whitehorse
JF-Expert Member
- Aug 29, 2009
- 2,565
- 4,432
Hello wana Chit - Chat
Nilikuwa napiga story ofisini na mates wenzangu tulikuwa na story za namna ya kuimaliza weekend ya mwisho wa mwezi bila vishawishi vya kutumia pesa ovyo ndio ikaja topic ya jinsi hali ngumu ya uchumi ilivyofanya watu wabadili utaratibu wa kula makange, pizza na burger huko kwenye food corners na maeneo mbalimbali ya kula bata batani hapa mjini.
Sasa kuna mate wangu akatupa story hii yeye ana mpenzi wake kweli mzuri sana wa sura na umbo ila tabia me sijui nadhani anaijua mpenziwe akatusimulia jinsi alivyochoka na umbumbu wa mrembo wake kwenye masuala ya kuandaa vyakula jikoni. Akasema alimshtukia mrembo siku myingi kuwa kwenye mapishi yuko ovyo hivyo akaamua kukaza a hapo hapo ili ajiridhishe kama ni kweli au hisia zake tu.
Huyu jamaa alipata kijisafari cha mkoani week zilizopita wakati anarudi akabeba kuku wa kienyeji huko njiani. Weekend iliyofuata akamkaribisha mrembo waje wamshughulikie. Jamaa anasema alimtafuta hamisi chinjachinja wa mtaani akampiga kisu ili awe "halal" kazi ikaangukia kwa mrembo sasa. Mrembo hajui manyoya kama hutolewa na maji moto jamaa akatoa maelekezo maana aliona mrembo haelewi namna ya kumnyonyoa kuku manyoya
Mrembo akafanikiwa kuweka maji moto na kuanza shughuli ya kumtoa manyoya kuku huku amenuna hamna mfano ☹️☹️☹️
Baada ya kumnyonyoa kilichofuata hapo ni kumkata vipande maana kama mjuavyo kuku ana vipande vyake kadhaa vinajulikana kwa macho na majina kama vile paja, kipapatio, shingo, firigisi na kadhalika jamaa anasema aliondoka jikoni akamuacha mrembo aendelee na phase (hatua) ya pili
Anasema baada ya muda mfupi aliamua kumchungulia mrembo wake ili kujua anaendeleaje na mambo ya butcher akakuta mrembo yuko busy anakataka nyama kwa mtindo wa ajabu kabisa alikuwa anakatakata vipande vidogo vidogo kama vya mishkaki . Jamaa akaona hii kali lakini alijipa moyo kuwa labda mrembo ana mikato yake ila jamaa anasema alikosa raha hakuamini alichokiona akaamua amuache aendelee kuandaa yule ndege kwa style ile mpya machoni pake.
Baadae akaendela na mapishi kule jikoni akapika na wali jamaa anasema alishindwa kula hata kipande kidogo maana kuku alikuwa haeleweki shingo imechanganyika na kipande cha kipapatio badala yake nyama ikawa inatisha sio kidogohalafu anasema ilikuwa na harufu ya mavi ya kuku anahisi utumbo ulikatwa katwa na hivyo kinyesi kikatapakaa kwenye minofu
Jamaa amepanga mkakati kwa sasa anafanya utaratibu wa kumtafutia kisa kidogo tu mrembo yule ili amuache mara moja ameona hana vigezo vinavyoendana na mambo ya jikoni. Mrembo ana miaka 24 hajui kuandaa kuku mbichi amezoea kutoa order vibandani " chips kuku paja funga na pilipili pembeni" na akiletewa kuku mwenye manyoya anashindwa kuonyesha hilo paja na kidari viko wapi
Weekend njema wana Chit-chat