Hulda-Tamarri
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 1,412
- 1,669
Kwani waliosoma wanamiliki ghorofa ? mbona wengi wanaganga njaa tu mtaaniMwacheni dunia itamfunza kuparami yalio mzidi umri kama papuchi ni investment kina mama ubaya wangekua na maghorofa yao mjini hapa.
Watu wanakariri maishaPengine aliona shule imemkataa sasa alazimishe? Akipata zero ndo itamfaidisha??!! Lol
ok KUHUSU MTOTO KUTOMALIZA SHULE NA KUWA BELOW 18- hilo halimuhusu diamond hata kidogo..mtoto aliacha shule zamani na alichukuliwa kama mtoto wa mtaani..je ni watoto wangapi wameacha shule na wapo mtaani au ni huyu tuu anaonekana.Tatizo lipo kwa mtoto na shule(WALIMU WAKE).. je mbona kipindi chote walikua wanamuona mtaani hawakusema lolote mpaka alipotokea kwenye video ya KWETU ndio wanaongea..tafakari hapo.. Huyo mwalimu ni JIPU..alikaa kimya mda wote na cha ajabu anasema anamfahamu huyo mwanafunzi vizuri mpaka mzazi wake,, JE KWA NINI HAKUMFUATILIA KIPINDI CHOTE ALICHOACHA SHULE..hapo nashauri huyu mwalimu MKUU ACHUKULIWE HATUA KALI ZA KISHERIA..ANAFANYA KAZI KWA KUTAFUTA KIKI TUUU..Ukisoma taarifa ya mtoa bango anasomeka kama nilivyokuwekea maandiko mekundu kwamba bado huyu binti hajamaliza masomo na umri wake ni chini ya miaka 18 na mwalimu anatumia busara ya kumuomba Diamond asaidie ili binti amalize masomo. Hizo ni taarifa tunazopatiwa na mtoa bango, je taarifa sahihi ni zipi?
Na kuna sehemu unasema hawa wa Haki za Wanawake ni wapuuzi, hilo jambo sio zuri kwa kuwa wenyewe wanafanyakazi kwa kufuata sheria na misingi ya jamii ilivyo. Hapa kuna mtoto wa kike aliye chini ya miaka 18 watu wanamtumia kujinufaisha na ni watu maarufu, hivi jamii ya kistaarabu inaweza kukaa kimya na kuwaangalia waendelee kuharibu watoto?
Kuna vitu kwa kweli watu wakifuatiliwa kisheria wataanza kulalamika kwamba ni vita katika biashara, kumbe mhusika amekiuka sheria. Juzijuzi tuliona wenye sheria zao wakimkoalia Snura na Chura wake, na leo tunamuona legend wetu akitumikisha vitoto ili kujinufaisha, tukae kimya? Au sheria zina watu wanaohusika lakini wengine mhhh?
Nafikiri tukianza kuzichezea sheria mwishoe kila mtu atakuwa kambare na hakuna wa kumuhukumu mwenzake. Sote ni washabiki na tunamtakia heri Bwana Diamond lakini kwa hili amekosea!
Hivi hapa mzazi ndio kasitisha masomo ya mwanafunzi au mwanafunzi ameacha shule ?, sio kila kitu kutolea mfano magufuli !!Hivi huko sauzi kuna shule za fastafasta? Nakumbuka wakati JPM akitangaza kutoa elimu bure alizungumzia suala la utoro wa wanafunzi shuleni na kukatiza masomo. Huyu mtoto anatakiwa awe wa mfano, serikali ilishatamka kuwachukulia hatua kali wazazi au walezi wanaositisha masomo wanafunzi.
Kuna sharia basi hapa bongo ?, nakumbuka mimi kuna msanii mmoja wa Bongofleva aliwahi kufanya kosa Basata wakatangaza wamemfungia, ghafla akaja onekana kwenye stage akicheza kwenye kampeni za ccm, Basata wakakaa kimya kama vile hawakuwa wamemfungia, hapo angekuwa amefanya jambo kama hilo hilo kiongozi wa chadema ungeona mpaka waziri anaacha kazi zake kufuatilia.Kama unakumbuka vizuri Akon aliwahi kumtumia msichana mdogo kwenye video shooting. Ile issue ilimsumbua sana na hata mauzo ya ile video yalikuwa kiduchu kutokana na kukiuka maadili na haki za watoto.
Kwa hili kama Diamond akigundulika kutumia vijana wa shule kwenye kazi zake, hawezi kukwepa mzigo wa lawama na taratibu za kisheria kama zipo.
Hahah pimpin ain't easyHahaha! Funny part ni pale Pimp anapojiita meneja. Kaazi kweli kweli.