni sawa mkuu ila kwa hizo busness zinaweza kukuongezea stress kuliko kupunguza, niliwahi kuwa na idea ya saloon na hiyo ya bodaboda ila baada ya kufanya utafiti nikagundua ina stress kuliko nilivyofikiri hasa kupitia kwa baadhi ya rafiki zangu waliofanya hizo biashara, biashara ya duka ndiyo nafanya sasa hivi na inanilipa sana ila inatokana na kuwa wife ndo mtu anayeshinda dukani na tunaelewana sana. Njia nyingine unayoweza kufanya kwa sasa au baadae ni kununua hisa katika mashirika yanayopata profit, unakua unapata gawio kila mwaka japo linaweza kuwa kidogo ila capital yako inakua salama. Ila ngoja tuone na michango mingine ya watu waliopractice hizo biashara hope mwisho wa siku utapata wazo zuri.
 
mechanical eng chuo gani?hapa dar nahitaji kuonana naww tafadhari
 
Anaweza Pata ilaa hesabuu ya kwa day yakumpelekea bosi wake wengiwao n elfu 7000 mpk 10000 cjui utampata wapi wa 22 kwa day hata wa mkataba hapati, ajaribu biashara nyinginee mkuu wangu
Mkuu soma vizuri thread nimesema bodaboda 2.
 
Asante mkuu nimekusoma vizuri na nimekuelewa.
 
Mkuu naomba uni pm kama huto mind...maana najaribu kuku pm afu inagoma
 
mkuu fungua duka la mahitaji ya nyumban has a ukipata sehemu yenye watu wengi kama mbagala..pili usimamizi uwe mzuri
 
Ongeza mtaji na uboreshe biashara uliyonayo sasa ya mchele...nyingine achana nazo mpaka umalize chuo
 

Yaah hata mimi nilidhani hivyo. Tayari una uzoefu katika eneo hilo, concentrate nguvu na akili zako hapo, in fact unachoweza kufanya cha ziada katika eneo/biashara hiyo, ni ku ADD VALUE kwenye mchele huo unaouza labda kwa kufanya packaging hususan kwa wateja wa hapo "Chuoni" ulipo. Lenga hata walimu wako na staff wengine kwa kufanya packaging ya kawaida tu, siyo sophisticated! Hiyo faida, weka akiba for a rainy day!
 
Kwa kuongezea tu aweke packaging ya uzito tofauti km kg 1, 2 na 5 then awe ameshauchambua kabisa. Anaweza kuvutia wateja zaid.
 
Biashara ya uhakika hapo ni kiduka cha reja reja, maana itakua rahisi Ku monitor biashara yako. Pia jitahidi uwe karibu.

Boda boda ni pasua kichwa sana, utaishia kuziuza kwa hasara, pia risk yake ni kubwa, ikiibiwa manake imepotea mazima.

Barber shop sijui kiundani, lakini nayo kama haupo mwenyewe nadhani inasumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…