MREJESHO: Simuelewi mume wangu

MREJESHO: Simuelewi mume wangu

Poleni na majukumu, wiki kama mbili zimepita nilikuja kuomba ushauri kuwa mme wangu hataki tushiriki tendo la ndoa, nashukuru wote mlionishauri na kunitia moyo. Mungu awabariki sana.

Mrejesho upo hivi; baada ya kukaa naye chini kumuuliza shida ni nini ameishia kunijibu kuwa anatumia eti dozi ya kupunguza mwili akimaliza dozi mambo yatakuwa mazuri kama mwanzo.

Kiukweli bado sijaridhika na hili jibu, naona kama ni usanii vile. Hivi kuna dozi ya kupunguza mwili ambayo mtumiaji anakatazwa kufanya mapenzi na mke wake? Naona tu kama mapicha picha bado yanaendelea.

Naombeni mnisaidie, vipi kutakuwa na ukweli wowote kuhusu haya majibu yake?

Pia soma: USHAURI: Simuelewi mume wangu
Pole
 
Atakuwa kapita sehemu yenye mashaka,

Anamaliza matibabu asije kukuambukiza
 
Poleni na majukumu, wiki kama mbili zimepita nilikuja kuomba ushauri kuwa mme wangu hataki tushiriki tendo la ndoa, nashukuru wote mlionishauri na kunitia moyo. Mungu awabariki sana.

Mrejesho upo hivi; baada ya kukaa naye chini kumuuliza shida ni nini ameishia kunijibu kuwa anatumia eti dozi ya kupunguza mwili akimaliza dozi mambo yatakuwa mazuri kama mwanzo.

Kiukweli bado sijaridhika na hili jibu, naona kama ni usanii vile. Hivi kuna dozi ya kupunguza mwili ambayo mtumiaji anakatazwa kufanya mapenzi na mke wake? Naona tu kama mapicha picha bado yanaendelea.

Naombeni mnisaidie, vipi kutakuwa na ukweli wowote kuhusu haya majibu yake?

Pia soma: USHAURI: Simuelewi mume wangu
Labda anakunywa PEP dawa za kujikinga na virusi pindi ukichepuka na mwadhirika. Dozi ni mwezi mmoja na inatakiwa unywe ndani ya saa 72 baada ya kushiriki kitendo
 
Back
Top Bottom