MREJESHO: Ulishawahi kusingiziwa ujauzito wakati wewe si muhusika? Je, ulifanyaje kukabiliana na hali hiyo?

MREJESHO: Ulishawahi kusingiziwa ujauzito wakati wewe si muhusika? Je, ulifanyaje kukabiliana na hali hiyo?

Itel A51

Member
Joined
Jun 4, 2020
Posts
57
Reaction score
110
Habari zenu wakuu?

I hope mko poaa wanajukwaa.

Mwaka 2020 niliandika post hii kuhusu binti mmoja ambaye alikua na ujauzito wangu lakini mimi kama muhusika nilionesha kutilia shaka ujauzito huo, na sababu za mimi kuwa na mashaka niliziweka katika post hio

>>>Ulishawahi kusingiziwa ujauzito wakati wewe si muhusika?

Baada ya kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali, wanafamilia pamoja na maoni mbalimbali kutoka katika jukwaa hili, niliamua kumwambia binti kuwa AKISHAJIFUNGUA KISHA TUKIMUONA MTOTO ndio tutajua kuwa mtoto ni wa kwangu au sio.

Mtoto alizaliwa, lakini ni AMEFANANA SANA NA MAMA YAKE!!! Japo mtoto ni wa kiume lakini hakuna mfanano wa moja kwa moja na mm baba yake!

Nimewashirikisha watu kadhaa, watu wazima wenye hekima zao, na wanfamilia, wamenishauri mambo mengi, ambayo yamenipa funzo kubwa na kunifanya nichukue uamuzi wa kukubali MAJUKUMU YOTE YA KULEA MTOTO HUYU KAMA BABA HALISI, na kukubali kwa moyo mmoja na mkunjufu kuwa huyu ni wa kwangu. Nimefanya maamuzi haya kwa akili zangu timamu kabisa!.

CHANGAMOTO ILIYOPO SASA!!!
Baada ya kuamua kuwa ntalea mwanangu huyu, nkaamua kurudisha mawasiliano kwa asilimia 100% na mama mtoto wangu kwasababu hatukua kwenye mawasiliano mazuri kutokana na hali halisi. nimemueleza dhamira yangu ya kuwa baba muwajibikaji na kulea mtoto wangu huyu!

Lengo langu likiwa endapo tutayaweka mambo sawa kati yangu mm na yeye, basi tuendelee na maisha kama wanandoa coz naamini wote tulikua na makosa katika hili. Ila Bado Sijamwambia moja kwa moja kuwa dhamira yangu ni nini.

Lakini cha ajabu ni kwamba baada ya mm kujishusha na kukubali mtoto huyu, mwanamke huyu sasa yeye ndo AMEKUA NA KIBURI NA JEURI FLANIi ambayo utaiona katika mazungumzo yake na matendo yake tu. Jambo hilii linazidi kunipa mashaka na kunikatisha tamaa kabisa, coz nashindwa kuelewa tena nini kinaendelea katika akili yake.

Hivyo wadau naomba mnishauri,
  • Hii inamaana gani?
  • Niachane na huyu binti nifocus na malezi ya huyu mtoto tu? (coz nlikua na plan za kumuoa huyu dada kama tutafanikiwa kumaliza tofauti zetu)
  • Niwapotezee tu wote kwa kuassume tu hii ni life accident, nianze upya huku nkiwa nmejifunza kutokana na makosa??
  • Au nifanyaje?
MSAADA WAKUU!!
 
Miaka ya ujanani nilishabambikiwa kibendi na kibinti ambacho tulikuwa tunasoma wote.

Kwa mikwara walikuja wajomba zake kabisa kudai fidia na kutaka nichukue jukumu la kulea.
Nafsi ilikataa maana mahesabu yalikuwa hayaniingii akilini ila ilibidi nikubali tu.

Ilikuwa full vituko. Demu ananiamsha saa 8 usiku kusema anatamani supu ya utumbo mara ubuyu wa pilipili.

Baada ya kujifungua nikajibeba na zawadi zangu nikamuone mtoto, nakutana na ndugu zake nje ya wodi.
Mama mkwe mtarajiwa ananisihi nikienda ndani nisihamaki maana watoto hubadilika ukubwani.
Sikuelewa anamaanisha nini mimi nikaingia tu.

Kufika ndani mtoto mchina pure kabisa. Japo kadogo lakini unakaona kabisa kuwa hapo hakuna mswahili. Demu full kilio baada ya kuniona.
Nilisepa zangu mdogo mdogo kuepusha shari.

Kumbe demu alitembea na mchina walienda club na wenzie (mmoja wapo ndio aliniambia) akaopolewa na danga la kichina la one night stand.
Na hapo ikawa ndio ukomo wa mahusiano yetu na pona yangu.

Ushauri kama umeamua kulea wewe lea tu ila usifosi mahusiano na huyo mwanamke maana ni wazi ana mawazo mbadala ya kuwa na wewe.
 
Hii ya kusingiziwa Kuna demu nilikazana mara mbili, mara ya kwanza akaniambia kesho anaanza period, baada ya wiki nikakazana nae akaniletea story Ile Ile baada ya kama mwezi ananiambia ana mimba yangu hadi kutangaza kwa Wana, nikaona isiwe shida nikakata mawasiliano akinililia shida mara moja moja nambless vichenji ila akiniitia nyau naikana tu kininja
 
Miaka ya ujanani nilishabambikiwa kibendi na kibinti ambacho tulikuwa tunasoma wote.

Kwa mikwara walikuja wajomba zake kabisa kudai fidia na kutaka nichukue jukumu la kulea.
Nafsi ilikataa maana mahesabu yalikuwa hayaniingii akilini ila ilibidi nikubali tu.

Ilikuwa full vituko. Demu ananiamsha saa 8 usiku kusema anatamani supu ya utumbo mara ubuyu wa pilipili.

Baada ya kujifungua nikajibeba na zawadi zangu nikamuone mtoto, nakutana na ndugu zake nje ya wodi.
Mama mkwe mtarajiwa ananisihi nikienda ndani nisihamaki maana watoto hubadilika ukubwani.
Sikuelewa anamaanisha nini mimi nikaingia tu.

Kufika ndani mtoto mchina pure kabisa. Japo kadogo lakini unakaona kabisa kuwa hapo hakuna mswahili. Demu full kilio baada ya kuniona.
Nilisepa zangu mdogo mdogo kuepusha shari.

Kumbe demu alitembea na mchina walienda club na wenzie (mmoja wapo ndio aliniambia) akaopolewa na danga la kichina la one night stand.
Na hapo ikawa ndio ukomo wa mahusiano yetu na pona yangu.
Hukudai fidia yako?
 
Ngoja waje mkuu ila binafsi nakushauri usioe mwanamke mwenye jeuri na kiburi utakwisha wewe lea mtoto wako inatosha
Ahsante sana...

Kwa kweli hii jeuri nnayo iona sasa inanipa mashaka, nawaza labda huenda kwa sababu mwanzo mm ndo nlikua kauzu sasa anaona nmekua mpole kwahyo na yeye ananona ni muda wake wa kuvimba?
 
Back
Top Bottom