Salama wakuu.
Miezi kama mitano nilikuja hapa na thread hii hapa chini.
Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi
Ingawa nimepata faida ya kutosha mpaka sasa lakini nilitaka nibadilishe au nipanue biashara yangu kidogo.Katika biashara nilizotaka nifanye ni hizi hapa chini.Nimeamua nibadili aina hii ya biashara ili niweze pia kumsomesha mdogo wangu wa amekosa mkopo.
Ningeomba mawazo yatakayotolewa yajikite katika biashara hizi tatu,nisingependa mtu atoke nje ya biashara hizi tatu.
1.Ninunue boda boda mbili niwape watu wasimamie kisha watakuwa wananiletea elfu 22 kwa siku.
2.Nifungue saluni BABER SHOP ya million 4(kwa siku hapa nipewe tu elfu 15)
3.Au nifungue kiduka cha rejaleja cha mtaani cha million nne(changamoto hapa nikumpata muuzaji muaminifu) hapa pia ntaendelea kufanya biashara yangu ya mchele.
NOTE:
Pesa niliyonayo mpaka sasa ni 4m Baada ya kupata msaada wa member mmoja wa Jf wa Million moja baada ya kutembelea na kuona biashara yangu.