Mrembo Irene anayedaiwa kuchepuka na Diamond kumbe ni mwanafunzi

Foolish age ni jipu kwa kwli!!!!kwa sasa hajui madhara yke atakumbuka shuka kumekucha wamemtumia,wAmemzeesha hana jipya ndo ningejua zinaanzia hpo lol inasikitisha sana kwa maisha ya sasa uschana kz sana!!!!
 
Kama unakumbuka vizuri Akon aliwahi kumtumia msichana mdogo kwenye video shooting. Ile issue ilimsumbua sana na hata mauzo ya ile video yalikuwa kiduchu kutokana na kukiuka maadili na haki za watoto.
Kwa hili kama Diamond akigundulika kutumia vijana wa shule kwenye kazi zake, hawezi kukwepa mzigo wa lawama na taratibu za kisheria kama zipo.
means mtu akiwa ana miaka 18++ ndio anatakiwa kutokea kwenye kichupa?? mbona siku hizi watoto wadogo wanaimba na wanatokea kwenye videos..u mbululaz.. hiyo sio kweli.. huyo binti aliacha shule SIMBA akaona anafaa kwenye video.. note..dogo ashlay, dogo janja, blue..kuna madogo wengi tuu wanatokea kwenye video za nyimbo za injili
 
Kwanza napenda ufahamu kwamba sio wote hupenda kutumia matusi katika kuwasilisha hoja au kutofautiana katika hoja. Tunapenda saana lugha isiyo na ukakasi ili wengi wafahamu uwasilishaji wa mawazo.
Nikirejea katika muktadha wa lililo mezani sidhani kama Bwana Diamond ataridhika saaana anapoambiwa kwamba yule aliyemshirikisha aliacha kusoma na kukinzana na maagizo ya serikali kuhusu elimu. Tafakari kidooogo umuhimu wa elimu na maagizo ya serikali kuhusu wanaoacha shule.
 
wakati diamond anamchukua huyo binti alikua ameshaacha shule na alimchukua kama binti wa mitaani.. tukirudi nyuma mbona watoto wadogo wengi tuu wanaonekana kwenye tv na wala maendeleo yao hayajulikani na haijazua mzozo kama hili.. Je unadhani diamond asingemtumia kwa kua ameacha shule?? au mlitaka amsomeshe?? hapo kwanza kumtoa kwenye video ni msaada sana.. wengi walioacha shule na hawana wazazi wanauza miili yao BUGURUNI, sinza na wengine ni machokoraa.. nadhania diamond apewe heshima na pongezi kubwa kwa kumnusuru huyo binti na hayo majanga
 
South ya Tandale mkuu...

Si unajua watoto wa uswazi wakiwekwa kinyumba lodge huwa wanadanganya home kuwa wako south??
Mimi naona amejigundua mapema, sio kila mtu anaweza kusoma, haina maana kupoteza muda halafu unapata ziro, bora afenye shughuli nyingine za kumwingizia kipato
 
wakati diamond anamchukua huyo binti alikua ameshaacha shule na alimchukua kama binti wa mitaani.. tukirudi nyuma mbona watoto wadogo wengi tuu wanaonekana kwenye tv na wala maendeleo yao hayajulikani na haijazua mzozo kama hili.. Je unadhani diamond asingemtumia kwa kua ameacha shule?? au mlitaka amsomeshe?? hapo kwanza kumtoa kwenye video ni msaada sana.. wengi walioacha shule na hawana wazazi wanauza miili yao BUGURUNI, sinza na wengine ni machokoraa.. nadhania diamond apewe heshima na pongezi kubwa kwa kumnusuru huyo binti na hayo majanga
Binafsi ni mpenzi wa nyimbo za Diamond ila anapofanya makosa kama haya siwezi kukaa kimya. Hebu msome mtoa mada halafu umuelewe uzuri. Ukumbuke uzembe kama huu ndio unaoleteleza matunda ya Buguruni. Waswahili wanasema Mwanzo wa Ngoma Lele. Kuwatumia watoto kwenye video kwa kufuata taratibu na haki za mtoto hakuna shida. Taabu ipo kwenye suala la KUACHA MASOMO ILI KUTUMIKISHA MTOTO WA SHULE.
Huyu binti aliacha masomo na kuna watu wanataka kuhalalisha kuacha masomo ili kumtumia kujinufaisha kwa maslahi yao. Hivi kwa mfano ikatokea mabinti wengi wakaacha masomo wakaiga anachokifanya huyu binti jamii inyamaze. Natumai ushawahi kuzisikia zipo asasi za kutatea watoto na husasan watoto wa kike ili waweze kufaidi elimu.
Sasa hapa yupo huyu ambaye kuna watu kwa makusudi wanadanganya kwamba alienda kumalizia elimu yake Afrika ya Kusini ili wajinufaishe. Na ukiwauliza kule Afrika ya Kusini alisoma shule gani utasikia wanavyojikanyaga na kutaka huruma kwa Dangote awasaidie. Ninayo hakika Diamond hakufamu kinachojiri nyuma ya pazia kwa huyu binti, kwa kuwa anayo menejimenti inayojitambua.
Natumai wanaohusika na watoto muda sio mrefu lazima utawasikia wakilikemea na kuhakikisha huyu binti anarudi shule na hao wanaomtumikisha ili kujinufaisha wanatakiwa waelewe taratibu za elimu zikoje. Na kwa hili menejimenti ya Diamond lazima isikae kimya kungoja jamii ipige mayowe, lazima watafute namna ya kulitolea maelezo.
 
Kwa maelezo yako nimekuelewa ila kuna upotoshaji mkubwa sana katika hii taarifa mimi nimepata taarifa sahihi kuhusu huyu binti..Na wewe mwenyewe soma hii taarifa vizuri utaelewa naona bado upo GIZANI.. 1.Je unajua video ya kwetu ilitoka lini???? 2. Je umesoma vizuri hapo juu mwalimu mkuu alisema huyu binti aliacha shule lini????Kifupi huyo binti aliacha shule zamani sana kabla hata video ya kwetu haijafikiriwa kutoka wala kutungwa..DIAMOND ALIMCHUKUA HUYO BINTI KAMA MTOTO WA MTAANI TUU na kumwezesha kisanaa na LAZIMA amepewa malipo hivyo hiyo pesa itamsaidia kujikimu maishani..HAWA WATU WA HAKI ZA WANAWAKE na WATOTO NI WAPUUZI NA WANAFANYA KAZI KWA MIHEMKO TUU.
 
sasa nae ana manager.huyo manager anasimamia shughuli gani?
 
Kwani mondi ndi kamuachisha shule!!

Itakuwa elim so kipaj aachwe tuu
 
“Anatupa wakati mgumu kwa kasi hii ya Magufuli sababu hakutoa taarifa kama kaacha au la, tumekuwa tukimtafuta kwa kipindi kirefu, mara tukaanza kumuona kwenye televisheni na magazeti, tupo tayari aje aendelee na kidato cha nne ili apate cheti kimsaidie maishani maana hata miaka 18 hajafika, au huyo Diamond atusaidie kumpata tuzungumze naye.”
Source: Tanzaniatoday

Ukisoma taarifa ya mtoa bango anasomeka kama nilivyokuwekea maandiko mekundu kwamba bado huyu binti hajamaliza masomo na umri wake ni chini ya miaka 18 na mwalimu anatumia busara ya kumuomba Diamond asaidie ili binti amalize masomo. Hizo ni taarifa tunazopatiwa na mtoa bango, je taarifa sahihi ni zipi?
Na kuna sehemu unasema hawa wa Haki za Wanawake ni wapuuzi, hilo jambo sio zuri kwa kuwa wenyewe wanafanyakazi kwa kufuata sheria na misingi ya jamii ilivyo. Hapa kuna mtoto wa kike aliye chini ya miaka 18 watu wanamtumia kujinufaisha na ni watu maarufu, hivi jamii ya kistaarabu inaweza kukaa kimya na kuwaangalia waendelee kuharibu watoto?
Kuna vitu kwa kweli watu wakifuatiliwa kisheria wataanza kulalamika kwamba ni vita katika biashara, kumbe mhusika amekiuka sheria. Juzijuzi tuliona wenye sheria zao wakimkoalia Snura na Chura wake, na leo tunamuona legend wetu akitumikisha vitoto ili kujinufaisha, tukae kimya? Au sheria zina watu wanaohusika lakini wengine mhhh?
Nafikiri tukianza kuzichezea sheria mwishoe kila mtu atakuwa kambare na hakuna wa kumuhukumu mwenzake. Sote ni washabiki na tunamtakia heri Bwana Diamond lakini kwa hili amekosea!

Kwa maelezo yako nimekuelewa ila kuna upotoshaji mkubwa sana katika hii taarifa mimi nimepata taarifa sahihi kuhusu huyu binti..Na wewe mwenyewe soma hii taarifa vizuri utaelewa naona bado upo GIZANI.. 1.Je unajua video ya kwetu ilitoka lini???? 2. Je umesoma vizuri hapo juu mwalimu mkuu alisema huyu binti aliacha shule lini????Kifupi huyo binti aliacha shule zamani sana kabla hata video ya kwetu haijafikiriwa kutoka wala kutungwa..DIAMOND ALIMCHUKUA HUYO BINTI KAMA MTOTO WA MTAANI TUU na kumwezesha kisanaa na LAZIMA amepewa malipo hivyo hiyo pesa itamsaidia kujikimu maishani..HAWA WATU WA HAKI ZA WANAWAKE na WATOTO NI WAPUUZI NA WANAFANYA KAZI KWA MIHEMKO TUU.
 
Foolish age ni jipu kwa kwli!!!!kwa sasa hajui madhara yke atakumbuka shuka kumekucha wamemtumia,wAmemzeesha hana jipya ndo ningejua zinaanzia hpo lol inasikitisha sana kwa maisha ya sasa uschana kz sana!!!!
Tatizo amekosa wa kumwongoza. Mwl amesema mama yake alivokuwa hai alijitahid sn kumfatilia. Shida imeanzia alipofariki mzazi wake. Mungu amsaidie.
 
Mwacheni dunia itamfunza kuparami yalio mzidi umri kama papuchi ni investment kina mama ubaya wangekua na maghorofa yao mjini hapa.
 
Back
Top Bottom