Mrejesho: Watoto wa mstaafu baada ya kupewa mitaji na baba yao

Nejad Rocket

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2017
Posts
298
Reaction score
197
Hi great thinkers baada ya juzi mwalimu mstaafu kuwapa mitaji wanae pesa zimeanza kutumika kama ifutavyo:

Watoto wa kike wawili wamenunua shamba ekari tano wameshanunua miche ya michungwa wanajiandaa kuipanda.

Wawili wa kike kila mmoja wamenunua vifaa vyote muhimu vya kufungua migahawa ikiwemo meza viti mapoti makubwa chupa za chai sahani wanaendeleza na kuboresha migahawa walikuwa wakifannya hivyo awali.

Mwalimu kanunua machine ya kutotolesha vifaranga anaboresha banda lake la kuku na bata pia mbuzi.Mdogo wao wa mwisho wamempeleka Veta Tanga kusomea mechanics.Nitaendelea kuwapa updates.
 
safi kabisa,Mungu awaongoze
 
Hivi ukistaafu unawapa mafao yako watoto wako au unayahifadhi na kuwekeza yakusaidie siku za usoni? binafsi nawekeza sana kwenye elimu ya wanangu na kuwafundisha kujitegemea. Mafao nitayatumia na mama yao nikija staafu inshallah
 
Funzadume acha uchoyo [emoji35]
 
sio uchoyo wape watoto elimu bora kipindi ukiwa na nguvu sio kuwaacha mkaja kugawana mpaka mafao yako ya uzeeni. Kipindi unastaafu watoto wanatakiwa wawe msaada kwako na sio wewe unawasaidia huko ni kufeli kwa hali ya juu
Hujasoma thread iliyopita aliyefanikiwa ni mmoja tu kati ya watoto sita hivyo akaona awape mtaji wanae hata hivyo akija zeheka hao hao watoto watakuja msaidia tu
 
kweli sikusoma topic ya kwanza ila kuna mapungufu tayari kumbe. Pole yake hata hapo kufanikiwa itakuwa ngumu sana Zaidi kutakuwa na kulaumiana tu anyway maji yameshamwagika hayazoleki
 
Duuu mkuu umenivutia sana ntaifuatilia hii thread hadi mwisho [emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
sio uchoyo wape watoto elimu bora kipindi ukiwa na nguvu sio kuwaacha mkaja kugawana mpaka mafao yako ya uzeeni. Kipindi unastaafu watoto wanatakiwa wawe msaada kwako na sio wewe unawasaidia huko ni kufeli kwa hali ya juu
Mkuu alietaka kuwagawia ni mzee mstaafu mwenyewe kwa lengo la kuwasaidia wanae. Hizo fkra zako zipo sahihi lkn Mshua kafanya hvyo kwa Upendo.
 
Kuna haja ya kutolewa semina kabla mstaafu hajapewa mafao ili tupunguze vifo vya kabla ya wakati vya hawa wazee. Zile pesa sio za urithi na sio nyingi kama ambavyo huwa zinaonekana mara zinapotolewa. Zinatakiwa kutumika kumuweka mstaafu katika hali njema uzeeni.
 
Kama mzee alishajijenga mzee hata awe na mamilioni atazimaliza kidogo kidogo akizinywa chai kahawa matako ya ngombe chapati mayai kuku na nke MDOGO kuwapa watoto kawekeza isitoshe watoto hawakufanikiwa kielimu.Zikijaisha watoto watamtenga kabisa huku wakimwambia fainali uzeeni
 
sio uchoyo wape watoto elimu bora kipindi ukiwa na nguvu sio kuwaacha mkaja kugawana mpaka mafao yako ya uzeeni. Kipindi unastaafu watoto wanatakiwa wawe msaada kwako na sio wewe unawasaidia huko ni kufeli kwa hali ya juu
Mkaka ya Leo sio yenu,elimu pekee bila pesa/mtaji sio msaada kivile ikizingatiwa watu walisoma wapate ajira na ajira zinazingua
 
Hata mie ukipiga pesa kivyako vyako zikiisha utulie hivyo hivyo kama ulivyotulia wakati unazila,tusisumbuane coz kila mtu akomae kivyake,kunisomesha ni sehemu ya wajibu wako wa malezi sio fadhila
 
Hi great thinkers baada ya juzi mwalimu mstaafu kuwapa mitaji wanae pesa zimeanza kutumika kama ifutavyo:

Watoto wa kike wawili wamenunua shamba ekari tano wameshanunua miche ya michungwa wanajiandaa kuipanda.

Wawili wa kike kila mmoja wamenunua vifaa vyote muhimu vya kufungua migahawa ikiwemo meza viti mapoti makubwa chupa za chai sahani wanaendeleza na kuboresha migahawa walikuwa wakifannya hivyo awali.

Mwalimu kanunua machine ya kutotolesha vifaranga anaboresha banda lake la kuku na bata pia mbuzi.Mdogo wao wa mwisho wamempeleka Veta Tanga kusomea mechanics.Nitaendelea kuwapa updates.
Sijaelewa mantikiq
 
Hivi ukistaafu unawapa mafao yako watoto wako au unayahifadhi na kuwekeza yakusaidie siku za usoni? binafsi nawekeza sana kwenye elimu ya wanangu na kuwafundisha kujitegemea. Mafao nitayatumia na mama yao nikija staafu inshallah
ni kweli ila mambo yanabadilika wenzetu familia zinakuwa tajiri kwa kuwa wanawezeshwa na wazazi/familia zao mfano bakresa,manji,rothschilds,rockefeller sasa sisi wazee wakiondoka waliobaki mnaanza upya badala ya kuendeleza walipoanchia wazazi. me naona hajakosea kwanza amechelewa sa hivi angekuwa na vitega uchumi vya kutosha ni kama anasahihisha makosa yake kwa watoto wake na kizazi kijacho. ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na masikini wanazidi kuwa masikini.
 
sio uchoyo wape watoto elimu bora kipindi ukiwa na nguvu sio kuwaacha mkaja kugawana mpaka mafao yako ya uzeeni. Kipindi unastaafu watoto wanatakiwa wawe msaada kwako na sio wewe unawasaidia huko ni kufeli kwa hali ya juu
Na hiyo mzee aliwa nyima elimu ndipo alipokosea
 
ni kweli ila mambo yanabadilika wenzetu familia zinakuwa tajiri kwa kuwa wanawezeshwa na wazazi/familia zao mfano bakresa,manji,rothschilds,rockefeller sasa sisi wazee wakiondoka waliobaki mnaanza upya badala ya kuendeleza walipoanchia wazazi. me naona hajakosea kwanza amechelewa sa hivi angekuwa na vitega uchumi vya kutosha ni kama anasahihisha makosa yake kwa watoto wake na kizazi kijacho. ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na masikini wanazidi kuwa masikini.
Matajiri wanawekeza elimu kwa watoto wao na wanawaandaa sana ili wazidi kuwa matajiri Zaidi ya wao. Hapa kosa ni kutowapa elimu bora watoto ambapo mwisho wa siku wanakuja kula mafao yako ya uzeeni na matokeo yake hapo ni lawama tu baadae kuwa nilikusaidia na wewe unisaidie wakati hilo lilitakiwa lije automatic
 
Back
Top Bottom