Uchaguzi 2020 Mrema na wanachama wa TLP wamlaki Magufuli Himo, awaombea kura wagombea wa CCM na kumzawadia Magufuli Mbuzi

CCM Damu

Member
Joined
Oct 29, 2007
Posts
15
Reaction score
28
TLP leo imemlaki Magufuli katika eneo la Himo jimboni Vunjo.






Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga Mrema

Akizungumza mara baada ya Rais kumpa nafasi ya kumuombea kura, Mrema amewaambia watu wa Himo na Vunjo kuwa kura zote kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli na ubunge kura ziende kwa Dk. Charles Kimei.


Mzee Agustino Lyatonga mrema pia alileta mbuzi mkubwa pamoja na mkungu wandizi kwaajili ya zawadi ya Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli.
 
Inteligensia ya Mrema kubwa " huwezi pambana na adui ungana nae"
 
TLP na wengineo, Haya ndio matawi ya mche wa mboga mboga ambayo yanafanya drama kwa wanachi sijui wanawachukuliaga wa tanzania wa ni wale wa miaka ya 2000 wenye uelewa mdogo...
 
Mrema ni Mzalendo, achana na wale Wasaliti wa Nchi
 
Nasubiri kauli, karipio, onyo, maelekezo, barua, wito, katazo au msimamo wa ofisi ya msajili wa vyama, na hasa hasa Bwana, Jaji Fransi Mutungi na Sisty Nyahoza.

Karibu, tunawasikiliza.!
 
Hongera Mrema
 
Mrema amejitoa?

Tume na Msajili kimyaa
 
Hiyo ni fursa kwa Chadema na NCCR Mageuzi kuunganisha nguvu ili mmoja wao ashinde
 
Siasa za kijinga ndio huwa zinapendwa na CCM Ndugu zangu Watanzania tungalie mustakbali wa Maisha yetu tusidanganywe na Mambo ya kijinga kijinga na rangi rangi wakati Maisha yetu ni magumu kuliko zamani
CCM ni mabingwa wa kulaghai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…