Kutokana na maelezo niliyosoma kwa global publishers sioni sababu ya kumsakama huyu binti, ameulizwa swali na akajibu kutokana na mtazamo wake.
Siku chache baada ya kuingia kwenye mjengo wa Bunge kuwawakilisha wananchi wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi Sugu ameiteka akili ya Miss Pwani 2010, Zaynab Ally, mrembo mwenyewe amekiri katika mahojiano na gazeti hili.
Miss huyo hakupata shida kuonesha hisia zake kwa mheshimiwa huyo pale alipohojiwa na Paparaza wetu juzi (Jumatano) kuhusu wabunge vijana walioingia bungeni ni yupi kati yao anayemfili toka moyoni.
Kusema kweli nampenda Sugu kwa sababu ni mbunge kijana pia ni msanii, nategemea ataweza kusaidia kutatua matatizo ya wasanii kwa ujumla ikiwa ni pamoja na sanaa ya urembo.
Binafsi ananivutia kwa vile ni mpambanaji mwenye ujasiri, siku zote amekuwa mtetezi wa wanyonge na jamii, hata ukisiliza nyimbo zake utaelewa ninachosema, alisema Zay.
Miss huyo aliongeza kuwa ana imani na bunge jipya lililochanguliwa hivi karibuni kwamba litakuwa na nguvu ya kuisukuma serikali kutekeleza mipango ya maendeleo kwa wananchi.
Kuhusu sanaa ya urembo, Zay ambaye ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao alisema haipaswi kupuuzwa na jamii kwa vile inaongeza uelewa kwa washiriki na kuwasaidia kufikia malengo yao kimaisha"[/B]