Mrejesho: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo?

Mrejesho: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo?

Habari za humu wana JF, natumai wote mko njema.

Natambua baada ya kuleta uzi wangu huu

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Wengi walitamani nilete mrejesho, ila kutokana na kuwa busy kidogo nilikuwa naona uvivu kuandika. Basi baada ya ule uzi, nashukuru sana nilipata mawazo mengi mazuri na mabaya pia, napenda niwashukuru wote kwani kwa pamoja ilinisaidia kutafakari na kujua nini cha kufanya.

Nilikaa nikatafakari sana na kuwaza na kuwazua, katika hali ambayo sikuitegemea kumbe baby alikuwa ashagundua siko sawa akaniuliza nini mbaya nikamueleza kuwa niko sawa tu. Ila akawa anasisitiza nimueleze nini kinanisumbua, nikamwambia nimemiss kutoka nae out nje ya dar twende sehemu tuliiivu and nitaigharamia hiyo safari. Akacheka akasema wory not baby wewe sema unataka tuende wapi then nitapanga ratiba na nitagharamia. Ila nilisisitiza nitagharamia mimi. Basi akasema sawa.

Akaniambia w.end atakayokuwa na muda, tukaenda zetu Magoroto huko sehemu tuliiivu. Tukafika hotelini mida ya saa 10 jioni, tukaingia tukaoga then nikamfanyia body massage vizuuuri arelax na nk[emoji12]
Baada ya hapo akapitiwa na usingizi mziiiito, akaja kustuka saa mbili usiku. Tukatoka tukapata dinner then tukarudi chumbani. Hapa tukawa tunapiga tu story za hapa na pale na mengine.

Kesho yake tukaenda hiking kidogo kama zoezi na kurefresh akili maana mazingira ni matamu yale nyie! Tulivyorudi baada ya kuoga na kupumzika ndio sasa nikaona ni muda muafaka wa kuyatoa ya moyoni. Nilipoteza raha ghafla na aliponiuliza i started crying, akanibembeleza weee na kutaka kujua nini mbaya ndio kwa sauti ya upoleeeee na kudeka kwingi nikiwa nimemlalia kifuani nikamuuliza ana mpango gani na mimi? Nikamueleza jinsi ninavyotamani kuwa na familia yangu na nyumbani wanavyonisumbua. Pia nikamueleza kama tutaachana basi niko tayari nimrudishie kila kitu alichonipa hata kazi nitaacha maana i was only with him because of love.

Akatabasamu kisha akaniambia “mke wangu yaani hilo ndilo linakuliza? To me you are my wife, na hata ukitaka tufunge ndoa niko tayari ndio maana hadi kwenu nafahamika. Sijafanya hivyo kwa bahati mbaya love, its because i love you so much. Hebu niambie ni nini kwangu unakosa ambacho unahisi huko unakotaka kwenda utakipata, i love you Saaly please dont leave me. Ila pia sikufungi ukitaka unaweza kuniacha ila sitaki unirudishie chochote, all i did i did for love nothing else. Tena kwa furaha uliyonipa hii miaka mitatu naona kabisa bado nina deni kubwa sana kwako, sijafanya vya kutosha. Please niambie ungependa nikufanyie nini, maana vingi nilivyokufanyia vilikuwa ni suprise hivyo sina hakika kama ndivyo ulivyotaka”.
Basi nikawa nimeishiwa pozi, kichwa changu kibovu kikawa kinaniambia nimwambie anioe ila nafsi ikawa inasita. Basi nikajifaragua pale nikamwambia nampenda sana na kila alichonifanyia ni zaidi ya nilivyohitaji. Akasisitiza niwe huru nimueleze na kama kipo ndani ya uwezo wake basi atanifanyia, nikamjibu “i only need your love” akanikumbatia vikafuata vya kufuata.

Baadae alinyanyuka akaenda kwenye begi lake akaja na makratasi, akanipa. Nasoma naona ni title deeds za viwanja viwili na nyumba Morogoro zikiwa na majina yangu. Nikabaki nishangaa, nikamuambia siwezi kupokea vitu zaidi kutoka kwake. Akaniambia basi utajua mwenyewe maana tayari viko kwa majina yako. Kama huvitaki viuze.

Yakafuata mahaba motomoto then kesho yake tukarudi Dar. Akaniambia nitafakari nini nataka then nitamuambia, ndio nikavurugika zaidi.
Okay wale mlotaka mrejesho there you go.
Daah 😍😍
 
Story za Kwa iddi makengo hizi
Mteja, kaka mim ni bint wa miaka 32 natembea na mume wa mtu kaninulia kiwanja ,kanijengea nyumba,kajitambulisha kwetu ,ila anaomba
Ni mbebe mimba
Iddi makengo ,dada nasema achana na huyo mwanaume ni mume wa mtu

Mrejesho wa mteja, kaka mim ni yule dada niliyekupigia simu nikakwambia natembea na mume wa mtu baada ya kubeba ujauzito huyo mwanaume kabadilika kweli Ata sjui nifanyeje

[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kama unachokifanya na unaona una furaha na upo sahihi, endelea. Ila cha kukumbuka tu, ubaya una tabia ya kujirudia haijalishi ni muda gani utapita. You'll pay the price!!!
 
Story za Kwa iddi makengo hizi
Mteja, kaka mim ni bint wa miaka 32 natembea na mume wa mtu kaninulia kiwanja ,kanijengea nyumba,kajitambulisha kwetu ,ila anaomba
Ni mbebe mimba
Iddi makengo ,dada nasema achana na huyo mwanaume ni mume wa mtu

Mrejesho wa mteja, kaka mim ni yule dada niliyekupigia simu nikakwambia natembea na mume wa mtu baada ya kubeba ujauzito huyo mwanaume kabadilika kweli Ata sjui nifanyeje
Kweli kabisa,yule kaka was facebook
 
Mkuu sana, ukweli ndio huo, hata kama ni stori ya kutunga lakini unaweza kuona response ya watu haswa wanawake, wanawake hawapendani na asilimia kubwa wengi wao hupatwa na uchungu kama wamekula ndimu karai zima kama wakimuona mwanamke mwenzao anafaidi kifedha, kimaisha, kimahusiano,n.k, comment pia kwa ujumla zinaashiria jinsi tunavyoangaliana kwa jicho la husda, inabidi kujilinda sana kila mmoja kwa imani yake, mana wachawi hua hawako mbali...
Hapana unaoona wanahasira ni wake za watu,hujaelewa tu!
Mume anauma kaka!
Atoe vitu nje wakati mna familia unafikiri muchezo?
Acha kabisa!
 
Kuna vitu haviingii akilini, ila inawezekana pia maana kuna walofanyiwa makubwa zaidi ya hayo. Ila Tanzania hii hii kweli? Hapana haiingii akilini.
Yapo Mengi tu, sema baadhi ya watu hawajakutana nayo. Lakini yapo makubwa kuliko hayo.

Hapo mdada hakuna namna. Assume tu kuwa Mke wa pili, kwa kuwa sioni dalili za kukuacha.

Ukitamka Tena utaonyeshwa nuclear weapon.
 
Back
Top Bottom