Mrembo kauteka moyo wangu, bila huruma Si kwa bastola, wala kwa pingu ila tabasamu lake

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,080
Reaction score
1,452
NAKEMEA UTEKAJI

Mrembo kauteka moyo wangu, bila huruma
Si kwa bastola, wala kwa pingu ila tabasamu lake.

Alinipiga jicho moja tu, nikajikuta mahabusu,
Nimefungwa kwa pendo kifungo kisicho na msamaha wala rufaa ya kusikika huko juu.

Kila nikiapa nitatoroka, nikimbilie uhuru,
Ananipigia simu na sauti laini, moyo wangu hucheza bila ya biti
Nikimlaumu kwa utekaji, ananijibu kwa utani:
“Mbona ni wewe mwenyewe uliniletea moyo wako kwenye sahani?”

Nimejaribu kutoa malalamiko, nikasema: "Ninakemea utekaji "

Lakini midomo yangu inaniganda, maana penzi limekuwa tamu kama asali ya kijijini.
Wenzangu wakiniona wananiuliza: “Umetekwa au umeamua?”
Nawajibu kwa ujivuni: “Labda vyote viwili, lakini sitaki kuachwa!”

Ndio maana nimesimama hadharani,
Ninapinga utekaji wa kihalifu, si wa mapenzi yenye ladha ya mahaba halisi!

Mrembo,
Basi teketeza kabisa, moyo huu usiwe na njia ya kurudi!

Naumia kwa furaha, napenda mateso haya matamu,
Na kama ni dhambi, basi sisi ni watenda dhambi kwa furaha isiyojutia.

Abuuabdillah ✍️
 
Dah kweli
 
Back
Top Bottom