Mrejesho wangu katika jitihada na mchakato wa kufungua biashara, kutafuta vibali katika Mamlaka mbalimbali

Jiang Yang

Senior Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
182
Reaction score
111
Habari zenu wapendwa. Kama kijana (mid 20's) ambaye kwa muda mrefu nimekuwa na ndoto ya kufanya biashara na ujasiriamali hivi karibuni nimeamua na kuanza kuchukua hatua ili kutimiza ndoto zangu za kuanzisha biashara na kuwa na mafanikio. Nikiwa mmoja wa waumini wakubwa wa kufanya biashara zilizo rasmi ni kimaanisha kuwa na vibali vyote husika pamoja na kulipa kodi, nimeona ni vyema nikaanza mchakato huu huku nikiwashirikisha wadau hapa changamoto nitakazo kutana nazo katika safari yangu hii.

Nitafanya mchakato huu bila kutumia njia fupi zozote ikiwemo kutoa rushwa wala connection (lengo pia ni kujua jinsi gani mifumo yetu ni rafiki kuwezesha biashara) .Kwa kifupi biashara niliyoamua kuanza nayo ni biashara ya uwakala wa Pesa (hasa makampuni simu). Nafahamu kuwa moja ya vielelezo vinavyohitajika katika kuomba uwakala katika kampuni hizi ni kuwa na TIN inayotolewa na TRA, pia kuwa na Leseni ya biashara unayotolewa na Afisa Biashara wa manispaa au mji husika. Basi nitaanza na TRA ili kupata TIN ambapo kwa mimi nilipo ni Manispaa moja hapa nchini

Stage 1. TRA kupata TIN
Mapokezi TRA baada ya kueleza kuwa ninahitaji TIN muhudumu aliuliza ni aina gani ya biashara ninayotaka kufanya, nikajibu biashara ya UWAKALA wa PESA wa mitandao ya simu. Muhudumu akasema ilinihudumiwe ninapaswa kwenda na "Barua ya utambulisho toka Mitandao husika ya simu".

Ofisi za mitandao hii hazikuwa mbali, nilienda ofisi za Tigo nakuwaelezea kuwa TRA wanasema ili niombe TIN namba ni lazima niwe na barua ya utambulisho toka kwenu (Makampuni ya Simu). Watu wa Tigo walinijibu hawajawahi kutana na case kama hiyo wala kuombwa document kama hiyo na watu wanaoomba uwakala kwao. Jibu hili hili nilipewa katika ofisi za Vodacom na Halotel.

Nikarudi kwa muhudumu wa TRA nakumueleza uhalisia niliokutana nao, akajitetea kuwa hao watu katika hayo makampuni ndio wananizungusha maana watu wengi wanaokuja na shida kama yangu hapo TRA huwa wanaenda kupewa barua za utambulisho. Akaendelea kusema kuwa yeye hana sababu ya kunizungusha maana angependa sana nipate TIN na niwe mlipa kodi.

(Swali; Inawezekana watu wote 3 toka ofisi 3 tofauti za makampuni tofauti wakaamua tu kunizungusha kunipa barua ombi ya utambulisho kwenda TRA ili nipatiwe TIN no.? kwa kufanya hivyo wanafaidika na nn?). Mwisho mtu huyo wa TRA alinishauri niende kwa mtendaji wangu kuchukua barua ya utambulisho kisha niende nayo manispaa kwa Afisa Biashara ambaye atanipa form ambayo nikiikamilisha nitaenda TRA na watanipatia TIN. Kwa leo niliishia hapa..nitaendelea na mrejesho wa hatua zitakazo fuata..

Note; Baada ya kuandika hatua ya kwanza, nashukuru wadau mbalimbali walionipa mawazo kuhusu hiyo case ya jamaa wa TRA. Nimefahamishwa kuwa ni rahisi sana kuapply TIN online kwenye tovuti. Nashukuru wote mliotoa mawazo, yamekuwa na msaada mkubwa.

Stage 2. Leseni ya Biashara Manispaa, ofisi ya Afisa Biashara.

Baada ya kuachana kwanza na mchakato wa kutafuta TIN, nikaamua kwenda kufuatilia leseni ya biashara kwanza inayotolewa Manispaa ofisi ya Afisa Biashara. Lakini kwa maelezo niliyoshauriwa na yule mtu wa TRA ni kuwa nianzie kwa Mtendaji kwanza kupata barua ya utambulisho wa eneo ninalotaka kufanyia biashara, hapa kwa mtendaji waliniambia niende kwanza Manispaa kupewa form ya kuomba leseni ndipo wao watafauta kuhusika katika kukagua. Nikaelekea Manispaa ofisi ya Afisa biashara na kumuelezea shida yangu ya kufungua biashara ya UWAKALA wa PESA.

Mtu wa Manispaa kanielewesha kuwa ili wanihudumie ninapaswa kuwa na barua toka kwa “Mwenyekiti wa Mtaa” ninaotaka kufungua biashara, nilimweleza nimetoka ofisi ya Mtendaji nimeambiwa nije huku, akasema wao wanamtaka Mwenyekiti wa Mtaa na si Mtendaji. Nikaondoka na kumtafuta Mwenyekiti wa mtaa. Nimefanikiwa kupata barua toka kwa Mwenyekiti wa Mtaa bila usumbufu sana.

Baada ya kuipeleka barua ya Mwenyekiti wa Mtaa Manispaa nikaulizwa kama tayari nimeshaanza biashara, nikasema bado, na pia nikaulizwa kama tayari nina ofisi, sikuwa nayo pia (Sikuwa nayo sababu sikutaka kulipia kodi ya frame kabla ya kujua hizi hatua za usajiri ni ngumu na ndefu kiasi gani).

Manispaa wanataka lazima uwe na ene la biashara tayari (Mkataba wa eneo unalofanyia biashara utaambatanishwa na barua ya mwenyekiti wa Mtaa katika maombi ya leseni). Hapa ninaelekea kukamilisha ulipiaji wa eneo (frame) ya kufanyia biashara ili niendelee na hatua za kupata leseni Manispaa. Nitaendelea...

Stage 3. Nimefanikiwa Kupata TIN na Tax Clearance Certificate.

Nilifanikiwa kuelewana na mwenye Frame (eneo la biashara), na kuandikishana mkataba, ambapo mkataba huo ulikuwa ukihitajika manispaa kama moja ya viambatanisho (pamoja na barua ya mwenyekiti wa Mtaa) ili nikidhi vigezo vya kupatiwa leseni ya biashara katika mtaa wangu.

Mara tu banda ya kupata mkataba wa eneo la biashara nilielekea manispaa ofisi ya afisa biashara ambapo alipitia form walizonipa hapo awali na nilishaijaza, form hiyo niliambatanisha na barua ya m/kiti wa mtaa na huo mkataba. Bila kupoteza muda aliisaini hiyo form na kuniambia sasa unaweza kwenda TRA (ili nikapatiwe TIN na Tax Clearance) Kisha nitarudi Manispaa kwa ajili ya kukamilisha process za kupata leseni ambapo ni lazima niwe na hiyo Tax Clearence toka TRA. Nilienda TRA na reception siku hii nilimkuta mtumishi mwingine tofauti na yule aliyenihudumia mwanzo (kama nilivyoeleza huko juu stage 1).

Mhudumu alinipeleka sehemu husika na baada ya muda nilipelekwa chumba flani maalumu kwa ajili ya kukadiliwa kodi yangu ambapo niliulizwa maswali kama 1. Unategemea kuwa na float ya sh.ngap? 2. Unategemea kupata commision kiasi gani. 2. Unalipia kodi kiasi gani ya frame? etc.

Baada ya hapo zilifuata process kadha wa kadha ikiwemo kupigwa picha, kusubiri waPrint TIN certificate yangu, kufanyiwa assessment, na kwenda kulipia % flani ya kodi ya frame,,,hapa nilielimishwa kidogo, kuwa TRA wanacharge % flani (aliitaja, kama sikosei ni 10%,,,sina uhakika) ya kodi unayolipa ya frame…hii anapaswa kuilipa mwenye eneo lakini wananitumia mimi kuikusanya…hivyo ninapaswa kila ninapolipa kodi kwa mwny eneo nikate % nitakayoilipa TRA.

Nilienda bank kufanya malipo (ilikuwa hela ndogo tu.)Baada ya kulipa BANK nilipewa Tax Clearance Certificate, hapa tayari nikiwa nimeshapewa TIN certificate. Kisha nikaelekea Manispaa kumalizia hatua za kupata leseni. Manispaa walinipa Bill ya kwenda kulipia BANK….ilikuwa ni hela ambayo nilikwisha jiaanda (Chini ya laki moja kwa Mwaka) hivyo nilienda kuilipa fasta. Nilirudisha stakabadhi na kuambiwa kurudia leseni baada ya situ 2. Inaendelea...

4. Update: Business Licence ✅ (Done)

5. Vodacom, Halotel, Aitel Line Pending...

Vodacom wanatoa kuanzia week hadi mwezi, Halotel ni siku kadhaa na Airtel ni week mbili.

Tigo ndo hawaeleweki, naambiwa kauli ile ile, kuwa wamesitisha kupokea maombi ya mawakala wapya kwa muda usiojulikana niendelee kupiga simu kuulizia!! Tigo Shop kabisa.
Funny fact, ukiulizia kwa njia mbadala mtaani line zinapatika na bei unapewa kabisa! na unahakikishiwa kuipata same day.

6. Nimeanza biashara rasmi leo
Ikiwa inakaribia kutimia week ya 2 (yaani siku 12 ukihesabu na weekend) tangu nianze mchakato huu, leo nimeanza rasmi biashara yangu. Japo naendelea kusubiri line zingine ambazo huchukua muda tofauti tofauti kuzipata kama nilivyoeleza katika hatua zilizopita huko juu, nimeanza na line ya mtandao wenye wateja wengi zaidi katika eneo hili, hivyo kutokuwa na line zote hakutanirudisha nyuma sana. Hii ndiyo itakuwa update ya mwisho katika uzi huu.

Mwisho.
Naamini uzi huu utasaidia watu wengine huko mbeleni, nashukuru kwa kila aliyeshiriki kwa namna tofauti tofauti kutoa ushauri na maoni. Nitaendelea kuufuatilia uzi hii, kujibu maswali (kama yatakuwepo) ama kujifunza tu zaidi toka kwa wadau.
Asanteni!.
 
Kaka acha kupotosha kwa TRA TIN unajipatia mwenyerwe kwani asa hv wamewezesha kwa kumfanya mlipakodi ajipatie TIN mtandaoni bila hata kufika TRA hivyo basi nakusiii ingia kwenye mtandao waTRA alafu chukua iyo TIN then nenda kwenye mkoa wa kodi husika uweze kupritiwa certificate yako na uweze kupata tax clearance kwa ajili ya kupata business licence kutoka manispaa husika kwa makadirio siku wanatoa mpaka siku 90 au 6 monthes kufanya biashara bila kulupa kodi

Note:inakubidi uwe na kitambulisho cha utaifa NIDA na kama huna TRA wana barua maalum yakukupa ili uweze kuarakisha mchakato wa kupata namba ya utambulisho wa taifa NIDA
 
TRA huwa wanazingua sana hawa jamaa...ni wapuuzi
.

Hao si bure walitaka kupata kitu toka kwako.
 
Hiyo ofisi ya TRA uliyoenda ni wapi? Kuwa wazi. Kesho asubuhi kaombe kuonana na meneja mweleze ulichojibiwa na huyo mtumishi.
 
Kamuripoti Takukuru hakika watajuta kukufahamu ..
 
Mm naomba niulize HIV ukichukua kitambulisho cha ujasiliamal so sawa na mtuu mwenye tin namba?? Msaada please
 
Hahhahaaaa sasa tin no mpaka uwe na barua?......nenda kawaambie unataka kununua gari au pikipiki chapu watakupa.......ila baadae utaibadilisha na kuwa mulyipurpose
 
We binti sasa hapo mtoa mada kapotosha nini? Kwa hiyo mtu asiyejua hata kutumia Internet naye aende kwenye website ya tra? Acha kujifanya mjuaji wakati kichwani empty, haya mambo ya kuzungushana bado yapo sana Tanzania, kila kitu ukifatilia unazungushwa hadi ukome... Kuna siku nilikua nna shida ya kusainisha doc wizarani, ambayo ingeweza kusainiwa Dar ila nikaambiwa Nenda Dodoma, nimefika Dodoma naambiwa anayepaswa kunisainia yuko Dar, nawakati naondoka Dar alikuwepo huyo mtu.. Baada ya kutoa malalamiko yangu wakaishia tu kuniomba msamaha
 
Nime update original post, Stage 2, Leseni ya Biashara Manispaa, ofisi ya Afisa Biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…