Mrejesho: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo?

Mrejesho: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo?

Natikisika sana, sorry nasikitika sana kwa ushauri wangu nilio haribu siku ile, kwakweli nimeghafilika, yaani hii ndo ile mapenzi hayashauriwi.
 
Uiiiiij sasa we ndo tukushaurije tenaaa?
We leta tu mirejesho maana mr anapangua yote ulopanga
 
Habari za humu wana JF, natumai wote mko njema.

Natambua baada ya kuleta uzi wangu huu

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo


Yakafuata mahaba motomoto then kesho yake tukarudi Dar. Akaniambia nitafakari nini nataka then nitamuambia, ndio nikavurugika zaidi.
Okay wale mlotaka mrejesho there you go.
Toka ndotoni kumekucha, unachelewa Daladala za feri kwenda kuparua Samaki.
 
Habari za humu wana JF, natumai wote mko njema.

Natambua baada ya kuleta uzi wangu huu
Una haki ya kuvurugika. The guy is a humble man you are a fine girl. Kama nyinyi ni wa imani ya kiislamu muoane kwa kuzingatia misingi ya imani. Tofauti na hapo muachane tu. Uzuri he has an open heart for that.
 
Una haki ya kuvurugika. The guy is a humble man you are a fine girl. Kama nyinyi ni wa imani ya kiislamu muoane kwa kuzingatia misingi ya imani. Tofauti na hapo muachane tu. Uzuri he has an open heart for that.
Imani ya kiislamu hairuhusu watu ambao wamesha fanya zinaa kuoana.
 
Habari za humu wana JF, natumai wote mko njema.

Natambua baada ya kuleta uzi wangu huu

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Wengi walitamani nilete mrejesho, ila kutokana na kuwa busy kidogo nilikuwa naona uvivu kuandika. Basi baada ya ule uzi, nashukuru sana nilipata mawazo mengi mazuri na mabaya pia, napenda niwashukuru wote kwani kwa pamoja ilinisaidia kutafakari na kujua nini cha kufanya.

Nilikaa nikatafakari sana na kuwaza na kuwazua, katika hali ambayo sikuitegemea kumbe baby alikuwa ashagundua siko sawa akaniuliza nini mbaya nikamueleza kuwa niko sawa tu. Ila akawa anasisitiza nimueleze nini kinanisumbua, nikamwambia nimemiss kutoka nae out nje ya dar twende sehemu tuliiivu and nitaigharamia hiyo safari. Akacheka akasema wory not baby wewe sema unataka tuende wapi then nitapanga ratiba na nitagharamia. Ila nilisisitiza nitagharamia mimi. Basi akasema sawa.

Akaniambia w.end atakayokuwa na muda, tukaenda zetu Magoroto huko sehemu tuliiivu. Tukafika hotelini mida ya saa 10 jioni, tukaingia tukaoga then nikamfanyia body massage vizuuuri arelax na nk[emoji12]
Baada ya hapo akapitiwa na usingizi mziiiito, akaja kustuka saa mbili usiku. Tukatoka tukapata dinner then tukarudi chumbani. Hapa tukawa tunapiga tu story za hapa na pale na mengine.

Kesho yake tukaenda hiking kidogo kama zoezi na kurefresh akili maana mazingira ni matamu yale nyie! Tulivyorudi baada ya kuoga na kupumzika ndio sasa nikaona ni muda muafaka wa kuyatoa ya moyoni. Nilipoteza raha ghafla na aliponiuliza i started crying, akanibembeleza weee na kutaka kujua nini mbaya ndio kwa sauti ya upoleeeee na kudeka kwingi nikiwa nimemlalia kifuani nikamuuliza ana mpango gani na mimi? Nikamueleza jinsi ninavyotamani kuwa na familia yangu na nyumbani wanavyonisumbua. Pia nikamueleza kama tutaachana basi niko tayari nimrudishie kila kitu alichonipa hata kazi nitaacha maana i was only with him because of love.

Akatabasamu kisha akaniambia “mke wangu yaani hilo ndilo linakuliza? To me you are my wife, na hata ukitaka tufunge ndoa niko tayari ndio maana hadi kwenu nafahamika. Sijafanya hivyo kwa bahati mbaya love, its because i love you so much. Hebu niambie ni nini kwangu unakosa ambacho unahisi huko unakotaka kwenda utakipata, i love you Saaly please dont leave me. Ila pia sikufungi ukitaka unaweza kuniacha ila sitaki unirudishie chochote, all i did i did for love nothing else. Tena kwa furaha uliyonipa hii miaka mitatu naona kabisa bado nina deni kubwa sana kwako, sijafanya vya kutosha. Please niambie ungependa nikufanyie nini, maana vingi nilivyokufanyia vilikuwa ni suprise hivyo sina hakika kama ndivyo ulivyotaka”.
Basi nikawa nimeishiwa pozi, kichwa changu kibovu kikawa kinaniambia nimwambie anioe ila nafsi ikawa inasita. Basi nikajifaragua pale nikamwambia nampenda sana na kila alichonifanyia ni zaidi ya nilivyohitaji. Akasisitiza niwe huru nimueleze na kama kipo ndani ya uwezo wake basi atanifanyia, nikamjibu “i only need your love” akanikumbatia vikafuata vya kufuata.

Baadae alinyanyuka akaenda kwenye begi lake akaja na makratasi, akanipa. Nasoma naona ni title deeds za viwanja viwili na nyumba Morogoro zikiwa na majina yangu. Nikabaki nishangaa, nikamuambia siwezi kupokea vitu zaidi kutoka kwake. Akaniambia basi utajua mwenyewe maana tayari viko kwa majina yako. Kama huvitaki viuze.

Yakafuata mahaba motomoto then kesho yake tukarudi Dar. Akaniambia nitafakari nini nataka then nitamuambia, ndio nikavurugika zaidi.
Okay wale mlotaka mrejesho there you go.
Dada tambua kuwa wewe ni kipozeo tu kwake, java hayuko radhi kumwacha mkewe kwa ajili yako, atakupotezea tu muda kwa kujifanya anakupenda sijuwi hawezi ishi bila wewe. Wewe kama una mwingine bora umuache tu na umwambie ukweli kuwa una mtu anayetaka kukuoa, hawezi kulia wala kukasirika.
 
Back
Top Bottom