Mrejesho

Kuna kitu mnakosea sana hasa mnapotafuta wenza mitandaoni.

Unapotafuta mwenza mitandaoni, usielezee hali halisi ya uchumi wako, hiyo inakusaidia wewe kumpata na kumjua akupendaye kwa dhati.

1. Kama una kipato cha 400,000/= kwa wiki basi mwambie unapata 150,000/= kwa wiki.

2. Kama umeshajenga nyumba yako nzuri, mwambie umepanga tu.

3. Kama wewe ni Waziri, basi mwambie wewe ni DC.

4. Kama una gari lako, mwambie umelikodisha au ni mali ya rafiki yako.

Tatizo wanaume wengi tunapendana tuonekane ma-doni fasta hata kwa mtu usiyemjua kwa undani zaidi.
 
Hivi unadhani wao hawamchunguzi muowaji? Kwani ukitaja chini ya ulivyonavyo, huna watu nje yako wanaojuwa hali yako halisi na kwamba anaweza akapata taarifa huko?
 
Kama unataka kuanzisha mahusiano mitandaoni.

Jenga urafiki kwanza...kwenye kujenga urafiki utaanza kupembua pumba ni zipi na mahindi ni yapi.

Wala usimwambie natafuta mwenza maana ataigiza. Binafsi siamini mwenza anatafutwa kwa kutangaza kama unauza kiwanja.

Hatuwezi kuvi-ignore vigezo vya vitu kwenye mapenzi ila hivi vinakuja baadae saana. Sasa wewe unatafuta mwenza cha kuanza kutanganza awe na kazi/nina kazi/ nina mshahara kiasi fulani...tayari ni kama unanadi kiwanja. Hayo mambo ni ya mwisho saana unapoamua kupenda.
 
Kumbuka wakati huo mnakuwa kwenye Long distance relationship.
Tena yawezekana hamjaonanana.
Hivi unadhani wao hawamchunguzi muowaji? Kwani ukitaja chini ya ulivyonavyo, huna watu nje yako wanaojuwa hali yako halisi na kwamba anaweza akapata taarifa huko?
 
Hivi mnao tafuta wenza mitandaoni huwa mko serious kweli au changamsha genge, Mwanaume unakosaje mwanamke mtaani, kazini barabarani.Huwa nachukulia mmeshindikana huko mnako ishi.
 
Ni vizuri kama umeligundua hilo mapema. Just tuliza mindset yako sasa...ili ufukie vizuri mashimo ya ujana wako.

Nje ya hapo, utakuwa unajitekenya na kujicheka mwenyewe!.
 
Hivi mnao tafuta wenza mitandaoni huwa mko serious kweli au changamsha genge, Mwanaume unakosaje mwanamke mtaani, kazini barabarani.Huwa nachukulia mmeshindikana huko mnako ishi.
Wengine hatutaki kuoa kwetu.
 
Ni vizuri kama umeligundua hilo mapema. Just tuliza mindset yako sasa...ili ufukie vizuri mashimo ya ujana wako.

Nje ya hapo, utakuwa unajitekenya na kujicheka mwenyewe!.
Nilikuwa nasikia watu wakisema "bora ukosee maisha kuliko kuoa" hapa ndo napata picha safi na kugundua wale vijana wazamani walio kuwa wanatafutiwa wake na wazee wao hawa hawakuwa wajinga.
 
Kwa mfano mimi kazi yangu naingiza 7000 per day nimdanganye naingiza sh.ngpi mkuu?
 
Sio mke tu mkuu hata michepuko pia inataka kujua inatembea na mtu mwenye nguvu gani ya kiuchumi.Ni bahati sana kupata wa kuanza naye chini mpaka kufikia mafanikio,na hata ukimpata anaweza kuwa hujampenda.Cha muhimu tafuta ela,hayo yote yatapita.
Una maanisha mapenzi pesa now days.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…