Mrejesho wa Project ya Kutatua kero ya upukuchuaji wa mahindi

nkobhe255

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2017
Posts
234
Reaction score
292
Kuna kipindi(about 5months ago) niliwahi kuleta idea yangu ya project,

. . . Project yangu ilijikita zaidi kuweza kutatua kero ya UPUKUCHUAJI wa mahindi kijijini kwetu na baadhi ya vijiji vya jirani ambavyo huzalisha mahindi kwa kiasi kikubwa.
....... Baada ya kumaliza kutafakari juu ya kufanikisha jambo hili, ndipo nilipokuja na wazo la kutengeneza LOW COST CORN SHELLER /MAIZE SHELLER.
. . . . Kwanza kabisa nilikwenda dukani kuulizia zile za Kichina huko Mwanza, nilikutana nazo ila bei yake ilikuwa sio ya nchi hii (Tsh 2,400,000/=) kwa mashine ndogo kabisa, pia nikaona kuna changamoto kubwa ya kupata SPEAR zake.
. . . . Mwezi wa Sita(6) mwaka huu nilikwenda Dar-es-salaam kutafuta baadhi ya Vifaa ambavyo kwa Mkoani kwangu(KIGOMA) sikuweza kuvipata. Vifaa hivyo ni ELECTRIC MOTOR na SREW PANNEL. Baada ya kuvipata vitu hivyo nilikuja navyo mpaka Home.
. . . . . Nilianda DRAWINGS za baadhi ya parts za mashine hiyo bila kuangalizia popote pale, hii niliweza kulifanya kwa kuimagine jinsi mashine hiyo inavyo fanya kazi. Baada ya kumaliza ndipo nika-assemble drawings zangu into an actual kit.
. . . . . Kwa kweli nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, ila nilipoifanyia TEST, nilikumbana na Changamoto ambayo ilinikatisha tamaa, lakini kwa vile nilishapoteza pesa zangu sikukata tamaa.
. . . . . Tatizo hilo ni kwamba, badala ya Mashine hiyo kupukuchua Mahindi basi yenyewe ilianza kupukuchua na kuvipasupasua na kuwa kama vipande vipande. Nilibadilisha Assembling lakini wapi.
. . . . . . Baada ya kuona nashindwa kupata suluhisho, ndipo nilipoanza kutafuta idea tofautitofauti kutoka mitandaoni. Breki yangu ya kwanza ilikuwa humu humu JF. Baada ya kuanzisha tu uzi huo, haukumaliza hata 24hrs,ambapo MODS waliufuta bila hata kunionea huruma. Kwa kweli nilitokea kuichukia JF ndipo nilipoamua kushusha matusi kwa MODS na ku-UNINSTALL App ya JF.
. . . . Kwa bahati nzuri nikutana na articles furani za jamaa furani wa URUSI ambaye alikuwa anaelezea jinsi ya Kuassemble vifaa hivyo. Ila nako nilikutana na changamoto ambayo mpaka leo nilishindwa kuelewa. Articles zake zilikuwa na Headings za Kingereza lakini nilipofungua ndani nikakutana na lugha ya ajabu kwelikweli, Kichina sio kichina, Kiarabu sio kiarabu na wala Kihindi sio kihindi. Hapo nikaacha kwa muda wa 1week.
. . . . Lakini nilipata wazo la kuendelea kumfuatilia jamaa, kuna wazo lilinijia la kutumia GOOGLE TRANSISTOR. Hapo ndipo nilipofanikiwa kujua jamaa alikuwa anatumia lugha ya KI-RUSSIA.

Nimefanikiwa kutengeneza mashine hiyo kwa gharama ya laki 7 na nusu. Ila nimeumiza akili yangu sana tangu nizaliwe.
. . . . . Kwa kweli ni ukosefu wa mtaji tu kwa kuwa hapa kijijini nimepata ODA kama 30 za wakulima maarufu kwa thamani ya Tsh 1,200,000/= kwa mashine moja. Hii ni kwa sababu msimu wa Mavuno unakaribia ambao ni mwezi wa 5 na 6.
. . . . . Nilishawaambia kwamba sitaweza kwa kuwa sina mtaji, ila kwa atakaye toa pesa ya Advance na ODA basi nitamtengenezea ndani ya 1month.
. . . . . . Pia kwa wale wakulima ambao hawatamdu kuzinunua nimewaahidi kuwakodisha ya kwangu ambapo kwa Siku watanilipa pesa nzuri tu, ila Mafuta watanunua wenyewe.
. . . . . HAPA kuna mtu atakuwa anajiuliza mafuta ya nini tena? Mafuta haya ni ya kuwashia Generator ambayo inafua umeme wa kuendeshea motor. Mashine hii kwa kweli inanishangaza na sijui kama nitaweza kutengeneza kama hii, Gunia moja la Mahindi(Debe 6) hata dakika 10 haziishi.

MTAZAMO.
Pia nilikuwa na idea ya Kutengeneza Bajaji, ila kuna watu watanibishia, nakuhakikishia hiyo bajaji ukipata Injini ya 250cc or 13HP ndani ya 3months namaliza kazi, coz mechanism zake ni rahisi sana kama ukitumia akili yako kufikilia zaidi. Sema wengi tu wazito wa kufikilia, na hata ukifikilia wazo furani basi wewe mwenyewe una-raise CRITICISMS dhidi ya mawazo yako. Hii nitaifanya baada ya kumanage hii ya kwanza kwa zaidi ya 5yrs to come.

Thakns, nkobhe255.
 
Kila siku tunatuhumu serikali inauwa vipaji kumbe hata hawa mods nao wapo hivo hivo ni hatari kwa afya ya maendeleo badilikeni mnaacha shudu mnafuta vitu vya msingi
 
umenikumbusha nilivyokua natengeneza mashine ya kupiga/kupukuchua mpunga. iliniumiza mpaka leo lkn nimeifanikisha julai 2017 imenikondesha kutoka kiuno namba 38 mpaka 32 na uzito kutoka kilo82 mpaka 68. jumlisha na vidonda vya tumbo. anyway nilifanikiwa
 
Daaa mkuu hii kali sasa, lakini hongera
 
Never give up on your dreams, no matter what mkuu.
 
Kwa anaefaham zinapopatkana iz mashine kwa kanda ya kaskazin, anipe info plz!!
 
Kuna kipindi(about 5months ago) niliwahi kuleta idea yangu ya project,

. . . Project yangu ilijikita zaidi kuweza kutatua kero ya UPUKUCHUAJI wa mahindi kijijini kwetu na baadhi ya vijiji vya jirani ambavyo huzalisha mahindi kwa kiasi kikubwa.
....... Baada ya kumaliza kutafakari juu ya kufanikisha jambo hili, ndipo nilipokuja na wazo la kutengeneza LOW COST CORN SHELLER /MAIZE SHELLER.
. . . . Kwanza kabisa nilikwenda dukani kuulizia zile za Kichina huko Mwanza, nilikutana nazo ila bei yake ilikuwa sio ya nchi hii (Tsh 2,400,000/=) kwa mashine ndogo kabisa, pia nikaona kuna changamoto kubwa ya kupata SPEAR zake.
. . . . Mwezi wa Sita(6) mwaka huu nilikwenda Dar-es-salaam kutafuta baadhi ya Vifaa ambavyo kwa Mkoani kwangu(KIGOMA) sikuweza kuvipata. Vifaa hivyo ni ELECTRIC MOTOR na SREW PANNEL. Baada ya kuvipata vitu hivyo nilikuja navyo mpaka Home.
. . . . . Nilianda DRAWINGS za baadhi ya parts za mashine hiyo bila kuangalizia popote pale, hii niliweza kulifanya kwa kuimagine jinsi mashine hiyo inavyo fanya kazi. Baada ya kumaliza ndipo nika-assemble drawings zangu into an actual kit.
. . . . . Kwa kweli nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, ila nilipoifanyia TEST, nilikumbana na Changamoto ambayo ilinikatisha tamaa, lakini kwa vile nilishapoteza pesa zangu sikukata tamaa.
. . . . . Tatizo hilo ni kwamba, badala ya Mashine hiyo kupukuchua Mahindi basi yenyewe ilianza kupukuchua na kuvipasupasua na kuwa kama vipande vipande. Nilibadilisha Assembling lakini wapi.
. . . . . . Baada ya kuona nashindwa kupata suluhisho, ndipo nilipoanza kutafuta idea tofautitofauti kutoka mitandaoni. Breki yangu ya kwanza ilikuwa humu humu JF. Baada ya kuanzisha tu uzi huo, haukumaliza hata 24hrs,ambapo MODS waliufuta bila hata kunionea huruma. Kwa kweli nilitokea kuichukia JF ndipo nilipoamua kushusha matusi kwa MODS na ku-UNINSTALL App ya JF.
. . . . Kwa bahati nzuri nikutana na articles furani za jamaa furani wa URUSI ambaye alikuwa anaelezea jinsi ya Kuassemble vifaa hivyo. Ila nako nilikutana na changamoto ambayo mpaka leo nilishindwa kuelewa. Articles zake zilikuwa na Headings za Kingereza lakini nilipofungua ndani nikakutana na lugha ya ajabu kwelikweli, Kichina sio kichina, Kiarabu sio kiarabu na wala Kihindi sio kihindi. Hapo nikaacha kwa muda wa 1week.
. . . . Lakini nilipata wazo la kuendelea kumfuatilia jamaa, kuna wazo lilinijia la kutumia GOOGLE TRANSISTOR. Hapo ndipo nilipofanikiwa kujua jamaa alikuwa anatumia lugha ya KI-RUSSIA.

Nimefanikiwa kutengeneza mashine hiyo kwa gharama ya laki 7 na nusu. Ila nimeumiza akili yangu sana tangu nizaliwe.
. . . . . Kwa kweli ni ukosefu wa mtaji tu kwa kuwa hapa kijijini nimepata ODA kama 30 za wakulima maarufu kwa thamani ya Tsh 1,200,000/= kwa mashine moja. Hii ni kwa sababu msimu wa Mavuno unakaribia ambao ni mwezi wa 5 na 6.
. . . . . Nilishawaambia kwamba sitaweza kwa kuwa sina mtaji, ila kwa atakaye toa pesa ya Advance na ODA basi nitamtengenezea ndani ya 1month.
. . . . . . Pia kwa wale wakulima ambao hawatamdu kuzinunua nimewaahidi kuwakodisha ya kwangu ambapo kwa Siku watanilipa pesa nzuri tu, ila Mafuta watanunua wenyewe.
. . . . . HAPA kuna mtu atakuwa anajiuliza mafuta ya nini tena? Mafuta haya ni ya kuwashia Generator ambayo inafua umeme wa kuendeshea motor. Mashine hii kwa kweli inanishangaza na sijui kama nitaweza kutengeneza kama hii, Gunia moja la Mahindi(Debe 6) hata dakika 10 haziishi.

MTAZAMO.
Pia nilikuwa na idea ya Kutengeneza Bajaji, ila kuna watu watanibishia, nakuhakikishia hiyo bajaji ukipata Injini ya 250cc or 13HP ndani ya 3months namaliza kazi, coz mechanism zake ni rahisi sana kama ukitumia akili yako kufikilia zaidi. Sema wengi tu wazito wa kufikilia, na hata ukifikilia wazo furani basi wewe mwenyewe una-raise CRITICISMS dhidi ya mawazo yako. Hii nitaifanya baada ya kumanage hii ya kwanza kwa zaidi ya 5yrs to come.

Thakns, nkobhe255.
mkuu kwa nn ukufikiria ya kutumia waterpump badala ya electric motor kwa maana ya challenge ya vijiji hakuna umeme ht km utatumia generator vp huon bdo km unamizigo ming ktk kuitransport sehem mbal mbal vijijin..
 
Back
Top Bottom