Mrejesho wa mliofanikiwa katika biashara ya network marketing

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Propaganda za hawa jamaa zimekua nyingi sana mara ooh nilikua professor wa chuo kikuu but now nimeacha hii fursa ndo imenifanya nikaacha kazi

Mara oooh nilikua masikini leo namiliki range rover sport 6

Oooh nilikua nafanya kazi kama bank manager nimeacha nimejiunga huku natengeneza milioni 5 kwa mwezi

Mara oooh sasa hivi natengeneza pesa napelekwa nje nishatembea nchi 20

Hizo ni propaganda zao wakati wakitafuta watu wa kuwaunga[emoji19][emoji19][emoji19][emoji19][emoji19][emoji1312][emoji1312][emoji1312][emoji1312]

Maneno yamekua mengi wengi wanaojiunga naowajua wameishia pabaya

Halafu hawasemag changamoto kazi yao ni kuhubiri mafanikio ya uongo kiujumla wanafake maisha

Mimi siwezi kupoteza pesa nijiunge vitu vya hovyo hakunaga pesa rahisi hivyo kamateni wengine lakini sio mimi
Haya mkuje wa humu mliowahi kujiunga na hizi network marketing na mkafanikiwa au mkapata changamoto mkuje
 
Akija kukushawishi usikatae kwa sharti moja tu la kukukopesha mtaji.

Unakuta anakuambia utatajirika kwa muda mfupi ila kwenye status za WhatsApp anapost maneno ya kutia moyo na uvumilivu, huku akidai mafanikio hayaji kwa haraka, na yanapatkana kwa watu wanaothubutu.
 
Nimeona post ya Idris Sultan,ametoa elimu ya wazi kabisa.ajabu watu bado watajichanganya.
 
Napata kiwewe yaani mie mwenyewe huwa nawaona wana swaga tu afu wanaganda mtu kweli.Kuna mmoja yuko Qnet yaani viatu vikula winga kachoka heri asingeenda humo.
Wanatia huruma sana
 
Kweli
Akija kukushawishi usikatae kwa sharti moja tu la kukukopesha mtaji.

Unakuta anakuambia utatajirika kwa muda mfupi ila kwenye status za WhatsApp anapost maneno ya kutia moyo na uvumilivu, huku akidai mafanikio hayaji kwa haraka, na yanapatkana kwa watu wanaothubutu.
 
Kiuhalisia hizi network marketing ni utapeli tu kama utapeli mwingine, ninawajua waliojiunga na hizo biashara hakuna chochote walichofanikiwa.

Inafika hatua mtu unaona huruma kuwauliza kuwa biashara inaendaje maana kila siku ndo wao wanakuomba hela ya vocha, unabaki unajiuliza tu milionea anaomba vocha. Tuwe makini hakuna fedha ya kuipata kirahisi duniani hapa kama wanavyoaminisha watu na shuhuda za uongo.
 
Wanasema nabii japo hakubaliki kwao,lakini huanza na mahubiri mlangoni kwao kwanza[emoji16][emoji16][emoji16],kama Yesu na israel.

Toka lini mtu akakukumbuka wewe kwenye fulsa,kaacha nduguze hukooo.
 
Kweli kabisa

Back
Top Bottom